Kamara Kusupa: Rais amepata wa kuendana naye. Je, ataacha kulalama?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
RIDHIWAN KIKWETE HANA SIFA ZA KUITWA WAZIRI WA WATANZANIA

(i) "HATIMAYE MAMA AMEPATA AINA YA WATU WA KWENDA NAYE”

(ii) "JE, ATAACHA KULALAMIKA? ATAACHA KUTOA VISINGIZIO VYA KUSHINDWA?”

Rais anao uwezo aliopewa na katiba wa kumteua yeyote kushika nafasi za wateule wa Rais, lakini huo uteuzi wa Ridhiwan Kikwete siyo wa kunyamaziwa. Hata Watanzania wakinyamaza iko siku mawe yatapiga kelele!

Kwa sababu Ridhiwan Kikwete hana sifa za kustahili kuitwa Waziri wa Watanzania, kwakuwa ameteuliwa ataendelea kuwa waziri wa serikali ya MAMA. Muda nao utasema serikali ya MAMA Samia ni serikali ya namna gani!

1. Nyerere alipokuwa madarakani kuna matukio mawili yaliyotokea, ningali nayakumbuka. Waziri wake wa muda mrefu Chediel Yohana Mgonja aliyekuwa pia Mbunge wa Same, alikuwa na vituko kwenye uwaziri wake, katika makala hii sitavisimulia.

2. Nyerere aliwavumilia sana walio kwenye “cream” ya uongozi wake, hakupendelea kumtupa nje kabisa ya mfumo mtu yule aliyezijua siri za serikali yake.

3. Lakini ulifika wakati wananchi wa Same walimchoka Chediel Mgonja, wakamwangusha kwenye uchaguzi. Nyerere asingeweza tena kumpa uwaziri Bw. Mgonja. Lakini ili kumsitiri na kum’bakisha kwenye tabaka la wateule, Nyerere alimteua Mgonja kuwa Mkuu wa mkoa. Wananchi kwenye mkoa huo wakaja juu “sisi siyo wa kutupiwa viongozi waliokataliwa”

4. Bahati nzuri Nyerere pamoja na wengine kumvika sifa ya kuitwa dikteta, lakini alikuwa na sifa mbili ambazo mimi niliona zilimfanya awe binaadamu anayezidi kawaida “extra ordinary person”

5. Nyerere alikuwa “msikivu” na “mvumilivu.” Mtu angeweza kumsemea ovyo uso kwa uso na Nyerere akabaki kumtazama tu! Wakati wengine wakihofia mtukanaji atakamatwa na kutiwa msukosuko, wanashangaa anendelea na maisha! Wengine wakitaraji labda atafukuzwa kazi wanashangaa “mtukanaji” anaendelea na kazi.

6. Mzee Waikela wa Tabora anaweza kuwa shahidi aliye hai, mwaka 1968 alimsimanga Nyerere hadharani, akamfedhehesha na kumwaibisha. Maneno yale ya Waikela angemwambia Rais Idd Amin Dada wa Uganda, ama angemwambia Sheikh Abeid Amani Karume Rais wa Zanzibar au angemwambia Rais Ahmed Seiko Toure wa Guinea, asingechukua masaa, angemalizwa haraka! Lakini kwa Nyerere ikawa “mnh!!” hadi leo Waikela yupo na mara kadhaa huusimulia huo ujasiri wake alivyomsuta Nyerere hadharani.

7. Mwingine ni rafiki yangu Oswald Mashaka Nindi Chimoto (sasa marehemu) wakati huo akitumika kuwapiga msasa wanaoteuliwa na Rais kuwa viongozi, ili waijue Itikadi ya chama na maadili ya uongozi, Chimoto alisema na walioteuliwa kuwa Wakuu wa wilaya.

8. Zamani hizo aliyeteuliwa na Rais “Presidential appointment” ilibidi kwenda Kivukoni kupigwa msasa kwa siku 90. Basi kwenye darasa hilo, Chimoto akasema maneno mengi ya hovyo dhidi ya Nyerere, anavyoteua wasiokuwa na uwezo. Waliomsikiliza walichukizwa, nadhani Chimoto kabla hajaanza darasa alikunywa vikali, katika yawezekana aliyasema yale akisukumwa na ulevi.

