Kama Watanzania, Target yetu kubwa ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Watanzania, Target yetu kubwa ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, May 21, 2012.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wadau,

  Mimi nataka kufahamu sisi kama watanzania target yetu kubwa ni nini?, Maana hata wakati nyerere na wale watu wengine target yao ilikuwa ni kumg'oa Mkoloni ili aingie Mtanzania ambaye hana uhusiano hata kidogo na wazungu, walowezi etc.

  Sasa wakati huu na karne hii kinachoonekana ni Ukoloni wa aina nyingine kiasi cha Kikundi fulani cha watu kujinufaisha wenyewe na ndugu jamaa na marafiki zao na hadi sasa wanafikia hatua ya Kuwanufaisha wageni. maana kama inafikia mtu anaona bora Mgeni achukue 90% yeye apate 10% kwa sababu tu akitenda haki watanzania watapata 1005 yeye 0% au mshahara tu.

  Kwa upande wangu,
  1. issue hapa ni kuiondoa CCM na Mfumo wake wote.. Tujipange kama Rwanda baada ya Mauaji.
  2. Kumweka mtu ambaye hana uhusiano na CCM pamoja na Mafisadi au Mtu ambaye hajawahi kuwa kiongozi CCM..
  3. Kuhakikisha wale wote ambao wanapingana na wanaotaka kuiondoa CCM na mfumo wake wote na wao wanaondoka na kuungana nao mtaani... Mfano Shibuda hata akilini mwake haamini kama ipo siku CCM itatoweka kama KANU pamoja na yeye kuwa Mbunge wa CDM...

  Huyu binti ambaye anapingana na mwenyekiti wa Bavicha na Viongozi wa Chama kwa ujumla.. mimi nafikiri hapa kuna Nguvu ya Watu fulani nyuma ya hawa wasaliti, kwa sababu katika hali ya kwaida sijui wanapata wapi Nguvi ya Kufanya hivyo..

  Swali kwa wadau.... Target yetu ni nini?
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Mkuu, tatizo tulilonalo sasa chini ya CCM, Linaweza kujitokeza tena chini ya CHADEMA, hivyo hakuna kuweka one time target, Target yetu hivi sasa inatakiwa kuwa progressive, kwamba, sawa, we have already made the right decision, CCM out, lakini ni lazima na hawa CHADEMA waelewe kwamba huko mbeleni wakianza kubweteka na wao out, out Taget is CHANGE.
   
Loading...