Kama vipi tuachane!

missa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Posts
360
Reaction score
193
Habari zenu wana JF.

kuna kaka yangu katika ukoo,alikuwa na mchumba wamedumu kwa miaka 3,mwaka huu mwezi wa 6 tulitarajia kula mpunga mana maandalizi ya ndoa yao yalikwisha anza, na huko kijijini kwetu walishaanza kuchangishana.

Cha kusikitisha kila wanapokuwa na mgogoro mdada alikuwa anatoa kauli" kama vipi tuachane, mana mi ni mzuri na wanaume wengi ma handsome wenye pesa zao wananitaka''

Basi hiyo kauli ikawa inatumika kama silaha kila wanapopata mgogoro na kaka yangu,iwe makosa ni ya kaka au ya mdada basi kaka yangu akawa ni mtu wa kujishusha na kuomba yaishe hata kama makosa ni ya mdada!na hii ilitokana na ukweli kwamba kaka yetu alimpenda sana mpenzi wake na alikuwa tayari kunusuru penzi lake kwa namna yoyote ile mradi tu kuondoa malumbano!

Mbali na hayo yote kaka ametumia gharama nyingi sana kumfungulia miradi mbalimbali mpenziwe zikiwemo saloon za kike lakini mdada ndo kwanza anajinadi kwamba yule mwanaume hawezi kumuacha hata iweje mana kwake amekufa ameoza!

Sasa mwezi uliopita wakagombana kisa mdada kapiga cm kaka akiwa kazini halafu kaka hakupokea cm,baadae kaka akampigia cm kumweleza kwamba hakupokea cm muda ule alikuwa na kazi,basi kama kawaida ya mdada akaanzisha ugomvi na kusema kama vipi tuachane,kaka akaomba radhi ikashindikana,Basi kaka akakubali waachane kweli!


Basi siku kadhaa zikapita huku wakiwa wamechuniana,baadae mdada akarudi akasema anaomba msamaha hatorudia tena,kaka akasema amemsamehe ila hataki mapenzi naye tena na uchumba uishie hapo mana kadri wanavyokaribia ndoa ndo anazidisha vituko!

Mdada kusikia akasema kama hataki waendelee atamwonyesha kazi,basi baada ya cku mbili kaka akakamatwa,kuuliza sababu wanasema katishia kumuua mpenzi wake,jamani wanawake wengine,baadae mahakamani ikaonesha kazusha na hana ushahidi isitoshe yeye ndo alikuwa anatuma sms za matusi ya nguoni kwa kaka na ushahidi ulikuwepo,kesi imefutwa!!!!

sasa kesi imefutwa anaendelea kumtumia sms za matusi kaka hadi leo hii ninapoandika,sasa najiuliza jamani kama bado unampenda mpenzi wako kwa nini ukimbilie kusema tuachane kila mnapogombana?sasa uchumba umekwisha na mipango ya ndoa imesitishwa japo alikwisha lipiwa mahari zote! Hellow ladies and Gentlemen learn how to control your mouth!
 
Hawa wanawake wanaotoroka mirembe kabla hawajapona wanasumbua sana,tuweni makini nao.
 

mmmmh,pole yke dada jamn ss nw kwa nini alkuwa anatngisha kibiriti wkt anajua jamaa anampenda na kumsapoti....unajua tingisha kiberiti ukiona jamaa ulyenaye mapenz hana,wenzie wanatafuta watu wa kuwapenda kiasi hicho hawapati zaid ya walaghai aya ss yamemkuta..mpe pole sana!
 
Alikua anatikisa kiberiti huyo na yamemtokea puani...pole yake....Inaonekana hakuwa na mapenzi ya dhati anyway...ukimpenda mtu humpi option ya kuachana bali unatafuta kila sababu muwe pamoja "FOREVER"...
Nampa hongera kubwaaa huyo mkaka kwa uamuzi alouchukua na asitatarike awe na msimamo thabiti....Ikiwezekana pia abadili namba ya sim na amripoti huyo dada"FOR STOCKING HIM"!!
 
sure,sasa kachanganyikiwa kweli kweli na wenzake wanamcheka mana kaka alimpenda sana na hata watu wake wa karibu na nduguze walijua hilo,walijaribu kumuonya alikuwa hasikilizi mtu zaidi ya kujibu yeye ndo mzuri watu wanamtongoza atapata mwingine,sasa kumbe alikuwa anatikisa kibiriti!!
 
