Sijaelewa mpaka sasa kwanini mnadharau maoni ya wanachama, hayo tumezoea kuyaona CCM ambako CCM walifika hatua ya kukanyaga maoni ya wanachi katika katiba mpya halafu UKAWA ikakataa.
Wanachama wameendesha kura za maoni katika majimbo, wamechagua wawakilishi wao. Bila kuwaeleza lolote, mnaamua kuwatoa wawakilishi waliochaguliwa na wanachama mnawaweka wengine, tena wasio na ushawishi wowote. Hebu angalia Kishapu, Mpendazoe hakubaliki, mmemuweka, tunapoteza jimbo, Kule Ludewa, mgombea aliyekuwa anakubalika mmemuacha, Tabora, Muleba kusini, Monduli, Hivi nani amewaroga? Au alipoondoka mzee asiyeweza kuhongwa Dr. Slaa sasa CCM imefanikiwa kupenya na kuamua kutibua utaratibu mzima? Inakuwaje mnawapuuza wananchi waliopigania chama katika majimbo hadi chama kikawa tishio leo hii hamthamini jasho lao?
Jeuri ya kukubalika hampaswi kuitumia vibaya. Wananchi wakiishaamua jambo, kama halina dalili ya usaliti waache. Sasa tuna uwezekano wa kupoteza majimbo mengi sababu ya maamuzi yenu ya kipuuzi. Nauliza tena nani kawaroga? Pamoja na wananchi kuichoka CCM haimaanishi kuwa hata kile anachokitaka umnyang'anye. Hapo mmekosea tena sana. Mnyika, Lisu, na Salim Mwalimu, hapo mmekatisha tamaa wananchi.
Mnyika, Lisu na wengine wote tokeni hadharani mtueleze ni vigezo gani mmetumia kukata majina ya watu wanaokubalika majimboni ? Hii ni keroo kubwaaa saaana!