9. Baadaye mashushushu walimfikishia taarifa Nyerere, kwamba “leo umetukanwa sana sana na Chimoto” akapewa mkanda wa maneno ya Chimoto. Naye Chimoto alipopata habari kuwa ameshitakiwa kwa Rais, alisema “mimi nimemtukana Nyerere kichama, siyo kiserikali, tutaonana kwenye chama.”

10. Hata hivyo Chimoto hakuadhibiwa bali inaonyesha Nyerere alinong’ona na Katibu Mkuu wake Rashid Kawawa, kisha kisirisiri “wakawa -mark all political rioteers” wakawaweka kwenye uangalizi mkali wa Kawawa.

11. Kuhusu Mgonja, wananchi walipomwonyesha Nyerere kwamba uteuzi wake umewakera, alikuwa msikivu, alitengua, akawapelekea Mkuu wa mkoa mwingine!

12. Tukio la pili lilimhusu Paul Bomani ambaye naye alikuwa Waziri mwandamizi kwenye serikali ya Nyerere kwa muda mrefu. Baba yake mzazi wa Bomani, kwasababu ya kulewa madaraka ya mwanawe na kiburi cha utajiri, aliwaropokea Wasukuma wenzake akisema katika Tanzania hii wanaojua kuzaa ni wawili tu, yeye na baba yake Nyerere!

13. Wasukuma walikerwa na kauli hiyo, wakaambizana na kukubaliana kumwangusha Paul kwenye uchaguzi, baada ya uchaguzi mkuu kupita Paul Bomani alianguka, sikumbuki Nyerere alimpa wadhifa gani. Lakini hilo liliwakera zaidi Wasukuma.

14. Siku moja Nyerere akiwa ziarani Mwanza, mtu mmoja alipangwa, akapanda ghorofani akiwa na bunduki yake, tayari “kumdungua” Nyerere atakapokuwa mkutanoni.

15. Lakini mtu mmoja aliyeshiriki mpango huo, alipata wazo tofauti, kwanini tumuue Nyerere wetu? Si tumwambie ukweli tu? Akikataa ndipo tumdungue! Akawaambia wana usalama kwamba kule ghorofani kuna mtu ana bunduki tayari kumuua Nyerere.

16. Wana usalama walimpandia wakamkuta kweli anayo bunduki, wala hawakutumia nguvu, walimwambia shuka chini upesi, uende ukamwambie mwenyewe, Nyerere yuko chini anakusubiri.

17. Huyo mtu alipomfikia Nyerere, alieleza yote kwamba hakuwa peke yake, bali ule ni mpango wa Wasukuma kwasababu, umetuudhi sana, pia umetudharau kwa kumpa cheo mtu ambaye sisi tumemwadhibu kwa kumnyima kura.

18. Nyerere hakufanya hiana, akawaagiza wasaidizi wake kwamba atakapomaliza mkutano wake, wamkusanyie wazee wa Mwanza kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa kuanzia saa 9.00 Alasiri hadi 11.00jioni. Kwenye kikao hicho Nyerere aliwaomba radhi wazee wa Kisukuma akisema hata yeye angekuwa Msukuma asingempa kura Paul, akawaahidi kulirekebisha suala hilo na mambo yakaishia hapo.

19. Kuhusu Rais Samia, hakuna mtawaliwa atakayemwambia kwenye serikali yake amteue nani wala amwondoe nani. Lakini hatimaye Watanzania walio wengi na walio makini watajua serikali yake ni serikali ya namna gani!

20. Nimeona mtandaoni kipande cha video inayomwonyesha Makamu wa Rais wa awamu ya tano, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi kwenye kampeni. Samia huyo alisema “kuhusu umeme mlikuwa mnaunganishiwa kwa shs laki tatu na elfu ishirini, lakini sisi tumeshusha hadi elfu ishirini na saba. Hii ndio CCM!” Kisha kuna video nyingine inayonukuu hotuba ya Rais Samia akiunanga huo uamuzi wa kuwaunganishia umeme kwa shs. 27,000/= Ajabu ya Samia Rais kumkanyaga Samia Makamu wa Rais, wakati serikali ni ikiwa ya chama kile kile!

