Kama unaipenda Hip-Hop karibu tujadiri haya.

Ningependa niongelee issue ya Premo na Dre, lakini nachelea kusema tunapotea. Thread ilikuwa ni discussion ya Hip hop. Lakini naona Dre na Premo wameteka mjadala. Naomba tuendelee na mada kuu. Kuna mengi ya kujifunza na wadau tuna mengi ya kusema na kuuliza.
 
Mi naona bora wangepambanisha watu wanaofanya kazi ya aina moja, DJ ni taaluma tofauti kabisa Rapper!

So Dj Primo yapaswa afananishwe na Producer mwingine anayefanya pia Djayiing!

Dr Dre apambanishwe na Rapper mwingne ambaye pia anafanya Production.

Huwezi fananisha Kiungo Mkabaji na Kiungo Mshambuliaji
 


OK umesomeka mkuu...
Ingawa ni ngumu kushiriki mjadala wa Hiphop bila kuwajadili hao watu.
Nakuahidi tu huu ubishi utajitokeza tena mbeleni kwenye thread hii hii.
turudi kwenye mada husika, je nini mchango wako!
 


Ok Baraka umesomeka...
Turudi kwenye Mada husika
 
mkuu Matola kwa heshima yako naomba uje utie neno katika mjadala huu.
mjadala huu mi niliutoa hapa JF na nikaupeleka mtaani ambako nilipata upinzani mkubwa mno kutoka kwa wadau
 
dre ni DJ pia. na primo siyo dj kama alivyo Funkmaster Flex, yeye ni dj kama dre (WALIANZIA) ila ana lay down tracks bila sampling.
 
Kobello umemvua nguo Dr Dre katika post zako...
Omba radhi
dre anatumia muda mwingi kutengeneza album moja, huwa anasema he takes his time to perfect the beat, well he samples 80% of his beats.
Hata wakati wa Deathrow, Dat Nigga Daz ndiye aliyekuwa anatengeneza beats nyingi za Pac, Dogg Pound. Dre ana beats mbili tu kwenye All Eyez on me!
Plus hana vina vya nguvu.
But he makes money though..... He really know where tha paper is at!
 

Hakuna ninachoweza kuandika nisirudie ulichokwishaandika! Nimekuvulia kofia mkuu!!!
 
dre ni DJ pia. na primo siyo dj kama alivyo Funkmaster Flex, yeye ni dj kama dre (WALIANZIA) ila ana lay down tracks bila sampling.

Kwa maana hiyo unataka kufananisha U Dj anaofanya Abubakar Sadiq na DJ JD(John Dillunga)?

Yawezakana wote mkawa mwafanya Djaying, lakini katia level tofauti?

Hiyo ndo maana yangu, Jermnan Dupri ni Producer na Rapper hata kama anafanya Deejaying sio kwa level ya DJ Primo
 
dre ni DJ pia. na primo siyo dj kama alivyo Funkmaster Flex, yeye ni dj kama dre (WALIANZIA) ila ana lay down tracks bila sampling.

Kama Dre ni DJ basi hata Primo ni rapper pia.

NWA DJ wao alikuwa Yella.
 
Mimi ni mpenzi sana wa De La Soul, The Jungle Brothers, na A Tribe Called Quest.

Phife Dawg aka the Five-footer is one of the illest MCs.
 
Kama Dre ni DJ basi hata Primo ni rapper pia.

NWA DJ wao alikuwa Yella.
Kasome historia yake halafu ndiyo uanze ubishi, Dre ni DJ Andre, ambaye pia alikuwa R&B singer. Dre ni kama Shalamar.... turned OG
 
Mkuu Kiranga pote umo? kutoka theories za universe na atheism hadi kumtambua producer mkali!
 
Chifu, Southern Hip Hop umeiacha wapi? Wenyewe wanaita Dirty South, Southern Rap..ikiibuka kujibu mapigo ya East na West - kujaribu kuuonyesha kwamba hata South nao wanaweza kuwa rappers. Kuanzia kwa kina the Geto Boys, Bun B and Pimp C (UGK - UnderGroundKings), 8 Ball & MJG, Jermain Dupri, Dungeon Family (OutKast, Goodie Mob, Killer Mike) hadi kwa kina Ludacris, TI, Lil Wayne, Lil Jon - ambaye naye amekuja kama vile kuirevolutionize hip hop kwa kuingiza punk rock beats - heavy bassline, na kuja na genre inaitwa crunk music - crunk hip hop. Hawa jamaa - hususani hii crunk music - kwa namna fulani imeharibu kabisa ile Hip Hop asili, ya East na West. Kwani sasa si East, North, Midwest na hata West, wanamuziki wengi wanatekwa na crunk music - angalia Lean Back ya Fat Joe, Smack That ya Eminem ft. Akon n.k.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…