Kama wewe ni fundi, au mkulima na upo site ila una upungufu wa vibarua wapate hapa

fungi06

JF-Expert Member
Jul 1, 2020
633
857
Hello there!

Kumekua na uhaba mkubwa wa ajira sana nchini kwetu, kiongozi sahihi atakae tokea kumaliza huu ukame atakua amesaidia sana taifa n hakika ataweka legacy kubwa kama ile iliyowekwa na baba wa taifa kwa kukomboa nchi.

Mbali na ugumu wa ajira uliopo sasa nchini huenda mda mwingine nikutokana na access ya information.
Juzi nimekuta fundi anatafuta vibarua wakusaidiana nae kubeba tofali kupandisha ukuta wa gorofa, ambapo par day ni elfu 10 mpaka elfu 8. Si sawa nakukaa bure.

Nikagundua ni tatizo la access ya information, fundi anajuana na watu wake ndio ila sio kila mmoja anakua na hali nzuri kila siku na sio kila kazi wanakua wanajitosheleza.

Huu uzi naomba MAFUNDI mlipo popote unaandika eneo unapofanya kazi,
Idadi ya mafundi(vibarua) unaoitaji,
Bila kusahau Namba yako sa simu.

Kazi za site jamani zisilale. Unakuta ujenzi wa wiki unachukua miezi kisa Vibaru hamna.

Vibarua wapo sema access ya information inakua hamna. Tusaidiane hapa maana vijana ni wengi mtaani wasio na kazi, ila wapo tiyari kuingia site mda wowote.

Pia kwa wale wanaoitaji vibarua pia washambani, mnaweza pia andika eneo ulilopo na idadi ya vibarua unaoitaji bila kuacha kuweka namba yako yasimu utafutwe utoe kazi.

Tusaidiane kwa chochote kitu, huwezi kula ngombe mzima mwenyewe kwenye jamii ya watu wenye upendo kama wa hii nchi yetu👷🏿👷🏿👷🏿👷🏿

Tuitane SITE.
 
Tunachukua vibarua wanaokuja site kuomba kazi direct, ukisema uokoteze wa mitandaoni mnaweza mkasumbuana baadae kwenye malipo, maana wengi kazi hawawezi ila kwenye malipo analeta vurugu.
Mkiwa hamjatimia na mkiona kuna uitaji sio mbaya kuitana kwa kuambuzana ukweki na kwa upendo
 
Nahitaji msichana wa kazi za ndani,eneo la kazi ni Arusha mjini,nyumba ina mfanyakazi mmoja wa kiume kwa kazi za nje kama garden,kutunza mbwa nk,msichana atawajibika kutunza watoto na usafi wa nyumba na vyombo,mimi baba nipo mbali ila mama yupo,karibuni.
 
Wafundi wengi wanamasaidia wao wanaojuana kitambo, na ukiona fundi anatafuta ovyo masaidia huyo Kuna walakini labda kwenye malipo mbabaishaji au nyodo masaidia wanaomjua wanamkwepa.
 
Uzi Kama huu Ni mzuri wa kusaidiana Ila wabongo wengi hawataki kusaidiana ukiwa unatafuta kazi ndio utajua,watu wanapeana kazi kwa kujuana saana,kazi za kibarua kupata kwa sasa Ni ngumu Sana mpaka uwe na refa.

Kama watu wenye uhitaji wa usaidizi wa watu wangekuja hapa kusaidia,sio tu ujenzi hata kazi mbali mbali.
 
Tunachukua vibarua wanaokuja site kuomba kazi direct, ukisema uokoteze wa mitandaoni mnaweza mkasumbuana baadae kwenye malipo, maana wengi kazi hawawezi ila kwenye malipo analeta vurugu.
We jamaa ulisadiwa kupata kazi humu,Leo hii ushasahau hutaki kusaidia watu?
 
kuna hekari 500 za kulima kama ww ni mwanaume wa kweli na unaitaji pesa, za kiume karb hekar elfu 70 kula kwa boss location: songea... town mikoan kama dar, mbeya mwanza nauli tunatuma hata kama hatukujui ikitaka naul unatumiwa sasa kula nauli ujue kama usiku ukilala unafanya kazi au unalala,, utapigiswa kaz mpaka useme naul yenu naludisha na hakuna mtu ataekutafuta
 
Nitumie hiyo nauli mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom