Kamati Kuu ya CHADEMA kukutana kwa dharura siku ya Jumamosi

Ni nafasi nzuri kwa EL kueleza yaliyo ongelewa ikulu na kamati kuu kufanya maamuzi sahihi kama inabidi. Swali kuu likiwa "Je mazungumzo yale yanasaidiaje ufanyaji siasa wa CDM na upinzani kwa ujumla au EL alikwenda na yake?"
Akiwaambia alipeleka malalamiko posho na stahili zake za Uwaziri Mkuu zilikuwa hazijaingia kwa mwezi uliopita mtamfanyaje....
 
Shida sio mazungumzo shida yeye kuisifia serikali ya Magu akijua kuna mengi yanaendelea nchini ndivyo sivyo sivyo ndivyo. Amesubiri Lissu ameondoka nchini yeye ndio akagongelee msumari. In other words ' he did stab T Lissu in the back'
Hafai Period!
Nitakalo kujua ni kama kuna alilozungumza na raisi ambalo linaweza kuja kusaidia siasa za upinzani au alikuwa na ya kwakwe tu? Sitaki kuamini kwamba yale tuliyo yaona na kuyasikia kwenye clip ndo hayo tu na hakuna mengine kutoka kwa kinara mmoja wapo wa upinzani aliepata nafasi ya kuongea na raisi. Kwangu mimi mkutano wa CDM kamati kuu ambako EL ni mwanakamati ni muhimu kwani EL atafafanua.
 
Chadema imepoteza mwelekeo.
Ijitafakari na kufanya mabadiriko makubwa ya kiuongozi na kiutendaji.
Mfano. Nafasi ya katibu mkuu imepwaya, mwenyekiti ajiangalie kiutendaji na pia kinapaswa kupunguza mihemko na kujikita kujenga hoja za maana.
isije kuwa hoja kwa bullets
 
Akiwaambia alipeleka malalamiko posho na stahili zake za Uwaziri Mkuu zilikuwa hazijaingia kwa mwezi uliopita mtamfanyaje....
Kwanza mimi siko huko, nitakacho ni kuwa na upinzani wenye nguvu na imara haijalishi kama ni chama gani. Pili sitarajii kiongozi wa upinzani apate nafasi adimu ya kwenda kuzungumza na raisi aishie kulalamikia posho na stahiki zake nyingine. Mtu wa namna hiyo hafai kuwa kiongozi wa upinzani nionavyo mimi. Sina la kufanya zaidi ya kuamua kura yangu niipeleke wapi.
 
ha ha ha ha kuna rafiki zangu kadhaa siku hizi utasikia wanasema ntakosa imani na CDM kama tundulisu akihama, ila lowasa kwa mm japo ni mtu sikumpenda kuingia chadema ila kwa kitendo cha juzi

sjaona kosa lake maana ka specify kabisa baadhi ya vitu alivyo sifia na hakusema vyote kwa huyo Mbowe na wenzake walitegemea akifika pale amwambie rais kuwa ww umetuma watu kumpiga risas tundulisu au rais kwann umetukataza kufanya mikutano au kwann watu wanatekwa na wengine kupotea na ww hutoi tamko.

Jamani jamani ebu tuwe serious ata kama angekuwa ni asingeweza kuropoka hivyo mbele ya rais ila mkimuondoa CHADEMA haina neno lowasa ana mtaji wa watu atatengenea chama na atagombea tena urais 2020.
 
Kamati kuu ya chama pendwa CHADEMA, inatarajiwa kukutana kwa dharura siku ya Jumamosi Tarehe 13.01.2018. Mtoa taarifa hajaeleza kwa kina agenda za kikao hicho cha siku moja zitakuwa zipi.
Wafukuze lowasa wadaiwe hela zake nabushahid u shahid upo kwa bordgurd wake
 
Kwanza mimi siko huko, nitakacho ni kuwa na upinzani wenye nguvu na imara haijalishi kama ni chama gani. Pili sitarajii kiongozi wa upinzani apate nafasi adimu ya kwenda kuzungumza na raisi aishie kulalamikia posho na stahiki zake nyingine. Mtu wa namna hiyo hafai kuwa kiongozi wa upinzani nionavyo mimi. Sina la kufanya zaidi ya kuamua kura yangu niipeleke wapi.
Pole sana,

Ebu tuambizane kidogo,hivi uliamini na bado unaendelea kuamini kuwa Lowasa ni mpinzani kweli ..... !

Lowasa baada ya kukatwa alijua alishapoteza lakini waliosababisha apoteze ni Chadema na ccm,kwa upande wa ccm akaona asiendelee kutunishiana nao misuli.

Kwa vile Chadema walizunguka nchi nzima wakimtangaza kuwa ni fisadi aliamua kuwatumia haohao ili wamsafishe hadi atakate na kwa kujua ni waroho,mbele ya pesa hawachomoi. Kweli hayawi yakawa,Lowasa akapokelewa usiku na asubuhi akatangazwa mgombea kupitia ukawa.

Welevu walisusa kimyakimya,wajinga tukapaza sauti lakini pesa isikie tu kwa mwenzio, nani angeamini kwamba Lisu,Mbowe,Lema,Msigwa na Sugu kuna siku wangemuona Lowasa ni mfalme...!

Hakuna kitu kilikuwa kikiniudhi kama kuwaona wakimnadi Lowasa kwamba mchapakazi na mwàdilifu,sikutaka tena maishani mwangu kuwa mwanachadema hadi pale Lowasa atakapoondoka.

