Kamati kuu ya CCM isirudie makosa kupitisha Wagombea ubunge wasio na uwezo

Tukiandika humu na kwingineko kuwa CCM ni kansa inayotafuna Tanzania,mnaleta porojo zenu.

Niambie toka moyoni mwako na kwa akili na uelewa ule aliokupa Mwenyezi Mungu aliyekuumba, bungeni wabunge waelewa na wenye msaada kwa Tanzania wanazidi 20!!?

Walipitishwa na nani!?

Walishindaje!?
Ningependa nilione jibu la hili swali kutoka kwa mama D ni swali zuri sana.
 
Ningependa nilione jibu la hili swali kutoka kwa mama D ni swali zuri sana.

Hao chadema wangekua hawakumchukua lowasa aliyekatwa ccm na kumsafisha na kumpa dhsmana ya kushika dola ningekua na jibu la kuwapa

Vinginevyo naona hizo ni blahblah tuu
 
Hao chadema wangekua hawakumchukua lowasa aliyekatwa ccm na kumsafisha na kumpa dhsmana ya kushika dola ningekua na jibu la kuwapa

Vinginevyo naona hizo ni blahblah tuu
Sijaona neno CHADEMA kwenye swali la muulizaji. Hiyo chadema imekujaje mkuu?
 
Hao chadema wangekua hawakumchukua lowasa aliyekatwa ccm na kumsafisha na kumpa dhsmana ya kushika dola ningekua na jibu la kuwapa

Vinginevyo naona hizo ni blahblah tuu
2015 nilisoma makala nyingi za wakongwe kina Joseph Mihangwa, Jenerali Ulimwengu, Padri Karigendo na waandishi wengine kwenye gazeti la Raia mwema kuhusu CHADEMA kumchukua Lowasa, wale wazee hawakuafiki kabisa na wakatoa tamko kwamba usalama wa CHADEMA ni kushinda tu ule uchaguzi vinginevyo wamekimaliza chama. Sasa hivi utabiri wao unatimia.
 
Sijaona neno CHADEMA kwenye swali la muulizaji. Hiyo chadema imekujaje mkuu?
Uzi unaijadili CCM na wachangiaji wanajaribu kuona kama kuna mbadala ila ukweli ni kwamba Chadema kama chama cha siasa hawana uwezo wa kuleta badiliko lolote chanya

2015 nilisoma makala nyingi za wakongwe kina Joseph Mihangwa, Jenerali Ulimwengu, Padri Karigendo na waandishi wengine kwenye gazeti la Raia mwema kuhusu CHADEMA kumchukua Lowasa, wale wazee hawakuafiki kabisa na wakatoa tamko kwamba usalama wa CHADEMA ni kushinda tu ule uchaguzi vinginevyo wamekimaliza chama. Sasa hivi utabiri wao unatimia.

Chadema ilijifia pale pale diranqhe kilichobakia ni sacco isiyofuata kanuni za saccos
 
KAMATI KUU YA CCM ISIRUDIE MAKOSA KUPITISHA WAGOMBEA UBUNGE WASIO NA UWEZO.

Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi... mjibu kwa pamoja CHAMA KIENDELEE. Leo nimekuja na ishu inayohusu chama pendwa na kilichobeba matumaini ya kila mtanzania ukiwemo wewe unayesoma huu uzi. Kuna mambo hayajakaa sawa hivyo mimi kama mwanachama nisiye na cheo chochote nimeona nitumie jukwaa hili kutia mawazo yangu. Ninaamini hapa kuna viongozi wengi wa chama wanasoma.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ninapenda kusisitiza kamati kuu ya chama ijiepushe kabisa na hawa wagombea ubunge wenye uwezo mdogo kielimu na kwenye kujenga hoja. Kwa miaka mingi kamati kuu imekuwa mbele sana kifikra kuzidi wanachama au hata watanzania wengi. Sisi wote ni mashahidi kwenye chaguzi nyingi jina likienda Dodoma halirudi. Yaana CC ya CCM huwa inakata majina hata kama limepita ngazi ya wilaya. Wengi wetu tumekuwa tukilalamika na kuona kama viongozi wa huu hawapendi demokrasia. Wale wajumbe wa kamati kuu kiukweli walikuwa mbele sana ya muda ndo maana maamuzi yao yalikuwa yakiepusha shari nyingi.

Kiini cha uzi huu ni hasira zangu nilizo nazo baada ya kuona baadhi ya wabunge wa CCM wakitoa hoja dhaifu na za ovyo mno. Kwa mara ya nyingine tumeona mbunge Shigongo akija na madai ya ovyo mno kuwahi kutolewa na mbunge makini wa CCM. Mara ya kwanza kusikia udhaifu wa hoja za Shigongo ni pale alipodai kuwa watu wapate nafasi ya kusoma degree bila kupitia kidato cha nne. Hoja yake ilipanguliwa kisomi na waziri Ndalichako. Wiki hii kaja kwa kutaka wananchi tufunge mikanda kama miaka ile baada ya vita ya Kagera ili serikali ipate tozo kupitia miamala ya simu.

Erick angekuwa mzalendo angefunga mkanda kwanza yeye kwa kukatwa mshahara wake kwa 100%. Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari akasema Rais awaondoe mkurugenzi wa Buchosa na idara ya uhasibu isipokuwa mweka hazina. Sababu ya kufanya hivyo anadai ni ubadhirifu wa pesa za umma. Huu ni ujinga wa hali ya juu kuwahi kutamkwa na mtu kama Shigongo aliyejijengea heshima kubwa kabla hata ya ubunge.

Itoshe kusema huyu mbunge hajui kazi ya baraza la madiwani, RAS, na Wizara ya TAMISEMI. Pia inaonekana hana ushawishi kwenye baraza la madiwani ndo maana inakuwa ngumu kwake kumwadabisha DED. Kauli yake ya kutaka mwekahazina aachwe pia ni ishara ya kuwepo maslahi binafsi kwenye jambo lake. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari ni wazi kwamba huyu mbunge hakustahili kuwepo bungeni.

Mimi naisihi sana kamati kuu ya Chama iendeleze weledi wake kwenye kukata majina ya vilaza wote wataobahatika kufikisha majina yao Dodoma 2025. Hawa wabunge wengi wa aina hii wanaweza kupitisha sheria za ovyo sana bungeni kitu ambacho kitaiweka CCM kwenye wakati mgumu sana mbele ya wapiga kura wake.
Wote hawana uwezo Sasa watamuweka nani?
 
Back
Top Bottom