Kama unataka mali utaipata shambani

Nyuzi kama hizi huwa zinatia moyo sana kwa watu waliomakini.
Nisemetu kuwa shamba ndiyo kazi nzuri kwangu.
 
Hivi hii dosari ni kwa raia wote ama ni kwa kundi la tabaka tawala tu ambao ndiyo watunga sera?

Maana kila serikali inayoingia madarakani haiji na mkakati wa kuboresha kilimo.

Vipaumbele vyao vinakuwa kwenye miradi mfu na matumizi makubwa ya rasilimali za nchi.
 
Tatizo letu wengi mnapenda lawama yani visingizio na sababu kila kukicha me naamini hakuna mafanikio Bila changamoto suala la serikali sijui kupangiwa vyote ni sababu za kujiandaa kashindwa.. Mshindi atoi sababu yy anajaribu akikosea anarekebisha..
 
Safi sana mkuu, Mwaka 2003 nilikuwa na ndoto za kwenda kusoma Uingereza sikuwa na kipato chochote nilitegemea nguvu ya ndugu wazazi wangu hawakuwa na uwezo, 2004 nikaja Dar kukaa kwa kaka yangu kwa ahadi kuwa atanisaidia kutimiza ndoto zangu haikuwa kweli niligeuka mlinzi wa nyumba na mfanyakazi wa miradi yake chini ya maisha ya hulka ngumu za Shemeji.
2005 nikaondoka nyumbani kwa kaka yangu nikisema liwalo na liwe nikaanza kwa kuokota chupa tupu za maji na makopo kisha nauza, haikuwa rahisi lakini niliweza, leo Mungu ni Mwema nina miliki viusafiri vyangu kadhaa nina nyumba kadhaa, Simtegemei mtu ila Mungu.

Ninawaangalia walio kuwa wakinikoga kwa ajira serikalini 2006, 2007. Wengi wao natumai nimewapita, kuna maisha Nje ya ajira ukiwa na nia ya dhati. Sijafika bali napiga mbio ili nifike niendako..
 
Dawa ni kuzidi kubana mianya mingi ya pesa holela, hapo akili za watu zitakaa sawa, natamani JPM angeongoza kama miaka 20. Ugumu wa maisha ndio kipimo cha akili.
Tanzania kuna fulsa nyingi sana mkuu ila tunashindwa kutumia na tukiamua tunaweza
 
Very true.! Imagine mtu kawa katibu mkuu kwa mgongo wa mtu fulani ambaye nae pia alikuwa mpigaji. Unategemea huyo atakaye muajiri atakuwa msafi ? Kwanini isiwe kwa misingi ya ngono au kujuana?
Hapa ndipo uozo ulipoanzia unaingia ofisi ya serikali hakuna anaye wajibika ama kumuwajibisha mwenzie.kwa makosa dhahiri sabbu wengi ni wale wale, kuna kiongozi alipoingia madarakani alisema

"NCHI HII IMEOZA KILA UNAPOGUSA NI UOZO TU"..

Itachukua muda mrefu kubomoa mizizi yote ya uozo ule ili upate watu fresh ambao ni watu stahiki wa maeneo husika ya kazi lakini ikiwa ni kipindi kifupi, watakusubiri umalize awamu yako then business as usual.
 
Emu acha hzo kaka miaka miwili ata mua uvuni itakuwa miti?
Ubishi huu ungekuwa unafanyika shambani lingekuwa jambo jema sana, mfano umeshapanda huo mti halafu unabishana na aliyekupa hilo wazo,
 
Jambo jema ingekuwa kwenda kupanda halafu uhakika wa miaka 2 au laa utaupata ukisubiria mavuno.
Tusibishane ila hakuna mti unaweza ukapanda ukavuna ndani ya miaka miwil full stop. Labda kama unavuna fito.
 
Shukrani Sana mkuu


Je nikalime korosho???? ...koroshow
Je nikalime mbaazi????

Adui yangu ni serikali yangu... Haswa ccm.... Natumai umenielewa
 
Acha uongo. 2003 LA saba then 2010 umemaliza chuo na serving ya bum 130000. Mnapeana moyo na ambayo hayapo.
 
Shukrani Sana mkuu


Je nikalime korosho???? ...koroshow
Je nikalime mbaazi????

Adui yangu ni serikali yangu... Haswa ccm.... Natumai umenielewa
Mbaazi soko lake bado halieleweki toka Manji amekamatwa misimu miwili iliyopita. Panda mikorosho na uitunze mkuu utaenjoy na upande ile ya kisasa
 
Tusibishane ila hakuna mti unaweza ukapanda ukavuna ndani ya miaka miwil full stop. Labda kama unavuna fito.
Hakuna mti wa kuvuna kwa miaka miwili ila nakushauri usiichi kwa malengo ya miaka miwili bali ishi kwa malengo ya miaka 20-50 mbele ili ujue faida ya miradi ya mda mrefu.
 
Hongera sana kwa kudhubutu ndugu. Omba sana uwe na afya ya mwili, roho na nafsi na usimsahau Mungu wako kwa kufanikiwa
 
Mashamba ya kule Ulaya ni ya kurithi aka generational. Baba anamwachia mwanaye. Na baba aliachiwa na baba yake, nk. Kwahiyo wale wanaorithi shamba la familia mara nyingi wanakuwa wanajifunza kilimo na ufugaji tu kimatendo hapo nyumbani, na elimu ya juu kwao siyo muhimu. Sasa hii ni tofauti sana na mtu kuanza kufyeka mapori na vichaka ili atengeneze shamba. Jambo lingine ni kwamba wakulima wa Ulaya wanapewa ruzuku kubwa na Serikali zao . Bila ya hizo ruzuku wasingeweza kuzalisha chakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…