Kamanda Mpinga: Taarifa kuhusu tochi Mpya (Speed Radar)

Walishanidaka wiki mbili zilizopita lakini walinikamua kishkaji cha 5 tu. Ingawa walinipiga sound kuwa ile picha waliyonipiga lazima wakaitolee maelezo maana haifutiki hivyo lazima niwape 30. Lakini yaliisha kiungwana tu.
 
kutokuvaa sare hiyo ni mbinu ya kuongeza mapato kuliko kupunguza ajali. Kama faini jan -june ni zaidi ya 4 bn sioni sababu ya traffic polisi kutokubuni mbinu za kuongeza mapato

hizo 4 bn zidisha mara 10 ndo mapato halali yalitakiwa kuingia serikalini, nyingine zimeishia katika mifuko ya sarawili na mashati meupe
 
nikweli lakn hapo kwenye kuwaambia wavae nguo za kiraia ili wasijulikane ndo sijaelewa.

Mkuu hiyo inasaidia sana kama itafanyika kwa uhalali bila rushwa.

Ni kwamba ukipita kwa speed isiyoruhusiwa sehemu ambapo yupo askari mwenye Tochi na amevaa kiraia, anachofanya yeye anakupiga Tochi tu pamoja na kukurekodi bila wewe kujua na hakusimamishi.

Ila anawapigia simu wenzie wenye sare walio mbele yako kama kilomita mbili au tano, wanachofanya ni kukusomea hukumu tu kuwa sehemu fulani umepita kwa speed isiyoruhusiwa.

Ukibisha wanakuletea ile tochi yenye picha na hata video ya gari lako ikionyesha mwendo uliopita nao.

Mbaya zaidi Tochi za sasa zinapiga Mbele na nyuma yaani hata ukiigeuzia mgongo unakurekodi tu.

Hivyo ukiwa kwenye eneo la speed hamsini ukimkuta askari wa Tochi hakikisha unamaliza eneo lenye speed hamsini ndio uongeze mwendo la sivyo utawalaumu askari bure.
 
Agizo la waziri wa fedha vipi?
Faini bila EFD machine kutolea risiti ni wizi wa kuaminiwa.
 
Mkuu hiyo inasaidia sana kama itafanyika kwa uhalali bila rushwa.

Ni kwamba ukipita kwa speed isiyoruhusiwa sehemu ambapo yupo askari mwenye Tochi na amevaa kiraia, anachofanya yeye anakupiga Tochi tu pamoja na kukurekodi bila wewe kujua na hakusimamishi.

Ila anawapigia simu wenzie wenye sare walio mbele yako kama kilomita mbili au tano, wanachofanya ni kukusomea hukumu tu kuwa sehemu fulani umepita kwa speed isiyoruhusiwa.

Ukibisha wanakuletea ile tochi yenye picha na hata video ya gari lako ikionyesha mwendo uliopita nao.

Mbaya zaidi Tochi za sasa zinapiga Mbele na nyuma yaani hata ukiigeuzia mgongo unakurekodi tu.

Hivyo ukiwa kwenye eneo la speed hamsini ukimkuta askari wa Tochi hakikisha unamaliza eneo lenye speed hamsini ndio uongeze mwendo la sivyo utawalaumu askari bure.

tujiandae kwa kipigo cha majambaz kwani wanaweza wakatumia fursa ya hao polis wasiovaa sare kusimamisha magar ya abiria na kuwateka.
police mpinga take care kwa hili
 
Askari akinisimamisha bila uniform sisimami
 
Mmeongeza biashara ingine watu wapige pesa kwanini nasema hivo hao askar wanao vaa kiraiya wanasimama sehem ambayo haina alama yoyote kwahivo nauliza tutembe spidi 50 mwanzo wa safari hadi mwisho wasafari? Naomba kufahamishwa.
 
tujiandae kwa kipigo cha majambaz kwani wanaweza wakatumia fursa ya hao polis wasiovaa sare kusimamisha magar ya abiria na kuwateka.
police mpinga take care kwa hili
Askari mwenye Tochi asiye na sare akikupiga/kukurekodi hakusimamishi anachofanya anawapigia simu wenzie mbele unakoelekea.

Huko ndio utasimamishwa na askari mwenye sare anakwambia sehemu fula umepita speed fulani ukibisha anapigiwa simu yule aliekupiga Tochi unaonyeshwa move nzima kuhusu mwendo wako.

