Kamanda Mpinga: Taarifa kuhusu tochi Mpya (Speed Radar)

Kamanda Mpinga: Taarifa kuhusu tochi Mpya (Speed Radar)

Ni jambo zuri, ila polisi hao wakae kwenye vibao vya 50khr, ili wasiwaonee wananchi, kama wanapokea faini wawe na risiti sio notifacation. Lakini ili kuleta tija zaidi fungeni kamera kwenye barabara kuu kuliko kusimamisha polisi njia nzima,hayo sio matumizi mazuri ya rasilimali watu.
 
Saa 10 asubuhi...saa tatu asubuhi nakula breakfast down town Moshi. Sasa huyo asievaa nakutana nae wapi.
 
Askari mwenye Tochi asiye na sare akikupiga/kukurekodi hakusimamishi anachofanya anawapigia simu wenzie mbele unakoelekea.

Huko ndio utasimamishwa na askari mwenye sare anakwambia sehemu fula umepita speed fulani ukibisha anapigiwa simu yule aliekupiga Tochi unaonyeshwa move nzima kuhusu mwendo wako.

Sidhani kama majambazi wanaweza kutumia fursa hiyo , maana asilimia kubwa Tochi zinakuwa mchana na kwenye makazi ya watu ambako kuna vibao vya speed limit.

Still bado kuna utata. Nimepita kwa speed pale kwenye down ya kuiacha mlandizi pembeni ya kituo cha polisi naelekea Morogoro, askari kapiga simu polisi wa Vigwaza. Nikibisha basi nikae pale vigwaza nasubiri tochi/video iletwe kutoka Mlandizi huo muda wa kusubiri upo kweli?

Na pili hiyo tochi/video inayotolewa mlandizi kuja kunionyesha mimi nilieko vigwaza si ilitakiwa imulike na wengine hapo mlandizi? Sasa wakiileta vigwaza sababu ya mimi si patabaki bila tochi?
 
Someni Vizuri Muelewe.Kuna Askari Aina Mbili Mwenye Sare Ndiye Mwenye Camera Na Mwenye Uniform Atakukamata Baada Ya Mawasiliano Baina Yao.Imetulia Sana Hiyo!

Asiye na sare ndio anashika tochi na mara nyingi hujificha ktk gari iliyoegeshwa pembeni ya barabara na kuwasiliana na mwenye sare ili kukamata mkosaji - ipate hivyo Kifarus. Pamoja na hayo kinachokera ni 50km/hr kila baada ya km chache na msafiri ana safari ndefu ya kwenda Mbeya au Bukoba. Miaka ya 90s Dar - Moro watu walikwenda kwa saa 2 kwa bus. Sasa ni saa 6. Tunarudi enzi za kutembea na layland na barabara isiyo na lami. Jitihada za binadamu ktk kusafiri ni kupunguza muda wa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Ndio maana kuna uvumbuzi wa gari za speed hadi 200 na barabara bora za lami, zenye inclination au degree of sloping ya kisayasi ili kulisapoti gari . siku hizi kuna kitu kinaitwa capsule kinaruka angani kutoka point moja hadi nyingine. Sisi hatujali kupoteza muda barabarani? Nasikia USA minimum speed limit ni 50 miles ambazo ni karibu 100km. Ukiwa highway unaangalia uwezo wako kulimudu gari. Napendekeza tutafute njia mbadala za kisayansi ili kupunguza ajali, tusi jikite kwenye tochi tu.
 
Someni Vizuri Muelewe.Kuna Askari Aina Mbili Mwenye Sare Ndiye Mwenye Camera Na Mwenye Uniform Atakukamata Baada Ya Mawasiliano Baina Yao.Imetulia Sana Hiyo!
Wewe unajifanya umesoma ukaelewa kumbe nawe ni walewale tu. Mwenye sare ndio mwenye uniform, au kwa muono wako ni tofauti?? Na huyu sie mwenye Kamera.
 
