Simba lunyasi
JF-Expert Member
- Sep 28, 2022
- 355
- 770
Jana jioni Nilipita hapo maeneo ya Jangwani nikaona greda zipo kazini, nikajiuliza maswali mbalimbali.
Mojawapo ya maswali yaliyonijia kichwani ni hivi kweli hawa Yanga wapo serious kujenga kiwanja cha kuchezea mpira hapo?
Leo nimesikia Rais wa Yanga kupitia vyombo vya habari ya kuwa ujenzi rasmi utaanza mwezi wa 4 baada ya hili zoezi la sasa la kuandaa eneo la ardhi itakayotumika.
Hapa nimejiuliza maswali mengi, Simba tumekuwa na mwekezaji karibu miaka 10 sasa, ambaye ameenda mbali zaidi na kudai ameshainunua Simba na ni moja ya mali zake.
Huyu mwekezaji wetu aliwahi kuahidi atajenga uwanja wa kuchezea na tukaanza kuchangia fedha kwa ajili ya huo ujenzi. Ila sijui fedha zile walikula wajanja au zilienda kutumika kwenye matumizi mengine.
Point yangu ni kuwa Simba S.C chini ya Mo Dewji ndio walikuwa wa kwanza kuja na hili wazo la kuwa na uwanja wake sasa naona Utopolo ndio wanaenda kutekeleza ilo wazo.
Kwa trend hii tunapoelekea Simba itaachwa na hawa utopolo kwenye kila kitu, hata huko kwenye rank za Caf napo ni suala la muda tu hawa utopolo watakuwa juu yetu.
Endapo ujenzi wa kiwanja utaanza hapo Jangwani basi ndugu Mo Dewji inabidi atuachie timu mapema ili apatikane mwekezaji ambaye ataweza kushindana na kasi ya Yanga maana tunazidi kuachwa na mchawi tunamjua