Kamanda: Mtunza nidhamu za wanafunzi wa Arusha

Kamanda: Mtunza nidhamu za wanafunzi wa Arusha

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,829
Habari za jioni wakubwa.

Thread hii inaweza kuwahusu watu wa Arusha hasa hasa wale waliosoma elimu ya msingi katikati ya jiji la Arusha kipindi hicho manispaa ya Arusha.

Kwa wanafunzi hasa wa shule zetu za kidumu fagio ni wazi mnamkumbuka huyu mbaba aliyekuwa akijulikana kama 'Kamanda'

Huyu jamaa alikuwa ni mgambo propbably mwajiriwa wa manispaa ya Arusha,wengi mtakaomkumbuka na kukumbuka heka heka zake basi mlikuwa watoro shuleni.

Kamanda alikuwa anazunguka mitaani na kwa mara chache alikuwa akiibuka mashuleni na kutembeza bakora za kufa mtu kwa wanafunzi watoro au watukutu.

Kilinichonisikitisha juzi juzi nimekutana na Kamanda maeneo ya sanawari akiwa tungi na katika dodosa dodosa eti watu wanasema 'kamanda' kawa bwabwa!
 
Alikua anaitwa kufa kunoga,ole wako ukutane nae kitaan saa za masomo utajuta.
 
Kibaba kilikuwa nuksi kile.......halafu kutwa kusisitiza muwe chipukizi........nkt.......ila tulikuwa tukimuingiza mitaa ya Pangani.......haoni kitu........
 
Alishawahi kunikimbiza maeneo ya Naaz enzi hizo ilikuwa ni duka sio mgahawa. Hakunipata nilishukia na njia ya Arusha School, nikatokea mto Themi upande wa pili wa wa Zambia nikaendelea na misele kuelekea mlima Shabaha.
 
Alishawahi kunikimbiza maeneo ya naaz enzi hizo ilikua ni duka sio mgahawa. Hakunipata nilishukia na njia ya arusha school, nikatokea mto themi upande wa pili wa wa zambia nikaendelea na misele kuelekea mlima shabaha.

Wewe sema ulikuwa una kwenda bwawani........ha ha.......kamanda bana........
 
Yah.......kwa chini kule kupitia Fire kuna sehemu unatokea kwa waZambia.......nadhani pia na Breweries au Emco........😜😜
Nimekusoma,unajua kinana ziko kichwani ndio maana akili inachelewa kucharge!
Mko na Daudi Mchambuzi ?kama mko nae basi mnatisha!
 
Last edited by a moderator:
Alishawahi kunikimbiza maeneo ya naaz enzi hizo ilikua ni duka sio mgahawa. Hakunipata nilishukia na njia ya arusha school, nikatokea mto themi upande wa pili wa wa zambia nikaendelea na misele kuelekea mlima shabaha.

Halafu we jamaa inaelekea ulikuwa unaoga Mto Themi wewe....

Dahh....Nimeoga sana mto Themi...
 
mkuu mto themi ulikuwa noma kipindi hiko,labda uniambie wewe ulikuwa mtukutu kiasi hicho!

Ha ha ha....Nimeoga sana...Tena tulikuwa tunatoroka class ile saa nne "mapumzikoo" tunaenda...

Dahh...Sitosahau bana...Kuna mkuda mmoja alimtonya ticha wa class kuwa tunaendaga Mto Temii kuoga....Ticha kapeleka wapambe wake wakatuandika majina..

Wacha kabisa....Kesho yake Mstarini asubuhi tukaona maticha wameshika mboko mbilimbili kila mtu....Kuhamaki mara..."Wafuatao watoke waje mbele".....Mstarini wote kimyaaa...

Tukaitwa....Mkuu mavi yalikuwa yanasukuma chu.pi....Nilitamani ardhi ipasuke nitokomee pale nilipoitwa....

Dahhh...Tukaambiwa tujipange mbele..."Kila mmoja apate nafasi....halafu shika vidole"......Wooooowi....Tulipigwa mboko ambazo sitasahau....

Halafu shida ilikuwa si mboko hapo mbele ya shule...Ishu ilikuwa ni kutaniwa hasa ule mda wa "mapumzikoo" na kutawanyika.."manyumbanii"....pale ndo ilikuwa shedaahhh!!!

Kuanzia siku ile mpaka leo wala sijui Mto "Temii" una rangi gani...
 
Hahaha....Kufa kunoga hadi utumbo wa ndani ......huyu jamaa ametutuma sana chupa za bia shuleni. Aliwaleta watu waliocha shule miaka ya zamani waje kumalizia shule ....nasikia kumbe jamaa na ubabe woote alikuwa bwabwa
 
Enzi hizo mboko ilikuwa ruksa mashuleni,ila leo mmhh!! Watoto wa siku hizi hawana cha kusimulia baadaye..
 
Hahaha....Kufa kunoga hadi utumbo wa ndani ......huyu jamaa ametutuma sana chupa za bia shuleni. Aliwaleta watu waliocha shule miaka ya zamani waje kumalizia shule ....nasikia kumbe jamaa na ubabe woote alikuwa bwabwa

Hivi zile chupa alikuwa anapeleka wapi........?.....kamanda bana.......
 
Ameshatukimbiza sana enzi hizo tunatoroka shule ya uhuru nakwenda kucheza mpira arusha sec
 
Back
Top Bottom