Kama unataka kuishi kwa raha Tanzania, tazama TBC, soma Tanzanite, Uhuru, Jamvi la Habari na Habari Leo.

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu kutumia simu elevu (smart phones), kutazama channel TV mbali mbali na kupekuwa mitandao ya kijamii tofauti tofauti kama Jamii Forums, Twitter, Facebook, Instagram na Whatapps.
Yote haya yamepelekea watu wengi kuanza kupata magonjwa yasiyo ambukizwa kama shinikizo la damu, stress na mengine mengi.

Haya yote yanatokana na watu kupenda kupekua pekua mambo yanayowachukiza hivyo kujikuta wakinyongonyea kwa habari wanazozipata ambazo hawazipendi na hawakutarajia kuzisikia.

Nyingi ya habari hizo ni za serikali kufanya baadhi ya uamuzi ambao wengi hawakuutarajia na hawakuzoea serikali za awali zikichukua uamuzi huo.

Wengine hujikuta wakitikana na kivunja sheria za mitandao na kujikuta wako kwenye mikono ya sheria.

Nawashauri muanze kusoma habari kwenye vyombo ambavyo venye mlengo wa serikali maana hapo utapata habari za ujenzi Wa reli kwa kiwango cha standard gauge, ujenzi wa bwawa la umeme pale Stiglier's Gorges, ununuzi wa ndege na mambo mengine ya namna hiyo.

Ukikomaa na habari za mitandao, magazeti mengine utakonda bure na pengine kufa kabisa kwa chuki dhidi ya serikali. Na mwisho wa siku huwezi badili chochote.

Nawatakia siku njema sana
 
Si wote mzee. Kuna watu habari nzuri au mbaya haziwapi shida au tatizo lolote. Wala hazileti stress. Inategemeana na mtu yukoje..
 
Kuna mambo mmeyachanganya, nani kakufundisha kuwa uliletwa duniani ili uishi kwa raha??

(ii). Kwamba kinachomkosesha raha mwanadamu ni siasa na Uchumi pekee - wangapi wako ktk stress sababu ya ndoa zao??

(iii). Wangapi wana strees sababu mvua imechelewa kunyesha??

(iv) wangapi wana stress sbb ya majanga ya moto, vita, nk

Note:
Mungu alikuleta duniani ili upambane na changamoto nyingi - kama siasa imelemaa, uinyooshe - kama ukweli unapindishwa, uukatae - kama uchumi unayumba, uuimarishe - kama demokrasia inakanyagwa, uioshe nk

Ni sababu ya changamoto hizo hata YESU alifariki akiwa na umri wa miaka 30 - usiogope, pigana vita iliyo kali kwa kuwa Mungu yu nawe!!!
 
Back
Top Bottom