Na Mpaka sasa suala la kusafishwa kwenye ufisadi kupitia Chadema limefanikiwa kwa 100% na kilichobaki atatangaza kustaafu siasa huko huko japo hajawahi kuwa mwenzenu.
 
4U movement aka "Alipo tupo" andaeni desa la kumpa mzee wenu ajieleze. Sisi tumeshapenya mpaka ikulu kusaka mazungumzo. Imebaki kulimwaga pilau kwenye sinia watu wale!
 
Kamati kuu ya chama pendwa CHADEMA, inatarajiwa kukutana kwa dharura siku ya Jumamosi Tarehe 13.01.2018. Mtoa taarifa hajaeleza kwa kina agenda za kikao hicho cha siku moja zitakuwa zipi.
IMG-20180110-WA0008.jpg
 
Pole sana,

Ebu tuambizane kidogo,hivi uliamini na bado unaendelea kuamini kuwa Lowasa ni mpinzani kweli ..... !

Lowasa baada ya kukatwa alijua alishapoteza lakini waliosababisha apoteze ni Chadema na ccm,kwa upande wa ccm akaona asiendelee kutunishiana nao misuli.

Kwa vile Chadema walizunguka nchi nzima wakimtangaza kuwa ni fisadi aliamua kuwatumia haohao ili wamsafishe hadi atakate na kwa kujua ni waroho,mbele ya pesa hawachomoi. Kweli hayawi yakawa,Lowasa akapokelewa usiku na asubuhi akatangazwa mgombea kupitia ukawa. Welevu walisusa kimyakimya,wajinga tukapaza sauti lakini pesa isikie tu kwa mwenzio, nani angeamini kwamba Lisu,Mbowe,Lema,Msigwa na Sugu kuna siku wangemuona Lowasa ni mfalme...! Hakuna kitu kilikuwa kikiniudhi kama kuwaona wakimnadi Lowasa kwamba mchapakazi na mwàdilifu,sikutaka tena maishani mwangu kuwa mwanachadema hadi pale Lowasa atakapoondoka.

Na Mpaka sasa suala la kusafishwa kwenye ufisadi kupitia Chadema limefanikiwa kwa 100% na kilichobaki atatangaza kustaafu siasa huko huko japo hajawahi kuwa mwenzenu.
Hapa siangalii ufisadi au vinginevyo kuhusu Lowasa ninachosema mimi kama yeye ni kiongozi "mkuu" CDM na akapata nafasi ya kuongea na raisi-amesogezaje ajenda ya chama chake mbele? Kama ameshindwa kufanya hivyo basi chama kitaamua.
 
Mgombea A: "wewe ni kiongozi mstaarabu sana. Uliendesha kampeni za kistaarabu kweli maana sikukusikia ukinitukana hata mara moja. Isipokuwa wapambe wako ndio niliwasikia wakiporomosha kampeni za matusi. Au uliwatuma?" Jibu toka Mgombea B: Hapana. Halafu kimya.

Ningekuwa mimi Mgombea B pia ningemuuliza: "Na wewe ulipokuwa unafanya push up ulinilenga mimi? Pili, japo sikukusikia unatoa matusi lakini wapambe wako walinitukana matusi hadi ya nguoni, je uliwatuma?"
 
Kamati kuu ya chama pendwa CHADEMA, inatarajiwa kukutana kwa dharura siku ya Jumamosi Tarehe 13.01.2018. Mtoa taarifa hajaeleza kwa kina agenda za kikao hicho cha siku moja zitakuwa zipi.
Ni vizuri wasiende kumlaumu Lowassa hapo kwa kukutana kwake na Rais. Chama kimeshindwa kufanya juhudi zozote za kukutana na Rais kufanya dialogue ya aina yoyote kumpongeza au kuwasilisha malalamiko/mapendekezo yao kama yapo. Katika hali ngumu ya kushindwa kuonana na Rais kama kikundi/chama hakukuwa na namna nyingine kwa Mh. Lowassa kutafuta mbinu mbadala ya kukutana na Mh. Rais kama alivyofanya. Akapongezwe badala ya kulaumiwa.
 
img-20180110-wa0008-jpg.673070

Hii picha inajieleza kwa kila kitu...!!!
Lowassa na Magufuli wanachekelea JINSI WAPINZANI WANAVYONYANYASWA. Pengine hapa Magufuli alimwambia Lowasa,'' Tundu Lissu anajifanya kijogoo wa Upinzani tumeshamtengeneza bahati yake saa hizi angelikuwa kwa udongo na akirudi toka Ulaya ataufyata. Kuna yule alikuwa anafuatilia uhalalai wa PhD yangu naye nimempoteza. Halafu kuna huyu mwandishi wa Mwananchi anaitwa Azory Gwanda, alikuwa anaandika andika habari za kiuchunguzi kuhusu mauaji huko Kibiti na kuichafua Serikali yangu naye nimempoteza. Mimi sijaribiwi Bwana...kwikwikwikwiiiiiiiiiiiiiii...!!!
 
Kikao hiki kisimhusu Lowassa. kinaweza Sababisha Chadema chama kisichoweza kukumbuka jinsi kilivyoshauriwa. na kitasababisha mpasuko mkubwa sana ndani ya chama hiki.
 
Back
Top Bottom