Kama una tabia hizi 10 huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako yote

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,701
.
Sipendi kuwa mtu wa kuleta habari mbaya kwako, lakini ukweli huwa unabaki kuwa ukweli iwe unapendwa au haupendwi.
.
Kuna watu huwa wanasema mafanikio hayana fomula. Watu hao huwa hawajui. Kuna vitu ambavyo waliofanikiwa wote wanavyo na kuna vitu ambavyo walioshindwa wote wanavyo.
Jambo hili haliwezi kuwa bahati peke yake, kuna kanuni inahusika.
.
Kuna tabia kumi ambazo ni sumu sana na zipo kwa wengi walioshindwa. Ukizijua hizi na kuzikana kwenye maisha yako, utaweza kufika kwenye mafanikio makubwa.

Tabia yako ya Kutokujitambua.

Kama hujijui wewe ni nani na kwa nini uko hapa duniani, utatumia muda wako mwingi kuhangaika na kila kinachokuja mbele yako.Kama hujui kusudi la maisha yako na huna ndoto kubwa unazozipambania kuzifikia, utaridhika na chochote kinachokupa chakula na malazi tuu.Tofauti kubwa ya waliofanikiwa na walioshindwa ni kujitambua.
Kama mpaka sasa hujajua wewe ni nani na uko hapa duniani kwa sababu gani, Huwezi kufika kwenye mafanikio yako makubwa.

. Tabia yako ya Kutokujisomea.

Kujisomea vitabu na kujifunza vitu vipya ndiyo nguvu ya kuleta miujiza mikubwa kwenye maisha yako.Chochote unachotaka kujua kipo kwenye vitabu. Changamoto na magumu unayopitia kuna wengine walishayapitia na uzuri ni waliyaandika kwenye vitabu, wajibu wako ni kusoma uzoefu wao na kuchukua hatua kwa hali yako.
Waliofanikiwa ni wasomaji wazuri, wanajua kuna mengi hawajui. Hivyo, unapaswa kujifunza kila siku mpaka siku utakayokufa.Kama hupendi kujisomea, huwezi kuzijua njia za kufanikiwa.

Tabia yako ya Kutokuweka akiba.

Kama unatumia kipato chote unachoingiza, huwezi kufanikiwa. Haijalishi kipato ni kidogo au kikubwa kiasi gani.Hebu fikiria mkulima ambaye anakula mavuno yake yote bila kuacha mbegu, hawezi kufanikiwa kwenye kilimo maisha yake yote.Mafanikio yako hasa kwa upande wa fedha hayatokani na kiasi unacholipwa, bali jinsi unavyotumia kiasi hicho.
Kuweka akiba ni tabia unayopaswa kuijenga, Usiseme huweki akiba kwa sababu kipato ni kidogo, kama huwezi kuweka akiba kwenye kipato kidogo, hutaweza kuweka akiba kipato kikiwa kikubwa.Jijengee tabia ya kuweka akiba kwenye kila kipato chako na kisha kuwekeza ili izalishe zaidi.

. Tabia yako ya Kutokujiamini.

Kama hujiamini wewe mwenyewe, hakuna mwingine anayeweza kukuamini. Na kama hakuna anayeweza kukuamini, huwezi kufanikiwa.Waliofanikiwa wanajiamini mno, Kama hujiamini, umeshashindwa hata kabla hujaingia kwenye mapambano. Jenga tabia ya kujiamini na kuamini katika kile unachokifanya. Ikiwa utajiamini hata watu wengine watakuamini na kuwa tayari kushirikiana na wewe.

.Tabia yako ya Kulaumu na kulalamika.

Kuwalaumu na kuwalalamikia watu wengine ni kukubali kuyaweka maisha yako kwenye mikono yao na waamue kuyafanya watakavyo.Huwezi kufanikiwa kama huishi maisha yako maisha yako, Jambo lolote linalotokea kwenye maisha yako, wewe ndiye unayewajibika kwa asilimia 100.
Usilaumu wala kumlalamikia yeyote.
Siyo serikali, siyo wazazi, siyo ndugu, siyo mazingira na wala siyo hali ya uchumi. Ni wewe ndiye unayewajibika na maisha yako,chukua hatua sahihi ili za kuyaishi maisha yako mwenyewe ili ufanikiwe.

Tabia yako ya Kuahirisha mambo.

Tabia yako ya kupanga vizuri kitu unachopaswa kufanya, lakini unapofika wakati wa kukifanya unaahirisha na kujiambia hujawa tayari kukifanya, utafanya kesho au wakati mwingine, Ni jambo litakalokufanya usifanikiwe katika maisha yako yote.Kama unataka kufanikiwa futa kabisa msamiati wa nitafanya baadae au kesho kwenye maisha yako.Kila unapopanga kitu cha kufanya na wakati wa kufanya ukafika ukajisikia kuahirisha, jiambie nitafanya sasa na kisha anza kukifanya.Huhitaji kufanya kwa kiasi kikubwa sana, wewe anza kufanya na utajikuta unaendelea kufanya.Nidhamu binafsi ni hitaji muhimu sana kwenye maisha yako.

