Kamanda' Lema Anachanja Mbuga Vita Ya Mtandaoni!

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Ndugu zangu,

Zimebaki takribani saa 26 kabla ya vituo vya kupigia kura kufungwa. Ni kwenye Pima- Maji ya http://mjengwablog.com . Anga ya mtandaoni imechafuka kwa vita kali ya kuwania kura. Ni vita ya usiku na mchana. Ni katika mchakato huu wa kumpata mbunge bora Kijana kwa mwaka 2011.


Habari kubwa siku ya leo?


Ni ’ Kamanda’ Godbless Lema.

Mtu huyu Godbless Lema anaonekana kuwa jeshi kubwa la ’Wanamgambo wa mtandaoni’. Alfajiri hii ninapoandika uchambuzi huu mfupi, ’ Kamanda’ Lema, kama anavyoitwa na wafuasi wake anaongoza kwa kura zaidi ya mia mbili. Lema yuko mbele ya Zitto Kabwe huku akiwa amemwacha nyuma John Mnyika aliye nafasi ya tatu kwa kura zaidi ya elfu moja na m ia sita. Naam, vita kali kwa sasa ni kati ya Godbless Lema na Zitto Kabwe.

Ilivyo sasa:

Kura zipatazo elfu na mia sita zitakuwa zimepigwa kwa siku ya kupiga kura itakayomalizika muda mfupi ujao. Ni ongezeko la kura mi sita kutoka idadi ya kura zilizopigwa jana. Kura 1600 kwa siku, ni rekodi mpya!



Tafsiri yake?


Kura hizi za mtandaoni ambazo mwanzoni kuna waliojitokeza na kuzibeza kwa nguvu zote zinazonekana kuwavutia wengi na kuwa ni kipimo kinachokubalika kisayansi katika kupima ’kina cha maji ya kisiasa’ ama upepo wa kisiasa kama inavyofahamika na wengi.


Ndio maana tumeona, kuwa kura hizi za mtandaoni zimeamsha hamasa ya kisiasa kwa vijana, dada na kaka zao katika siasa na nje ya siasa, na hata wazee pia, walio ndani na nje ya siasa. Naam, kwa anayetaka kujifunza, basi, kuna mengi ya kujifunza katika kufuatilia mwenendo wa kura hizi.





Zitto Kabwe:



Yuko nyuma ya Lema kwa kura mia mbili. Lakini, kwa mtu makini ataweka kichwani, kuwa ” You Should Never Count Him Out!”- Kwamba kwenye karata za kisiasa, kamwe usimtoe Zitto Kabwe kwenye hesabu zako. Niliandika juzi, kuwa Zitto Kabwe ni mwanasiasa kijana lakini mkongwe mtandaoni na hata nje ya mitandao. Ana uzoefu wa uwanja wa mapambano.



Zitto Kabwe anazijua njia za kupita mtandaoni na kukusanya kura. Ameonyesha uwezo wa kukusanya kura zaidi ya mia moja za mtandaoni ndani ya dakika 80. Hivyo basi, Lema anayeongoza kwa kura mia mbili hawezi na hapaswi kujiamini. Kwamba yaweza kuwa makosa kwa Lema kusimama njiani na kuanza kunywa juisi kabla kipenga cha mwisho wa kupiga kura kupulizwa.


Kulikoni Kijana John Mnyika ?

Bado yuko kwenye nafasi ya tatu. Ameacha nyuma na Zitto kwa zaidi ya kura elfu moja. Kwa Mnyika kupanda kwenda nafasi ya pili ni jambo lisilowezekana kwa sasa. Na kushuka toka alipo kwenye nafasi ya tatu nako hakuwezekani. Hivyo basi, John Mnyika atabaki kufuatilia na kutafsiri mtanange unaoendelea sasa kati ya Zitto na Lema.



Mr. Sugu ’kajituliza kwake kasuku?’


” Hapendi matata, hapendi maneno!” Sugu, kama nilivyomwelezea juzi, anaelekea kwenda kugota kwenye kura mia na kitu, na si zaidi. Lakini, ni muhimu naye akaanza kutambua, kuwa mapambano ya kisiasa huko tunakokwenda yatahitaji pia juhudi na uwezo wa kupambana mtandaoni.


January Makamba:

Pamoja na kuwa wa kwanza kutamka kuwa kura hizi si za Kisayansi, namwona ndugu yangu January Makamba akiwa amekaa na kalamu na karatasi. Anachambua ’ Kisayansi’ mwenendo wa kura hizi na tafsiri yake katika juhudi za kulikamata kisiasa na ’ Kisayansi’ kundi la vijana. January Makamba amebaki na kura tatu kufikisha kura mia moja. Yawezekana.


’Mo’ Dewji


Ni mtu wa mikakati. Katika ’ biashara’ ya siasa ’ Mo’ Dewji ataangalia kwanza faida aliyoipata katika mchakato huu; kuwa ametambulishwa hata kwa wale ambao hawakumfahamu sana kisiasa. Na biashara ya siasa ni kujitangaza kama ilivyo biashara nyingine. Hilo la mwisho ’ Mo’ Dewji hahitaji kwenda darasani. Maana, anajua pia, kuwa ’ Kiduku’ kimempandisha chati pia!

Mkosamali kakumbuka shuka kumekucha!
Katika siku mbili hizi Mkosamali kafikisha kura sita kutoka kura mbili. Anamzidi Peter Serukamba kwa kura tatu. Katika mchakato huu kuna ’ Ligi’ zaidi ya moja.
Naam, siku ya leo nayo inaweza ikazaa habari mpya kesho. Nenda sasa http://mjengwablog.com kupiga kura yako. Mahali ni juu kulia.

 
Unakosea unaposema watu walizibeza. Ni kama vile una maanisha walizipinga bila ya ku-reason. Nadhani unakumbuka vizuri kuwa baada ya watu kutoa mitazamo yao juu ya zoezi zima, utaratibu ulibadilishwa.

Ni sahihi kwa Lema kuongoza, Lema ni ana elements za uongozi, elements ambazo zimejizalisha kwa wengi ndani yake na kujenga sifq za uongozi.

Zitto ni kwa sababu ya jina lake kuwa katika anga la siasa kwa muda mrefu jumlisha sababu ilizozitaja ndiyo kinachomfanya ashike nafasi hiyo ni political opportunist.
 
MJENGWA%2BHEADR.jpg


Hii blog ya mjengwa siipendi na hii rangi ya sisiemu aliyoweka.inaonekana ni mwandishi asiyejielewa kwa kuelemea upande flani
 
Back
Top Bottom