Sio maadui watatu tu
Mwalimu: # 4 ni JAMII YA WATANZANIA.
Watanzania hasa wa kipato cha chini ambao ndio waathirika wakuu wa elimu
mbovu wamekuwa wakwanza kuwadharau walimu na taaluma nzima ya ualimu.
Ni ajabu unamshauri mwalimu atafute namna ya kujikimu na ualimu uwe
ziada then unategemea mwanao apate elimu bora toka kwa mwalimu huyo
huyo. Nashauri watanzania tubadilike, matatizo ya walimu yanatuhusu sana
kwa namna moja ama nyingine.
Kuwashauri walimu waidharau na kuitelekeza fani ya ualimu ni sawa na
kumshauri baba mwenye nyumba aitelekeze familia yake ambayo
ameitengeneza kwa gharama kubwa kuanzia kutafuta mchumba, kuoa na kuzaa
watoto. Ni ushauri mzuri kuwekeza kwenye shughuli nyingine za kujipatia
kipato kama uchumi binafsi wa mwalimu, na wengi wamekuwa wakifanya hivyo
na imesaidia sana LAKINI (behind the scene) tunashuhudia matokeo
mabaya ya wanafunzi darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita.
Hayo yote pamoja na mambo mengineni matokeo ya poor concentration among
teachers in and out of the four walls of the classroom.
Sasa hivi unaweza kuona walimu wametulia tu wameshagundua jitihada zao
na matatizo yao hakuna anayeyaona si serikali wala jamii ya watanzania,
kwa mtazamo wangu naona kuna mgomo baridi katika fani ya ualimu.