Tabia yako ya Kutokutoa Sadaka.

Unataka ufanikiwe halafu hutaki kubadili namna unavyoishi maisha yako. Hiyo ni sawa na kuwa na pipi, unataka kuila lakini pia ubaki nayo.Hiyo sayansi haipo, kupata kitu bora ambacho huna sasa, lazima upoteze kizuri ulichonacho sasa. Yote tunayojifunza hapa kuhusu mafanikio, yatafanya kazi kama utakuwa tayari kutoa kafara.Ili uweze kuweka akiba lazima utoe kafara kifedha, uachane na baadhi ya matumizi mazuri na unayoyapenda ili uweke akiba.
Ili upate muda wa kujisomea, lazima utoe kafara ya muda, uachane na mazuri unayofanya sasa ili upate muda wa kujisomea na kuwa bora zaidi.Ili uzungukwe na watu sahihi, lazima uwe tayari kuwapoteza wale ulionao sasa.Kuwa tayari kutoa kafara, kuwa tayari kutengana na unachokipenda sana ili uweze kupata makubwa zaidi.

. Kutokuwa king'ang'anizi.

Safari ya mafanikio siyo ya njia iliyonyooka. Kuna milima na mabonde na pia kuba kona kali.Utakutana na vikwazo na changamoto za kila aina. Kama mawazo yako ni mambo kuwa rahisi, hutafika mbali.Utashindwa, utaanguka, lakini haimaanishi huo ndiyo mwisho wa safari.Unapaswa kung'ang'ana na kuendelea na safari yako bila kujali nini umekutana nacho.Ili ufanikiwe, lazima ujipe agano kwamba utapata unachotaka au utakufa ukiwa unakipambania.
Ng'ang'ana hasa mpaka upate kile unachotaka.

. Tabia yako ya Kuamini njia za mkato.

Kama unaamini siku moja utalala masikini na kuamka tajiri basi jua utakufa masikini.Kama unasubiri 'zali la mentali', kwamba ukutane na bahati ambayo itakutoa ulipo na kukufikisha juu unajidanganya.Kama unaamini kuna siri ulizofichwa ambazo wachache tu ndiyo wanazijua utabaki kwenye mahangaiko yako siku zote za maisha yako.
Kama utaishi kwa kudhani kila waliofanikiwa ni freemason au wana njia zisizo za kawaida ambazo wametumia utahangaika sana na kuendelea kubaki pale ulipo.Acha kuhangaika na njia za mkato za maisha ya watu wengine na wala usizitamani, tengeneza njia yako hata kama ni ngumu kiasi gani mtangulize MUNGU na komaa hapo mpaka ufanikiwe.
.
. Tabia yako ya Kuzungukwa na watu wasio sahihi.

Wale wanaokuzunguka na unaotumia nao muda wako mwingi wanaathiri sana maisha yako.Ukitaka kuthibitisha hili, angalia maisha yako na ya wale ambao unatumia nao muda wako mwingi.Utagundua hamtofautiani sana, viwango vyenu vya mafanikio vinalingana.Ili ufanikiwe zaidi, unapaswa kuzungukwa na watu ambao tayari wameshafanikiwa zaidi yako au wako kwenye safari ya kufika kwenye mafanikio makubwa kama wewe.
Najua hili ni gumu kwenye jamii zetu, kuwapata watu sahihi siyo kazi rahisi.Lakini ipo jamii ya kipekee sana ambayo unaweza kujiunga nayo na ikakusaidia kufanikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabia yako ya kujiona mkamilifu.

Unahisi usipofanya jambo fulani ( ambalo ni mawazo yako binafsi tu) basi huwezi kufanikiwa. Basi ukiwa na tabia hiyo kufanikiwa kwako ni kwa mbinde saana.
Maana hakuna formula ya mafanikio.
 
Bookmarked
 
Hiyo ni sawa na kuwa na pipi, unataka kuila lakini pia ubaki nayo.Hiyo sayansi haipo,
Hiyo sayansi ipo!! inawezekana ukabaki na pipi yako kwa sababu km ninataka kubaki na pipi yangu nitafanya hivi....Nalamba kidogo utamu then naifunga tena kule Musoma wanaita '''kujiyangirisha''

ukitunze kikutunze!! sasa wey mleta mada umelisoma tu la kusoma huko ukatuletea humu km lilivyo!...nakuhakikishia hiyo sayansi ipo na inafanya kazi mnoo!! ukiishindwa hiii sayansi yako ya pipi utajiri kwako sahau!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom