Kamanda Sirro Mkuu wa Mkoa alitaja majina 69 hadharani na kwa mujibu wa taarifa zako waliokuja watu

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Kamanda Sirro Mkuu wa Mkoa alitaja majina 69 hadharani na kwa mujibu wa taarifa zako waliokuja police mpaka sasa watu sita akiwemo Manji na Gwajima.

Ila la kushangaza umeamua kushangaza umma kwa kauli zako kuwa Mbowe Ana 48 hours , wale wengine waliotajwa na Makonda na hawajatii wito umewapa muda gani? Juma ....Miezi au Miaka ? Kwanini umeamua kumsingle out mmoja kama hakuna lililojificha?

Je ? Ni kweli kuwa juzi ijumaa ulipatiwa wito wa Mahakama Kuu ukitakiwa wewe, ZCO na Mkuu wa Mkoa Makonda Mahakama Ni keshokutwa jumanne ?

Nakushauri kama raia wa Tanzania ...timiza wajibu wako kikamilifu na ukifuata sheria Kwani wewe Ni msomi wa sheria pia unajua mipaka ya mihimili.

Tumia taratibu zenu za kuita watuhumiwa ...haichukui dakika 2 kuandika wito ....tuone kama Mbowe atakataa wito huo halali kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Kamishina Sianga ameonyesha njia katika hili amekataa kutajwa kwa.majina ya watu bila uchunguzi kufanywa ....amekataa kuonea watu....

Naamini utafikishiwa andishi langu hili ...Nakutakia Jumapili njema katika kutimiza majukumu yako
.Mkurugenzi
Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema
 
Back
Top Bottom