Someni Vizuri Muelewe.Kuna Askari Aina Mbili Mwenye Sare Ndiye Mwenye Camera Na Mwenye Uniform Atakukamata Baada Ya Mawasiliano Baina Yao.Imetulia Sana Hiyo!
Mkuu, kuna tofauti gani kati ya sare na uniform?
 
Wangekaa tu hadi usiku, maana mchana yanaenda pole pole ila giza likiingia tu wanaanza kutupeperusha kama vishada

Tayari wameanza, jana saa 11 asubuhi tena kuna giza kali nimepigwa tochi Mafinga mahali pa 50kmph nilikua 130km/h nikaliwa 30 elfu,

Ila walikuwepo polis wa kutosha
 
Itabidi safari ndefu tuwe tunatembea usiku.
Huu muda wa mchana 50kph ni kama unasindikiza msiba.
Ila Mpinga ajue hapa hajatatua tatizo ila ameongeza mianya ya rushwa.
 
KUHUSU TOCHI MPYA(SPEED RADAR)

Ndugu wanahabari,
Ninapenda kuwatarifu uwepo wa vifaa vipya vya kisasa vya kupima mwendo wa magari. Vifaa vinauwezo wa kurekodi mwendo wa gari na wakati huo huo kuchukua picha ya mnato au video ya gari husika. Ili kuongeza ufanisi wa vifaa hivi, tumeelekeza askari wanaoshika vifaa hivyo wasivae sare ili wakishapata mwendo na picha za magari yaliyokiuka mwendo watoe taarifa kwa wenzao wenye sare wafanye ukamataji. Utaratibu huu unasaidia kuondoa dhana ya askari kujificha na kusimamisha magari kwa kushtukiza na kwa upande mwingine itapunguza tabia ya madereva kupeana ishara kuonyesha mahali walipo askari.

Ndugu wanahabari,
Jeshi la Polisi linawakumbusha Madereva na watumiaji wote wa barabara kuziheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani. Aidha nachukua nafasi hii kuwakumbusha askari wote kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani bila woga au upendeleo kwa kuzingatia maadili mema ya kazi.

Aidha nawajulisha watumiaji wote wa barabara hususani madereva kuwa askari wataendelea kuwa wakali sana katika kipindi hiki kwa kusimamia sheria kikamilifu ambapo hatua kali za kisheria zitachuliwa kwa yeyote atakayekamatwa akivunja sheria za usalama barabarani.

Ndugu wanahabari,
Mwisho napenda kuwaasa wananchi na wadau wa usalama barabarani kwa ujumla, watupe ushirikiano zaidi kwa kutoa taarifa za uhalifu wa usalama barabarani, kufuata sheria, kanuni na maelekezo kwa ajili ya usalama wao watumiapo barabara.

Kila mmoja atambue haki na wajibu wake awapo barabarani ikiwa ni kuwa na subira na kujali watumiaji wengine wa barabara kwani kila mmoja anayo haki sawa ya kutumia barabara. Watoto wasiachwe kutembea barabarani bila ya uangalizi wa watu wazima.

ENDESHA SALAMA - OKOA MAISHA.

Imetolewa na:
MOHAMMED R.MPINGA – DCP,
KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)

Hivi bado Tunahitaji kamera zinazoshikwa na "askari wasiovaa sare" katika karne hii? Yako wapi matunda mema ya teknolojia wanayofaidi wanadamu wenzetu huko kwao? Huyu "askari asiyevaa sare" ataacha kujikinga mvua ikinyesha? Atasimama barabarani kama mlingoti kwa masaa mangapi kabla hajachoshwa na jua kali na kuamua kujihifadhi kwenye kivuli? Let's be serious! Kwa utitiri na u-tembo wa kodi tunazolipa, ufike wakati tutendewe haki. Kwa mtindo huu wa kuchukua teknolojia mtumba wallah ajali hazitakuja zikome nchi hii!
 
Nimezipenda sana, leo mesafiri dar-moro, ABC bus kapigwa tatu njiani kapasuliwa 210,000/= mazima kilka moja 70 elfu

kaliwa huyo na ujanja wake,70 kwa sheria ipi?na ukiwa na notification moja unatembea nayo siku nzima.
 
Back
Top Bottom