mbinguni
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 2,786
- 1,080
Kila siku inapofika saa kumi na mbili jioni pale stendi ya daladala,kuna kuwa na abiria wengi sana ambao wanahitaji usafiri wa kwenda majumbani mwao.Kinachosikitisha sana ni kuwa serikali(Trafiki polisi na sumatra) wanakuwa likizo huku wananchi wakiteseka sana na kuchelewa bila sababu ya msingi.Hali hii inachangiwa na serikali kuwa likizo wakati huo.Katika muda huo wapiga debe wakishirikiana na madereva wa daladala wanakatisha route zao kama jinsi leseni zao zinavyowataka.
Ndugu mbunge katika hili nakuomba ukaguzi wa ghafla katika stendi hiyo ujionee wapiga kura wako wanavyoteseka.
Nakuomba kama mbunge wabane watendaji hawa watusaidie tuondokana na mateso haya yasiyo ya lazima.