Kaka kachukua uamuzi wenye busara, "Kama vipi tuachane" hili neno lingetumika kama silaha hata baada ya kufunga ndoa.

Ndo tatizo la baadhi wanawake wanaosifiwa wazuri na kupendwa kwa dhati wa wenza wao...ptuuuuu
 
tunaogopa hata kumsogelea kumpa pole mana kachanganyikiwa anahaha huku na huko, na nduguze wamejitoa kabisa kwenye mambo yake wanasema amewafedhehesha!
 
Ukipanda magotini nakuacha,
ukipanda kifuani nakuacha,
ukipanda mabegani hamna shida nakuacha,

ukipanda kichwani hapana sikuachi, lazima nikushushe chini kabisa.

Hii ni sheria ya wanaume, haruhusiwi mtu yeyote yule kupanda kichwani.

Huyo dada amepanic.
 
Je ni gharama / Hasara kiasi gani itakayokufanya uvumilie maumivu na stress za kila siku maisha yako yote..., A Stitch in Time Saves Nine.

Pia kabla hajakurupuka ajue kwamba Action Speaks Louder than Words, aangalie vitendo kuliko maneno huenda huyo mwenza amekosa tu busara na ni mlopokaji lakini anampenda (Pia jamaa asiangalie ametumia gharama kiasi gani, kama hayupo Sure asepe) sio kuangalia ni mangapi kamfanyia au preparation za harusi zimekamilika
 
bahati haiji mara mbili acha achakaze soli za viatu sasa kwa kujipitisha kwa vidume
 
^^
missa naomba umpe nguvu kaka yako ktk hili.
Anachotakiwa kufanya ni kubadili mawasiliano na huyo mdada, na kisha atafute mtu mwingine ambae atakuwa kinga yake (hata kama si mahusiano rasmi, amfahamishe mkasa wote na ajue yeye ni kinga ya nini).
Nasema haya kwa sababu wasichana wa tabia za huyu mdada, wana kawaida ya kutumia hata mbinu za kishirikina ili kumrudisha mwanaume waendeleze majigambo yao ya kutojitambua.
^^
 
Last edited by a moderator:

Mwambie huyo kaka yako awe makini aongeze maombi mara mbili huyu alivyodata hata kwa kalumanzila hashindwi kwenda kumvuruga. weka mbali na watoto......
 

Kama ulikuwepo mahakamani,ni mlopokaji balaa,mahakamani aliwaacha watu hoi kwa uropokaji!!ukimuona kweli ni mzuri lakini visa vyake,utachoka kabisa!
 
Mwambie huyo kaka yako awe makini aongeze maombi mara mbili huyu alivyodata hata kwa kalumanzila hashindwi kwenda kumvuruga. weka mbali na watoto......

kweli kabisa,tumemwambia kaka aongeze ukaribu na mungu,na atulie amuombe mungu ampatie mchumba mwema ambaye baadae atakuwa mke mwema!
 
Huo mdada mshamba tu uzuri kitu gani?

Asilielie uzuri alilia bahati wangapi wazuri hata salamu hawapati lol.....

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
missa, huyo kaka yako na huyo dada ni kabila moja? umri wao unatofautiana vipi?

nijibu tafadhali...
 
Last edited by a moderator:
the same is happening to me. I posted it here this week, though mine is complicated but nampongeza kaka yako na asirudi nyuma.
 

kweli nadhani alimpendea support zake na si mapenzi ya dhati,mana kamtoa katika hali ngumu kamuweka katika maisha fulani yenye uhakika wa kupata chochote kilicho ndani ya uwezo wa kaka yetu,na heshima kwa sana!mana kaka hakuwa na namba za wanawake wengine kwenye cm yake zaidi yake,labda sisi nduguze tu!!lakini bado hakuridhika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…