Kamati Kuu ya CCM yawapitisha Job Ndugai, Dkt. Tulia Mwansasu na Abdullah Mwinyi kugombea Uspika

Mpaka zoezi linaisha alikuwa amerudisha Zungu tu..Baadae utaratibu ulibadilishwa na muda wa kuchukua fomu ukaongezwa Chifu..


Naibu spika lazima awe mwanamke kwa kufuata gender, kwa sababu wagombea wote waliojitokeza nafasi ya spika ni wanaume kuhusu zungu mdahalo umefungwa umeelewa?
 
Kwa nn? Usishangae viti maalum vya ukawa ndugu
...ukawa hawatawali nchi....wenye kututawala ni ccm na ndio ninaowazungumzia...kama ukawa wangekuwa watawala na kutufanyia hivi ningesema vile vile....'nepotism' kwenye utawala ni janga.....nenda ukajifunze....
 
...ukawa hawatawali nchi....wenye kututawala ni ccm na ndio ninaowazungumzia...kama ukawa wangekuwa watawala na kutufanyia hivi ningesema vile vile....'nepotism' kwenye utawala ni janga.....nenda ukajifunze....

so wanaamua kuwekana kienyeji bungeni kisa hawa tawali nchi ,nilipenda kuona vyama vya upinzani vinafanya upitishwaji wa wabunge wao kwa wazi yani wanashindanisha watu wenye sifa kula za maoni ndio ziwe zinazungumza sio kisa kubenea kawa mbunge basi mkwe mbunge wa viti maalum ina maana ukawa haina watu wengine wenye uwezo
 
Nilijua mtoto wa Mwinyi lazima apite!

Sijui hata kaibukia wapi huyu!

Ni mwendo wa kila mtu kuisoma namba.

CCM ni ile ile!

Sitta tunakusubiri uende mahakamani.

Kaka kama mtu anapenda kazi ya baba mta mkataza ,ndio maana ukiuliza watoto wengi unataka kazi gani atakwambia kama ya baba so watanzania tuwe waelewa kidogo ...
 
Naipongeza Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi kwa kukata jina la mgombea usipika wa Bubge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Samwel Sitta.

Watanzania bado tuna makovu juu ya Samwel Sitta alivyoendesha bunge la Mabadiliko ya Katiba na kuua mustakabali wa nchi kupata Katiba mpya iliyotokana na maoni ya wananchi.

Kwa kujiamini akafikia hatua ya kuwatolea lugha ya kejeri watumishi wa mungu wakiwemo maaskofu.

Namshukuru mwenyezi mungu kwamba fimbo ya mussa imeweza kumpiga bakora akiwa bado hai hapa duniani ili apime kwa namna alivyoshiriki na kusimamia kuzika matumaini waliyokuwa nayo wananchi.

Amekatwa kwenye Urais na sasa amekatwa kwenye Usipika. Hakuna mtu aliyejiamini kama Goliat na ufalme wake lakini ilipofika tamati dola yake iliangushwa. Anguko analopata Samwel Sitta ktk medani ya siasa liwe fundisho kwa watu wenye matendo yanayofanana na hayo.
 
Back
Top Bottom