Kama unaipenda Hip-Hop karibu tujadiri haya.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari zenu mashabiki wa Hip-Hop! Leo ningependa tuelezane mambo mbalimba kuhusu music huu ili na wengine wajifunze.

Yawezekana kabisa wengi wetu hapa hatujui kwamba hip-hop ina matawi mengine mengi kwasababu hip-hop ni genre ya music basi nayo pia ina sub-genres zake kwa kuanzia tu Hip-Hop kwa kule Marekani imegawanyika katika vipengere kadhaa kutokana na geographical position hapo kuna.
-WEST COAST HIP HOP
-MIDWEST HIP HOP
-NORTH WEST HIP HOP
-EAST COAST HIP HOP.

Lakini lengo langu sio hizo geographical differences ningependa tujadiri sub-genres kama,

1-HARDCORE Hip-hop
2-GANGSTA RAP
3-HORROCORE
Ziko nyingi lakini kwa kuanzia tuanze na hizi.

Ukianza na Hardcore hip hop ambayo ilianzia pande za East Coast hasa katika jiji la New York na watu wanaosadikika kuianzisha ni Emcez kama, Run-D.M.C.,

Schoolly D,
Spoonie Gee,

Boogie Down
Productions,
Public Enemy and Kool
G Rap,
Miaka ya 1980's-1990's. Ikiwa na mtazamo wa kuelezea ubaguzi wa rangi, starehe, maisha ya mtaani na mengineyo.

Baadaye inakuja Gangsta Rap ikiwa inatokea upande wa West Coast na muanzilishi akiwa ni Ice -T na N.W.A ikiwa kama zao la Hardcore Hip Hop ndio maana bwana Schoolly D anaonekana kama pia alichangia kukua kwa muziki huu pia. Gangsta Rap pia ilikua ikichambua maisha ya mtaani ya mtu mweusi, ubaguzi wa rangi, starehe lakini baadhi ya wasanii wakaja kujiingiza katika makundi ya uharifu kana Crips na Bloods (nitakuja kuyaongelea pamoja na maana ya rangi za bandena).

Horrocore ni subgenre nyingi inayotokea Mid America sehemu za Detroit ni kwingineko na kundi la Ghetto Boys wanaonekana kama ndio waanzilishi na pia wasanii kama Kungfu Vampire na sasa Eminem ni mifano ya style hii iliyoegemea katika mashahiri ya imagination.

Kwa leo tuishie hapa lakini nafungua darasa hili kama kuna chochote waweza kuongeza au kuuliza. Karibuni wadau.
 
kwa jina naitwa Shifta natokea pwani ya Baidoa.
Swali langu linasema hivi,
Je kati ya DJ Premier na Dr Dre nani nyoko?
 
Dah swali lako gumu kweli kweli. Lakini kwa upande wangu nitatoa maoni kama ifuatavyo Dr. Dre ni producer mkali sana kwa Album alizofanya kwa wasanii wengi, lakini Dj Premier a.K.a Preem a.K.a Primo ni beat maker mkali we sikiliza beats alizowafanyia wakali kama, Apathy, Big L, Big
Daddy Kane, Bun B,
Canibus, D.I.T.C., Fat Joe,
Game, Jay-Z, Kanye
West, KRS-One, Lord
Finesse, M.O.P., Mos Def,
Nas, Rakim, Royce da
5'9", The LOX, The
Notorious B.I.G., Snoop
Dogg, Xzibit, rock band
Limp Bizkit, Ill Bill, Joell
Ortiz, and pop/R&B
singer Christina
Aguilera utapata jibu.

Ngoja wadau watatupa mwanga.
 
Nafikiri Mods wangeunganisha threads zote za Hip hop alafu iwekwe sticky iwe darasa maana kuna topic kibao toka miaka hiyo humu!!!
 
Dah swali lako gumu kweli kweli. Lakini kwa upande wangu nitatoa maoni kama ifuatavyo Dr. Dre ni producer mkali sana kwa Album alizofanya kwa wasanii wengi, lakini Dj Premier a.K.a Preem a.K.a Primo ni beat maker mkali we sikiliza beats alizowafanyia wakali kama, Apathy, Big L, Big
Daddy Kane, Bun B,
Canibus, D.I.T.C., Fat Joe,
Game, Jay-Z, Kanye
West, KRS-One, Lord
Finesse, M.O.P., Mos Def,
Nas, Rakim, Royce da
5'9", The LOX, The
Notorious B.I.G., Snoop
Dogg, Xzibit, rock band
Limp Bizkit, Ill Bill, Joell
Ortiz, and pop/R&B
singer Christina
Aguilera utapata jibu.

Ngoja wadau watatupa mwanga.