21. Wanaomwambia Samia ni Rais wa awamu ya sita wanamdanganya mchana kweupe, wakimsadikisha uwongo mweupe!

22. Ukweli ni kwamba Samia ni Rais wa sita kwenye awamu ya tano, amekabidhiwa kijiti ili aifikishe ngwe ya pili mwisho wa safari yake 2025. Bado awamu ni ile ile, bado serikali ni chama kile kile CCM. Bado sera za chama ni zile zile na Ilani iliyowaingiza madarakani ni ile ile.

23. Hayo mabadiliko ya “U – turn” anayoyafanya inabidi Samia mwenyewe ajiulize na ajipe jibu mwenyewe, kwamba anamwasi nani? Anamkomoa nani? Anayafanya hayo kwa manufaa ya nani?

24. Ikiwa Samia anajua anatawala Watanzania, basi walau awe na akiba kwamba hao anaowatawala wanazo kumbukumbu, bado wanakumbuka walichokipigia kura mwaka 2020, bado wanaikumbuka Itikadi ya CCM, pia wanaikumbuka Ilani ya CCM.

25. Rais Samia amewastaajabisha Watanzania makini alipofika New York alikuwa na wakati mzuri na Bi. Mange Kimambi “mtukanaji” anayejulikana wazi alivyoisemea mbovu serikali ya Magufuli.

26. Sijui kwa tendo hilo Rais Samia alitaka Watanzania wamweleweje? KWAMBA alikuwa Makamu wa Rais tu, wala hakuwa sehemu ya utawala wa Magufuli?

27. Baadaye nilisikia jinsi Rais Biden wa Marekani alivyoutolea nje ujumbe wa Tanzania, hakukutana na Rais wetu hata kwa mazungumzo ya salamu tu za dakika chache. Rais Biden hakutaka hata kupiga picha ya pamoja na Rais Samia!

28. Yawezekana Biden alijiepusha na “demonize” yaani picha moja aonekane yuko na Rais wa nchi, kisha picha nyingine huyo Rais aliyeonana na Biden, anaonekana yuko na “vimange?” Hapana! Hilo lingeifedhehesha Marekani kama dola.
 
Kipindi cha magufuli ungetoa hili chapisho ungeonekana wa maana sana
Binafsi sielewi Rais anataka kutuaminisha nini kwa kuteua watu walioondolewa kwa aibu na mwendazake.Pia uteuzi wa Ridhwani aangalie upya watanzania wanalalamika kuwa kwa sasa JK anaendesha nchi kwa rimoti. Kwahiyo anapomteua Kijana wake ndio anaharibu zaidi nchi inaenda kuwa ya kifalme. Nape alisema chama kina wenyewe na wenyewe ndio hao wanachaguana.
 
Binafsi sielewi Rais anataka kutuaminisha nini kwa kuteua watu walioondolewa kwa aibu na mwendazake.Pia uteuzi wa Ridhwani aangalie upya watanzania wanalalamika kuwa kwa sasa JK anaendesha nchi kwa rimoti.kwahiyo anapomteua Kijana wake ndio anaharibu zaidi nchi inaenda kuwa ya kifalme.Nape alisema chama kina wenyewe na wenyewe ndio hao wanachaguana.
Kwani JK alifanya dhambi gani kama mtawala mbona amefanye mazuri tu pia tuache wivu riz one kuwa waziri ni jambo la kawaida tu naye ana sifa
 
Mzee hii ni historia nzuri yenye mafunzo. Ila nikusaidie kuhusu sakata la marehemu Chediel
Mgonja: Alipokosa Ubunge, ni kweli Rais alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa lakini aliyemkosoa Nyerere kwa utenzi huo na Nyerere akaufuta alikuwa marehemu Timothy Apiyo ambaye alikuwa ndiye Chief Secretary wakati huo. Labda niseme hapa kuwa Chief Secretary kwenye serikali ana nafasi pekee, ya kuwa Mkuu wa Watumishi wote wa Serikali na pili ndiye Katibu wa Baraza la Mawaziri.

