Kama yamekushinda ondoka kwa heshima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama yamekushinda ondoka kwa heshima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima wa Kuku, Nov 13, 2011.

 1. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nimepata bahati ya kutembelea nchi kadhaa hapa ulimwenguni. Wenzetu wana shida zao kama sisi tulivyo na za kwetu. Kinachotofautisha wenzetu ambao tunasema wanashida na sisi ni kuwa hata kama wanalia kuna shida kuna mambo ya msingi hakuna anayeweza kuyachezea. Kwa mfano miundombinu katika ujumla wake. Ukifika kwenye mji kama Harare nimepata muda wa kuuzunguka kwa miaka mingi karibu wote. Sijaona Squatter area hata moja. Wabongo wenzangu wanaoifahamu Harare watakubaliana nami. Mpango mji ukiwekwa hakuna yeyote atakayeuvuruga kwa namna yoyote. Ukijenga kibanda ukasema unataka uongeze kwenye nyumba yako kesho asubuhi kinavunjwa kwa sababu ya mipango mji. nafasi za wazi zote ziko vilevile tangu mkoloni.

  Mheshimiwa Mkulu wetu anakimbiliaga sana kwenda kusuluhisha migogoro ya wenzake kule nje, lakini ya kwake imemshinda...gogoro la umeya Arusha ameliachia na linazidi kukua huku kila siku mara Kenya, mara Somalia mara kule.

  Ushauri wangu wa bure kwa JK ni kuwa kama nchi imemshinda awaachie wengine kuliko uharibifu huu tunaouona sasa hapa Bongo.
  Nawasilisha.
   
 2. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Ni aibu hata kusema mi mtanzania.
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mimi naona umewakilisha katika mlango mdogo sana wa Kikwete kushindwa kuongoza nchi. Nionavyo mimi rais wetu inabidi ajiuzulu kwa sababu kuu tatu:
  1.0 Kishindwa kisimamia uchumi wa nchi hadi saizi serikali ipo hoi kimapato wakati matumizi yanazidi kuongezeka kila kukicha. Hii baada ya muda ni dalili ya serikali kufilisika maana itafikia hatua itashindwa kukopesheka. Kuna kipindi cha Mkapa tulishawahi kuambiwa tufunge mikanda kwa sababu nchi inalipa madeni. Tulikuwa tunapewa takwimu sahihi na kinacholipwa lakini siku hizi ukimya ndiyo umetalawala.
  2.0 Kushindwa kukemea maovu na kibaya zaidi hata yale aliyoyasema hadharani, mathalani alitangaza zoezi la kujivua gamba lakini mpaka leo bado jambo hilo limezua mgogoro mkubwa mpaka saizi kisa ni udhaifu wa mheshimiwa kusimamia mambo ya chama. Hili haliishii hapa, litakuwa linakwenda mbali zaidi hata katika mambo nyeti serikalini.
  3.0 Suala la ajira kwa vijana. Nchi imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ajira kwa vijana kuliko kipindi chochote kile. Mfumo usio rasmi haupewi kipaumbele katika kukuza soko la ajira.
  Yapo mambo mengi sana ya kuonyesha JK nchi imemshinda, mengine mtajazia nilipokomea.
  Nawasilisha.
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Mie nadhani vasco anataka kuiacha nchi imeingia vitani alafu akimbilie nje
   
 5. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ki ukweli hatutamruhusu achomoke pale uwanja wa ndege.
   
 6. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kila kitu bora liende!
   
Loading...