Kamanda Sirro: Ninapigiwa simu usiku wa manane na wanawake

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,695
22,720
Kamishna Sirro afichua siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha EastAfrica Breakfast, ambapo amesema pamoja na changamoto hizo, anajitahidi kukabiliana nazo kwa kuwa tayari amekwishawazoea.



Amesema kuna wanawake wengine wakiona amependeza kwenye tukio fulani, wanajua lazima atakuwa na pesa za kuwasaidia katika maisha yao hivyo wakati mwingine humpigia usiku, na yeye akidhani kuwa ni taarifa za uhalifu, lakini hukutana na vishawishi vikiambatana na sifa kedekede."Mwigine anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini, wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi".


Amesema Kamanda SirroSirro ametaja changamoto nyingine ambazo hukutana nazo kuwa ni pamoja na suala la askari wake kulalamikiwa jambo linaloonesha dhahiri kama kiongozi ameshindwa kuwasimamia vijana anaowaongoza na mara nyingi huwa anachukua hatua.


Lingine ni uhalifu kuzidi katika eneo fulani na hufanya wananchi kuwa na uoga, na kupoteza imani kwa jeshi la polisi jambo ambalo linamfanya yeye ajisikie vibaya zaidi kuliko hata wananchi, huku nyingine ikiwa ni viongozi wa mitaa kutowajibika katika kudhibiti uhalifu pamoja na kuletewa taarifa za uongo.


Chanzo : EATV
 
Ivi EA Na EA wamekua reliable source of information kwa tz, naona kila kitu na kiongoz taarifa ikitoka utasikia akizungumza na East Africa Tv/radio, by tha way not bad keepit up IPP.
Kamanda sirro beba hiyo mizigo
 
Back
Top Bottom