Sidhani kama majambazi wanaweza kutumia fursa hiyo , maana asilimia kubwa Tochi zinakuwa mchana na kwenye makazi ya watu ambako kuna vibao vya speed limit.
 
Mkuu hiyo inasaidia sana kama itafanyika kwa uhalali bila rushwa.

Ni kwamba ukipita kwa speed isiyoruhusiwa sehemu ambapo yupo askari mwenye Tochi na amevaa kiraia, anachofanya yeye anakupiga Tochi tu pamoja na kukurekodi bila wewe kujua na hakusimamishi.

Ila anawapigia simu wenzie wenye sare walio mbele yako kama kilomita mbili au tano, wanachofanya ni kukusomea hukumu tu kuwa sehemu fulani umepita kwa speed isiyoruhusiwa.

Ukibisha wanakuletea ile tochi yenye picha na hata video ya gari lako ikionyesha mwendo uliopita nao.

Mbaya zaidi Tochi za sasa zinapiga Mbele na nyuma yaani hata ukiigeuzia mgongo unakurekodi tu.

Hivyo ukiwa kwenye eneo la speed hamsini ukimkuta askari wa Tochi hakikisha unamaliza eneo lenye speed hamsini ndio uongeze mwendo la sivyo utawalaumu askari bure.

Mkuu bado kuna utata mkubwa, kwani hiyo video inaonyesha na kibao cha 50km/hr..?? kama haionyeshi je utajuaje kama ni kweli askari huyo alikua kwenye eneo husika? Kwa hili nadhani ni wajibu wa hao askari kutoa ushahidi wakutosha kabisa kabla ya kumtoza mtu faini isijeonekana kuwa kuna uonezi unaoweza kutokea
 
Wangekaa tu hadi usiku, maana mchana yanaenda pole pole ila giza likiingia tu wanaanza kutupeperusha kama vishada
 
Zinasaidia kwa kiasi flani, ila rushwa imeongezeka. Kwa barabara ya dar-moshi-arusha rushwa ni elfu kumi kama hutaki unalipa 30000 yao unaandikiwa resiti.
 
Tochi sawa na efd je? Nilitegemea utoaji risiti nao uwe electronic kama waziri wa fedha alivyoagiza
 
Mkuu bado kuna utata mkubwa, kwani hiyo video inaonyesha na kibao cha 50km/hr..?? kama haionyeshi je utajuaje kama ni kweli askari huyo alikua kwenye eneo husika? Kwa hili nadhani ni wajibu wa hao askari kutoa ushahidi wakutosha kabisa kabla ya kumtoza mtu faini isijeonekana kuwa kuna uonezi unaoweza kutokea

Shinyanga kuna road bump speed limit ni 20 ukivuka na 27 unao, hongera sana.
 
So itabd umsubirie mwenye video aje akuonyeshe wewe mmoja uliyekamatwa halafu anapokuja anaacha wazi wengine wanaendelea kupita na spidi na kusababisha ajali???!!!!!!!!je hizo video zinaseviwa ijulikane ni magari mangapi na yapi yameovaspidi !!!! Na je kurekodi ninkwa matakwa ya turafiki? Au mashwine imeswetiwa inarekodi tu ukiweka on?? Maswali haya ni vzr yakazingatiwa maana kuna dalili za mianya ya rushwa na ajali
 
Nauliza:Hivi ajali hizi huwa zinatokea yale maeneo waliyoweka vibao vya speed 50 tu au?

Baada ya swali mi napendekeza askari hawa wa tochi ikibidi wawepo hata pale ambapo hakuna hivyo vibao maana tumechoka kupoteza ndugu zetu kwenye ajali.
 
Hii kamera imeletwa kwa nia njema ila zinatumiwa vibaya na wahusika. Nakumbuka nilikamatwa kingorwila moro nikaambiwa nilipita kwa spidi 57 wakanichezeshea video ya gari yangu na namba zake lakini bado ilikuwa ngumu kujua kwa uhakika km mhusika alinirekodi kabla au baada ya kibao cha 50km.

Kwa maoni yangu yule jamaa ni aidha alinirekodi nikiwa umbali mchache sana kabla ya kukiacha kibao cha 50km au pengine tayari nilikuwa nimekiacha kibao kwa sababu nilikuwa na tahadhari kubwa kwa sabab nilishajua wapo maeneo hayo
 
Maigizo mengine haya...

Tatizo kubwa linaletewa solution ndogo...
 
Back
Top Bottom