Kama una hela huwezi kuishi Dar | Mji wa kishamba sana

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,998
Katika miji mibovu East Africa mojawapo ni Dar es Salama kwanza ujenzi wake ni holela inashindwa na miji ambayo haina mipango kama Moshi. Mtu alinunua kiwanja chake anataka ajenge mpaka amalize sehemu yake bila kuacha nafasi hata kidogo tu.

Hali ya hewa ni mbaya sana, hii ni kasoro nyingine inayofanya mji huu kuwa mbaya. Joto kali huwezi kulala ndani bila feni na hali joto inachochewa na mbanano wa baadhi ya nyumba.

Wizi, ukabaji na mambo ya kiswahili mengi ni tatizo lingine katika mji huu. Kile unachofanya lazma majirani zako wakumulike na kuja kutia huruma nyumbani.

Kama una akili utaishi Dar kwa ajili ya kutafuta tu sababu ya miangaiko ya kimaisha tu na ukishapata tafuta sehemu ya kupumzika ule matunda yake taratibu bila bugudha.

Ni mji gani unafaa kuishi na kula matunda yako unayolima Dar?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo Bakhressa hana hela ?, Mo Dewji hana hela?
Ipo tofauti kati ya kuishi Dar na kuishi Daslamu...Wanaoishi Dar hawana malalamiko hata siku moja, ila wa Daslamu ndio kutwa kulalamika ..

Mikocheni B - Dar
Masaki - Dar
Posta -Dar
Mbezi Beach -Dar
Mbagala - Daslamu
Sinza - Daslamu
Yaani mtu kweli uishi Masaki halafu ulalamike!! Shida ipo kwa wale wakazi wa Ubungo Maziwa au Tandale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuuu unaikosea heshima Daslam. Hata kama unaishi Mbagala, wewe tafuta pesa mazingira ya nyumbani yawe ya kuvutia, wikiendi Lunch huko Serena au Kempnsik, Meryy Brown, Live Band Nenda Zako New Afrika Hotel, Mademu nenda kawatafutie pande za IT Plaza Club, Nyanya na Sukar Mliman City, Gym nenda Colosium, Beach nenda zako Sunrise au huko Silver Sand brother Dar ni kama Newyork shida ni mfuko wako tu acha dharau
 
Shida ya kukimbilia Dar kwa mashemeji unakaa siku 2 ndo hii.Zunguka Dar uone uzuri wa jiji.Kiukweli hata kama unaishi keko machungwa bado kuna watu wanashi maisha mazuri huko,sasa kulalamika joto joto kutokana na jiografia ya mji.

Kama ni foleni hakuna jiji lina foleni Nairobi.Na pia kwenye jiji lolote kuna kuwa na masikini na matajiri pia.Hata Holiwood ukienda utakutana na masikini,N Y,L A ndo usiseme paris pia.Sasa unashangaa Dar au ndo ushamba wa kutosafiri.

Tafuta hela wewe utajenga hata ghorofa kwenye mkondo wa Nungwi na litasimama miaka hadi unaliacha.Mchawi pesa na umasikini wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Randy orton,
Hivi huko Dar mna BRT kama hii ya Jo'burg?
14052364_1092151040865317_1192054726_n.jpg
 
Back
Top Bottom