Witmak255
JF-Expert Member
- Feb 5, 2019
- 3,264
- 5,403
Picha hii imerushwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali hapa nchini ndugu Erick Shigongo. Ikiwa inaonesha mazingira magumu ya watoto hawa ambao wamekaa kwenye kijumba cha tope (kama darasa) na wakati huo huo mvua imenyesha na maji yamejikusanya ndani ya kijumba hicho (kama inavyoonekana).
Ni dhahiri kuwa mazingira ya wanafunzi wanaotoka katika familia maskini hapa nchini ni magumu sana, kiasi ambacho hayastahili kwa mtoto anaendaliwa kwa ajili ya kupata elimu bora ya kumsaidia katika maisha ya kesho yake na kulisaidia Taifa.
Ni kweli kuwa Serikali imeonesha kushindwa sehemu kubwa sana katika kuimarisha mazingira ya watoto hawa wale wanaoitwa "wanyonge" ambao ni tegemeo la kesho katika familia zao. Serikali imeshindwa kabisa kuboresha huduma hi ya Elimu hususani kwenye shule za Misingi.
Lakini turudi katika jamii zetu, hivi ni kweli kuwa jamii inayozunguka shule kama hii haioni hali ya watoto hawa?
Kwamba unaweza ikajichanga walau ikajenga darasa moja kwa ajili ya watoto hawa.
Hivi ni kweli kwamba eneo hili halina Diwani wa kuweza kuliona hili jambo na kulishughulikia kwa namna ambayo anaweza yeye?
Hapana!! Hapana!! Hapana!! Tusikubali kabisa kuwatelekeza watoto wetu katika mazingira haya. Huu ni utelekezaji wa watoto. Watoto kama hawa tunategemea waelewe nini hapa?
Hata mentality zao hazipo kabisa katika kuelewa.
Hebu jamii tusijisahau kwa kiwango hiki, ikiwa kuna mtu anatakiwa kuwajibika katika hili basi na awajibishwe na jamii hata kwa kumlazimisha kuwajibika.
Nimesononeka sana moyoni mwangu!! Maana hata Mimi nimesoma katika mazingira ya kawaida na magumu lakini si ya namna hii.
Tuwasaidie watoto hawa, hawana hatia.
Ndugu Eric Shigongo na wote mnaofahamu tusaidieni kufahamu mahala hii shule ilipo.