Wakuu Reajo na wengine, hawa wachina wametapakaa sehemu nyingi sana duniani na Afrika kwa sasa ndio kwao kwani wapo kila pembe.
Hata katika nchi zilizoendelea hawa wasichana na wavulana wa kutoka China wenye vipaji katika kutengeneza kucha, nyusi na hata kutoa ushauri wa dawa za kienyeji za kichina, ndio wanaofanya shughuli hizi.
Juzijuzi nilikuwa nyumbani Tanzania kutembea kidogo, na kuna siku nikawa napitapita kutembea maeneo ya Kariakoo. Kuna sehemu mtaa wa Narung'mbe niliona wachina wanafanya usafi na sehemu hio inaonekana panafanyika ujenzi.
Walikuwa wanafagiafagia na kutumia ndoo za maji kwa kupiga deki eneo linalozunguka jengo hilo. Lakini nikaangalia upande wa pili wa barabara na nikawapona vijana wa kitanzania wamekaa wanapiga soga na wengine wakicheza bao.
Sasa hapo pana mambo mawili, moja ni kwamba inawezekana mkandarasi anajenga jengo hilo au washirika wake wanatoka China na inawezekana waliamua kuajiri wachina wenzao.
Pili ni kwamba utandawazi kwa nchi zetu umefungua kila kitu mpaka vitabu vya sheria za kwetu ambapo serikali inalazimika kuwasikiliza hao wawekezaji ambao hudai kuwaleta raia wa kutoka nje ili waje kuwafanyia kazi zao ambazo zingeweza kufanywa na raia wenyeji.
Au ni uzembe tu katika kila kitu ambapo wageni wanakuwa huru mno katika kufanya watakacho.