Haihitaji elimu ya chuo kikuu kugundua kuwa uko upande wa DJ Premier, kwani hata Dr Dre anawasanii kibao aliowahi kuwafanyia kazi ambazo ziliwatoa kimaisha na kuwapa more money na kuwaweka kwenye nafasi ya juu ya top 10 au 20 nyingi Duniani lakini huja waorodhesha.

Nina mashaka na Thread yako.
Kama umeanza kuonesha mapenzi katika post yako ya pili, basi huko tunakoenda ni lazima uwe Dikteta.
 
Haihitaji elimu ya chuo kikuu kugundua kuwa uko upande wa DJ Premier, kwani hata Dr Dre anawasanii kibao aliowahi kuwafanyia kazi ambazo ziliwatoa kimaisha na kuwapa more money na kuwaweka kwenye nafasi ya juu ya top 10 au 20 nyingi Duniani lakini huja waorodhesha.

Nina mashaka na Thread yako.
Kama umeanza kuonesha mapenzi katika post yako ya pili, basi huko tunakoenda ni lazima uwe Dikteta.

Mkuu mimi nimezungumzia upande wa Primo na hiyo haikufanyi ushindwe kutoa mtazamo wako kuhusu Dr Dre
 
Mkuu mimi nimezungumzia upande wa Primo na hiyo haikufanyi ushindwe kutoa mtazamo wako kuhusu Dr Dre


Mkuu nimeitafuta Thread mpaka nimeipata then naomba tuendelee na mjadala.
Je kati ya Dr Dre na DJ Primo ni yupi ambae amewatoa wasanii wengi na wakanata katika kilele cha mafanikio?
 
lakini kabla ya yoote ningependa tufahamu kwanza ubora wa producer tunaemtafuta hapa...
naomba unifahamishe
 
Kuongelea hii fani bila kumtaja Jermaine Dupri ni sawa na kuongelea kandanda bila kumtaja Ronaldinho Gaucho!
 
DJ Primo ni DJ na Producer.
Dr. Dre ni Rapper na Producer.

Wote ma producer, katika DJ'ing Dr. Dre hamuwezi Primo (DJ Premier), sikiliza scratching katika Code of The Streetz au turntable wizardry katika Mass Appeal- Gangstarr.Katika rapping Primo hamuwezi Dr. Dre kwani Primo si rapper.

Jibu linategemea na mapenzi ya mtu. The comparison is quaint.

Mie nimekuwa influenced sana na East Coast, ilikoanzia Hip Hop (The Sun Rises in The East - Jeru Tha Damaja), kwa hiyo naweza kusikiliza Primo cuts for hours on end.

Na hata nikisikiliza minimalism ya Primo (N.Y State of Mind Pt II -Nas, So Ghetto Jay-Z) Siwezi kuilinganisha na minimalism ya Dr. Dre, if you can call it that- (Keep Their Heads Ringin' **plastic**)

Not to say that the entire "The Chronic" is not a classic, lakini ukiangalia kwamba Dre kama alivyosema mwenyewe ni "producer who can rap and control the maestro" (Ain't Nothing But A G Thang) na Primo hajafanya hivyo, unaona kazi ilivyo kubwa kuwapambanisha. Upande mwingine DJ skills za Premier, sampling na scratching Dre hawezi hata kuzikaribia.

Lakini kwa sababu common ground yao ni producing, kwa mtizamo wangu, nampa DJ Premier ushindi.

There is a certain elegance to Primo, almost a Fibonacci like symmetry that I cannot get from the sometimes run of the mill clutter that could be Dr. Dre.
 
Kuongelea hii fani bila kumtaja Jermaine Dupri ni sawa na kuongelea kandanda bila kumtaja Ronaldinho Gaucho!


ahah hah hah haaah Companero ndugu yangu yaani alimradi tu unataka nionge...haya bana.
Ila juzi kati wewe na kundi lako mkamzushia Saint Gaucho amefariki...dah haya bana
 
JD mkali.


Ok kwa upande wako...
Mkuu Nyani ngabu nakuheshimu mno na ningeomba kujuwa unamkubali nani kati ya watu hao wawili ambao wameingilia hii thread, je kati ya DJ Primo na Dr Dre nani unamkubali?
Na kwa nini unamkubali?
Kitu chake kipi so special alichowahi kukifanya na kupelekea umkubali?

Tafadhali
 
Nimeelewa neno "nyoko" tu humu. Meningine nimeshindwa kuyaelewa. Niwatakie siku njema wana hip hop na wapenzi wa ma "dj nyoko".
 
Nimeelewa neno "nyoko" tu humu. Meningine nimeshindwa kuyaelewa. Niwatakie siku njema wana hip hop na wapenzi wa ma "dj nyoko".


asante mkuu...
ila kwa wana Hiphop hilo neno ni la kawaida sana.
Sijui kwenu wana Taarab...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom