Kamati kuu ya CCM isirudie makosa kupitisha Wagombea ubunge wasio na uwezo

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,212
22,266
KAMATI KUU YA CCM ISIRUDIE MAKOSA KUPITISHA WAGOMBEA UBUNGE WASIO NA UWEZO.

Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi... mjibu kwa pamoja CHAMA KIENDELEE. Leo nimekuja na ishu inayohusu chama pendwa na kilichobeba matumaini ya kila mtanzania ukiwemo wewe unayesoma huu uzi. Kuna mambo hayajakaa sawa hivyo mimi kama mwanachama nisiye na cheo chochote nimeona nitumie jukwaa hili kutia mawazo yangu. Ninaamini hapa kuna viongozi wengi wa chama wanasoma.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ninapenda kusisitiza kamati kuu ya chama ijiepushe kabisa na hawa wagombea ubunge wenye uwezo mdogo kielimu na kwenye kujenga hoja. Kwa miaka mingi kamati kuu imekuwa mbele sana kifikra kuzidi wanachama au hata watanzania wengi. Sisi wote ni mashahidi kwenye chaguzi nyingi jina likienda Dodoma halirudi. Yaana CC ya CCM huwa inakata majina hata kama limepita ngazi ya wilaya. Wengi wetu tumekuwa tukilalamika na kuona kama viongozi wa huu hawapendi demokrasia. Wale wajumbe wa kamati kuu kiukweli walikuwa mbele sana ya muda ndo maana maamuzi yao yalikuwa yakiepusha shari nyingi.

Kiini cha uzi huu ni hasira zangu nilizo nazo baada ya kuona baadhi ya wabunge wa CCM wakitoa hoja dhaifu na za ovyo mno. Kwa mara ya nyingine tumeona mbunge Shigongo akija na madai ya ovyo mno kuwahi kutolewa na mbunge makini wa CCM. Mara ya kwanza kusikia udhaifu wa hoja za Shigongo ni pale alipodai kuwa watu wapate nafasi ya kusoma degree bila kupitia kidato cha nne. Hoja yake ilipanguliwa kisomi na waziri Ndalichako. Wiki hii kaja kwa kutaka wananchi tufunge mikanda kama miaka ile baada ya vita ya Kagera ili serikali ipate tozo kupitia miamala ya simu.

Erick angekuwa mzalendo angefunga mkanda kwanza yeye kwa kukatwa mshahara wake kwa 100%. Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari akasema Rais awaondoe mkurugenzi wa Buchosa na idara ya uhasibu isipokuwa mweka hazina. Sababu ya kufanya hivyo anadai ni ubadhirifu wa pesa za umma. Huu ni ujinga wa hali ya juu kuwahi kutamkwa na mtu kama Shigongo aliyejijengea heshima kubwa kabla hata ya ubunge.

Itoshe kusema huyu mbunge hajui kazi ya baraza la madiwani, RAS, na Wizara ya TAMISEMI. Pia inaonekana hana ushawishi kwenye baraza la madiwani ndo maana inakuwa ngumu kwake kumwadabisha DED. Kauli yake ya kutaka mwekahazina aachwe pia ni ishara ya kuwepo maslahi binafsi kwenye jambo lake. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari ni wazi kwamba huyu mbunge hakustahili kuwepo bungeni.

Mimi naisihi sana kamati kuu ya Chama iendeleze weledi wake kwenye kukata majina ya vilaza wote wataobahatika kufikisha majina yao Dodoma 2025. Hawa wabunge wengi wa aina hii wanaweza kupitisha sheria za ovyo sana bungeni kitu ambacho kitaiweka CCM kwenye wakati mgumu sana mbele ya wapiga kura wake.
 
Duh haya bwana .sema huyu jamaa baada ya kusikia zile riwaya zake alikuwa n copy and paste kutoka kwa waandishi nguli wa huko ulaya nilisikitika sana .nikajua ni kipaji chake cha asili kutunga ile mikasa kwenye stori zake kumbe......anyway labda wana msingizia tu wasiompenda.ila kama ni kweli ameniangusha sana yaani
 
Duh haya bwana .sema huyu jamaa baada ya kusikia zile riwaya zake alikuwa n copy and paste kutoka kwa waandishi nguli wa huko ulaya nilisikitika sana .nikajua ni kipaji chake cha asili kutunga ile mikasa kwenye stori zake kumbe......anyway labda wana msingizia tu wasiompenda.ila kama ni kweli ameniangusha sana yaani
Aisee jamaa ana kipaji cha kutunga stori... hata kama kuna copy & paste ni kiasi tu. Kwenye ubunge na mambo ya kisomi ndo dhaifu
 
Duh haya bwana .sema huyu jamaa baada ya kusikia zile riwaya zake alikuwa n copy and paste kutoka kwa waandishi nguli wa huko ulaya nilisikitika sana .nikajua ni kipaji chake cha asili kutunga ile mikasa kwenye stori zake kumbe......anyway labda wana msingizia tu wasiompenda.ila kama ni kweli ameniangusha sana yaani
Huyo ni tapeli tupu
 
Na wewe pia.

Unacheka mazuri hayo?

Inaonekana mwenzako kaandaliwa desa, waliomuandalia wamekosea badala ya kuandika 3.9% wameandika 39%, na yeye kameza nzimanzima bila kumung'unya.

Nimechaka sanaaaa 😂😂😂😂😂lol
 
Ikumbukwe kamati iliwalongeza wabunge wao kwa kupitisha bajeti hii kwa kishindo .
Mjadala unaweza kuanzia hapo kama hamtojali
 
Nimecheka kwa nguvu katikati ya watu wenye huzuni

Jioni njema Kiranga
Tukiandika humu na kwingineko kuwa CCM ni kansa inayotafuna Tanzania,mnaleta porojo zenu.

Niambie toka moyoni mwako na kwa akili na uelewa ule aliokupa Mwenyezi Mungu aliyekuumba, bungeni wabunge waelewa na wenye msaada kwa Tanzania wanazidi 20!!?

Walipitishwa na nani!?

Walishindaje!?
 
Acha mambo ya ajabu wewe
Sasa kati ya mimi na wewe ambae unawasingizia na kuwasukumizia kuwa wabunge wa CCM kama hawa wana uwezo ni nani ana mambo ya ajabu?
109_20210722_043703.jpg
 
Back
Top Bottom