DR SANTOS
JF-Expert Member
- Mar 11, 2019
- 14,480
- 32,733
Ni mwendelezo wa visa na mikasa ya kweli kabisa. Yafuatayo yalimkuta rafiki yangu.
Nilimkuta siku moja akiwa anaongea na binti kwenye simu niliwasubiri wamalize ndipo nikamuuliza vipi bro, kwani una mtoto wa nje? Hapo ndipo akaamua kunieleza kila kitu kwamba awali wakati anaanza kazi alikua na mwanamke ambae walipendana sana na kwakua alikua akisoma walikubaliana binti amalize masomo kwanza ndipo mambo mengine yaendelee.
Wakiendelea na mahusiano binti alimwambia rafiki yangu kwamba alikua mjamzito, awali rafiki yangu alikubali kulea lakini kikwazo ilikua ni binti ambaye alikua akihofia kuhusu shule na wazazi.
Mwisho binti alikubali kulea ujauzito ule na jamaa alikua akihudumia mpaka hatua ya mwisho binti anajifungua jamaa aligharamia kila kitu.
Ikapita miaka kadhaa pasipo kuonanana binti huyo mpaka alivokuja kumtafuta na alipoulizwa mahali alipo alidai yupo Dar na alikua akiishi geto na mwanae, huku akifanya fanya vishughuli vidogo ambavyo vilimwezesha kuishi na mwanae.
Muda mwingi nilikua na jamaa angu na stori walizokua wakipiga ni kuhusu miamala tu, mara mtoto anaumwa mara luku imeisha, na jamaa alikua akituma kila kitu. Nilijaribu kumshauri afanye kila njia amwone mtoto maana anaweza akawa analisha mwanaume mwenzie.
Rafiki yangu alikusanya akiba yake na alijipanga kwa safari kwakua ilikua ni wiki la kazi alimuomba mwenzie amlindie goli hadi atakaporudi.
Ilikua ni Ijumaa jamaa aliniaga vizuri nami nilimtakia kila laheri katika safari yake ya kwenda kumuona mtoto jijini Dar es Salaam. Aliondoka wakiwa wanawasiliana vizuri kabisa lakini jamaa alipokaribia Dar mawasiliano yalikatika simu ya yule dada haikua ikipatikana tena.
Kwakua alikua na namba ya beki tatu wao alifanikiwa kuonana na beki tatu ambae alimpa ramani nzima mpaka shule ambayo alikua akisoma mtoto ambapo jamaa alienda moja kwa moja mpaka shuleni na kumuulizia mtoto huyo na kufanikiwa kumuona kisha alimpiga picha na kuondoka zake.
Baada ya yote simu ya yule dada ilipatikana na walikutana kisha wakarudia mambo yao tena na baada ya hapo jamaa alirudi mkoani na kunijuza kila kilchoendelea, nilimshauri apige simu shuleni kuuliza ni nani anaelipa ada ya mtoto, pia majina ya wazazi wa mtoto.
Majibu yaliyorudi ni kwamba mtoto ana wazazi wote wawili na katika majina ya wazazi halikuepo jina la jamaa yangu wala yule dada hivyo jamaa alikua akipigwa pesa kila siku na kumbe binti mimba alishaitoa na mtoto si wake.
Tuweni makini sana na hii michezo, wengi sana wanapigwa.