Kama watoto(under 18) hawatakiwi kutumia kwanini watangaziwe Pombe kamari nk

yeto

Member
Aug 23, 2010
59
40
Habari wakuu

Kuna matangazo mengi ya vitu ambavyo mtoto chini ya miaka 18 haruhusiwi kutumia lakini tangazo linakuwa kuubwa mwishoni ndio unakuta hilo onyo

Kwa mzazi yoyote atakubali kuwa haya matangazo jamii ya kwanza kuathirika ni watoto kwa kuwa wao ndio wanatumia muda mwingi kwenye TV na vichwa vyao havina mambo mengi.

Matangazo haya mengi yana picha au nyimbo nzuri ambayo kwa watoto ni rahisi kukumbuka.Hivyo ni vigumu baadae kuja kumshawishi kuwa siyo kitu kizuri.

Matangazo haya yanawekwa muda ambao watoto wengo wako macho au na mengine wanayaona mabarabarani mfano matangazo ya kubeti mpaka ndani ya mabasi ya mwendo kasi.

Je miaka ijayo tukiwa na kizazi cha walevi na wacheza kamari nani alaumiwe

Tuondoe matangazo yote kama ya pombe na kamari ili tukiokoe kizazi chetu kama tulivyofanya kwenye sigara na pia tunavyopambana na suala la viroba.

Nawasilisha
 
wanatumia TV kutangaza biashara zao, wewe mzazi chunga mwanao, hawawezi kutangaza biashara usiku wa manane nani ataangalia na hali karibia kila mtu amelala!
 
Kwa kuweka hilo onyo wao wanakua wametimiza wajibu wao uliobaki ni wa wazazi, jamii na serikali.

Mfano muuza duka angekua anagoma kumuuzia mtoto kilevi au kumruhusu kucheza kamari mpaka mtoto aoneshe kitambulisho (bahati mbaya vitambulisho vyenyewe vimeanza juzi tu).
Jamii ikimuona mtoto anafanya yaliyo kinyume iende ikaripoti, na serikali ichukue hatua.
 
Back
Top Bottom