Kamata ya Diamond Platnumz ni ngoma mbovu mno, jamaa kaishiwa ubunifu

Ngoma mbovu kinoma..
Ndani matusi matupu watu siku wanaona njia ya kuwakamata nikuimba matusi hii nyimbo ina matusi ya dhahiri kuliko hata ile Nyegezi ambayo sikuona hata sababu ya kufungiwa kwa kuwa haikuwa mbaya kwenda kuifungia ila hii nimeisikiliza mara moja na sidhani kama kuna mtu anaweza kuisikiliza na watoto au watu anaowaheshimu.
 
Swala la wana-mziki naona kama wakati wa kuingia kwenye tasnia huwa wanawatafuta watunzi waliotulia au wanaiba melody za nchi za nje na nyimbo zinatoka vizuri. Wakishapata umaarufu wakakubalika wanaachana na watunzi wanaanza kutunga wenyewe matokeo yake ndo haya.

Ili kuweka sawa hali ya hewa ni kwamba hata KIBA ukisikia mashairi ya wimbo wa Sindelela ni tofauti na zilizofuata; Sikia mashairi ya wimbo wa Jide 'machozi' halafu sikia 'ze ndindindi'. Huyu Mondi msikilize mashairi ya wimbo wa 'mbagala' halafu sikia uchafu wa jejejejejejejejeeee.
Wasanii msije kusema kwamba sikuwaambia............. rudi kwa watunga mashairi ninyi mbaki kuwa waimbaji.
 
Mlio karibu na Sadala mshaurini kama upeo wake umefika mwisho kwenye kutunga mashairi atafute watu wenye idea mpya wamwandikie yeye abaki kuimba tu.

Msisahau jana King kaachia Good music akiwa kamshirikisha Rude Boy ngoma inaitwa Salute
Yaan wew unaeona mashahiri ya diamond ni mabaya na ya alikiba ni mazuri wew ni nani? Ni jaji?(maana hata jaji mwenyewe ni binadamu. Kimsingi wew hater wa diamond)

tega masikio usikie ndugu yangu "muziki ni hisia" muziki unaouona mbaya ni hisia zako na huyo mwingine ambae anaona mbaya(yupo anaeuona mzuri na c shabiki wa kiba wala diamond)

Acha ulafaa aisee
 
Back
Top Bottom