Ki itifaki ana hadhi kubwa sana Serikalini ingawa wanaowateua wakati mwingine huwa wanamteua mwenzao badala ya kuteua mtu wa kuwa na hadhi pia kauli ya mwisho kuhusu Utumishi serikalini . Kuhusu story yetu ya Mgonja, Timothy Apiyo alimweleza Nyerere kwamba kwa sababu wapiga kura wa Same wamemkataa Mgonja kuwa Mbunge, na kwa sababu wakati ule Mkuu wa Mkoa alikuwa pia anakuwa Mbunge (ex officio), kwa kumteua Mgonja kuwa Mkuu wa Mkoa Nyerere alikuwa anamrejesha Mgonja Bungeni kwa mlango wa nyuma jambo ambalo siyo sahihi. Na viongozi wa wakati ule, hata Nyerere, walikuwa wanaheshimu hoja za msingi, akatengua Ukuu wa Mkoa wa Mgonja. Nakushukuru sana Mhe. Kasyupa.
 
Binafsi sielewi Rais anataka kutuaminisha nini kwa kuteua watu walioondolewa kwa aibu na mwendazake.Pia uteuzi wa Ridhwani aangalie upya watanzania wanalalamika kuwa kwa sasa JK anaendesha nchi kwa rimoti.kwahiyo anapomteua Kijana wake ndio anaharibu zaidi nchi inaenda kuwa ya kifalme.Nape alisema chama kina wenyewe na wenyewe ndio hao wanachaguana.
Ipi sababu ya mwendazaje kumuondoa nape? Kisa makonda? Mwendazake alikuwa na chuki,hasira kisasi na malipizi
 
Watawala kimewajaa kiburi,nazani hili ni fundisho kwa hitaji la katiba mpya,sio tu kwa Chadema hata kwa CCM pia,halafu huyu Rais, Kikweta atatuletea matatizo makubwa sana huko mbeleni
 
kwani JK alifanya dhambi gani kama mtawala mbona amefanye mazuri tu pia tuache wivu riz one kuwa waziri ni jambo la kawaida tu naye ana sifa
Rizimonko anasifa gani ya kuwa waziri? Naomba uwe bayana. Unajua kipindi cha kuteka watu na kuwatesa na wengine kuwapoteza kwa kasi sana kiliasisiwa na nani na ama kilikuwa kipindi gani?

Unajua ambaye CCM ilimfia mikononi ni nani?
Unafahamu ongezeko la matumizi ya madawa lilinawili wakati gani?
Unafahamu ufisadi wa kutisha tangu taifa lianze ulifanyika lini?
Unajua elimu ilishuka kwa kazi ya 5g kipindi gani?
Unajua teuzi za hovy hovyo zilifanyika kipindi gani?
Ni kwanini siku zake watu tukivaa nguo za kijani tulikuwa tukizomewa na kupeprushiwa mchanga mahala pengine tukipita?

Unajua nguvu gani iitumumika kuirudisha CCM madarakani 2015?
Unajua urais wake aliupataje?

Kama wewe ni wa shule z amulugo, au ni aina ya Aisha mke wa mohamed, hutakiwi kusema neno maana hakuna ulijualo.
Kama wewe ni underage, nenda kacheze na wenzako wako kule mchangani.
 
Binafsi sielewi Rais anataka kutuaminisha nini kwa kuteua watu walioondolewa kwa aibu na mwendazake.Pia uteuzi wa Ridhwani aangalie upya watanzania wanalalamika kuwa kwa sasa JK anaendesha nchi kwa rimoti.kwahiyo anapomteua Kijana wake ndio anaharibu zaidi nchi inaenda kuwa ya kifalme.Nape alisema chama kina wenyewe na wenyewe ndio hao wanachaguana.
Huyu anayemdanganya kufanya teuzi tatanishi anawmingiza mitini. Ipo siku atakumbuka.
 
