Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,163
- 11,230
KUHUSU TOCHI MPYA(SPEED RADAR)
Ndugu wanahabari,
Ninapenda kuwatarifu uwepo wa vifaa vipya vya kisasa vya kupima mwendo wa magari. Vifaa vinauwezo wa kurekodi mwendo wa gari na wakati huo huo kuchukua picha ya mnato au video ya gari husika. Ili kuongeza ufanisi wa vifaa hivi, tumeelekeza askari wanaoshika vifaa hivyo wasivae sare ili wakishapata mwendo na picha za magari yaliyokiuka mwendo watoe taarifa kwa wenzao wenye sare wafanye ukamataji. Utaratibu huu unasaidia kuondoa dhana ya askari kujificha na kusimamisha magari kwa kushtukiza na kwa upande mwingine itapunguza tabia ya madereva kupeana ishara kuonyesha mahali walipo askari.
Ndugu wanahabari,
Jeshi la Polisi linawakumbusha Madereva na watumiaji wote wa barabara kuziheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani. Aidha nachukua nafasi hii kuwakumbusha askari wote kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani bila woga au upendeleo kwa kuzingatia maadili mema ya kazi.
Aidha nawajulisha watumiaji wote wa barabara hususani madereva kuwa askari wataendelea kuwa wakali sana katika kipindi hiki kwa kusimamia sheria kikamilifu ambapo hatua kali za kisheria zitachuliwa kwa yeyote atakayekamatwa akivunja sheria za usalama barabarani.
Ndugu wanahabari,
Mwisho napenda kuwaasa wananchi na wadau wa usalama barabarani kwa ujumla, watupe ushirikiano zaidi kwa kutoa taarifa za uhalifu wa usalama barabarani, kufuata sheria, kanuni na maelekezo kwa ajili ya usalama wao watumiapo barabara.
Kila mmoja atambue haki na wajibu wake awapo barabarani ikiwa ni kuwa na subira na kujali watumiaji wengine wa barabara kwani kila mmoja anayo haki sawa ya kutumia barabara. Watoto wasiachwe kutembea barabarani bila ya uangalizi wa watu wazima.
ENDESHA SALAMA - OKOA MAISHA.
Imetolewa na:
MOHAMMED R.MPINGA – DCP,
KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)