neno1
Senior Member
- Oct 9, 2013
- 196
- 141
Ni kawaida kibongo bongo au kiafrika kwa ujumla kulelewa na ndugu asiye mzazi wako. Yawezekana kutokana na uwezo mfinyu wa wazazi au kuchukuliwa kwao mapema na Muumba. Ila nilichogundua unaposaidiwa na ndugu siku ukitoka basi ujue unadaiwa.
Mimi ni kati ya niliolelewa na ndugu, akanisaidia kusoma hadi sekondari kabla ya kupata mkopo wa chuo. Sasa tangu nimepata kazi, nimejitahidi sana kusaidia watoto wa ndugu kulipa lipa ada lkn pia na wao wenyewe pale wanapokwama. Lakini nimegundua wanapokuomba kitu sio kwamba ni hiari utoe au la, kwao ni lazima utoe ilimradi wanajua una kazi haijalishi wewe una mikakati gani. Mbaya zaidi ionekane una fanya mambo yako makubwa kwao inakuwa kama ulistahili kuwafanyia wao kwanza. Halafu ikitokea pesa yako ikapita kwao, kuitumia kwao sio tatizo. Haya yote wanafanya kwa kigezo kuwa walikusaidia na huna cha kusema maana lawama ni tusingekuwa sisi usingefika huko.
Kwa ufupi nimejifunza kama unaweza lea watoto wako mwenyewe la sivyo unawaandalia deni la hadi mauti. Najua hata wazazi tunawahudumia lakini kauli kama za kwamba kama sio hao sio rahisi wazitoe maana wao ndo walikuleta na ilikuwa wajibu wao kukupa mahitaji yako.