Wewe ni legend wa ukweli mzalendo wa ukweli, vipi maoni yako kuhusu maoni ya Ndugai n.a. kujiuzuru kwake naomba maoni yako kwa andiko natamani useme neno naona Hii simulizi inawasha taa
 
Rizimonko anasifa gani ya kuwa waziri? Naomba uwe bayana.
Unajua kipindi cha kuteka watu na kuwatesa na wengine kuwapoteza kwa kasi sana kiliasisiwa na nani na ama kilikuwa kipindi gani?
Unajua ambaye ccm ilimfia mikononi ni nani?
Unafahamu ongezeko la matumizi ya madawa lilinawili wakati gani?
Unafahamu ufisadi wa kutisha tangu taifa lianze ulifanyika lini?
Unajua elimu ilishuka kwa kazi ya 5g kipindi gani?
Unajua teuzi za hovy hovyo zilifanyika kipindi gani?
Ni kwanini siku zake watu tukivaa nguo za kijani tulikuwa tukizomewa na kupeprushiwa mchanga mahala pengine tukipita?
Unajua nguvu gani iitumumika kuirudisha ccm madarakani 2015?
Unajua urais wake aliupataje?

Kama wewe ni wa shule z amulugo, au ni aina ya Aisha mke wa mohamed, hutakiwi kusema neno maana hakuna ulijualo.
Kama wewe ni underage, nenda kacheze na wenzako wako kule mchangani.
Hongera kwa memory nzuri hakika unamfahamu Kikwete mwanamtandao, tume ya Daud Mwakawago na ripoti yake, kubakwa kwa awamu ya wazanzbar 2005
 
Binafsi sielewi Rais anataka kutuaminisha nini kwa kuteua watu walioondolewa kwa aibu na mwendazake.Pia uteuzi wa Ridhwani aangalie upya watanzania wanalalamika kuwa kwa sasa JK anaendesha nchi kwa rimoti.kwahiyo anapomteua Kijana wake ndio anaharibu zaidi nchi inaenda kuwa ya kifalme.Nape alisema chama kina wenyewe na wenyewe ndio hao wanachaguana.
Rizi wani aneteuliwa miongoni mwa wabunge halali wa JMT.
 
Mzee hii ni historia nzuri yenye mafunzo. Ila nikusaidie kuhusu sakata la marehemu Chediel
Mgonja: Alipokosa Ubunge, ni kweli Rais alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa lakini aliyemkosoa Nyerere kwa utenzi huo na Nyerere akaufuta alikuwa marehemu Timothy Apiyo ambaye alikuwa ndiye Chief Secretary wakati huo. Labda niseme hapa kuwa Chief Secretary kwenye serikali ana nafasi pekee, ya kuwa Mkuu wa Watumishi wote wa Serikali na pili ndiye Katibu wa Baraza la Mawaziri.

Ki itifaki ana hadhi kubwa sana Serikalini ingawa wanaowateua wakati mwingine huwa wanamteua mwenzao badala ya kuteua mtu wa kuwa na hadhi pia kauli ya mwisho kuhusu Utumishi serikalini . Kuhusu story yetu ya Mgonja, Timothy Apiyo alimweleza Nyerere kwamba kwa sababu wapiga kura wa Same wamemkataa Mgonja kuwa Mbunge, na kwa sababu wakati ule Mkuu wa Mkoa alikuwa pia anakuwa Mbunge (ex officio), kwa kumteua Mgonja kuwa Mkuu wa Mkoa Nyerere alikuwa anamrejesha Mgonja Bungeni kwa mlango wa nyuma jambo ambalo siyo sahihi. Na viongozi wa wakati ule, hata Nyerere, walikuwa wanaheshimu hoja za msingi, akatengua Ukuu wa Mkoa wa Mgonja. Nakushukuru sana Mhe. Kasyupa.
Wote wawili ni kama hii historia imewapita pembeni kidogo. Wacha na mimi niwape historia ninayo ijua,

Mgonja mwaka 1980 alishinda ubunge ila mpinzani wake akakata rufaa. Mahakama kuu mgonja akashinda Lakini mahakama kuu ya rufaa akashindwa na kuambiwa haruhusiwi kugombea ubunge kwa miaka 10.

Mwaka 1983 Nyerere akamteua kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga. Wakati huo ukiwa mkuu wa mkoa ulikuwa unakuwa mbunge pia.
Watu mbalimbali wakamkosoa Nyerere kwamba amevunja katiba. Nyerere akawa msikivu na akatengua ukuu wa mkoa wa Mgonja.

Waliomshauri Nyerere ni Sinde Warioba aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali na Sokoine ambaye alikuwa waziri mkuu.

Nyerere akasikiliza ushauri wao na kutengua uteuzi wa Mgonja.
 
Back
Top Bottom