Kama wana-cheat sijui lakini dah, hawa wanafunzi kama wanaenda A-Level za kawaida (za serikali), wengi wao huwa wanafeli; cjui kwanini!! Nakumbuka mwaka wetu, wanafunzi waliokuwa wametoka seminary schools wengi walifanya vibaya sana including na mkali aliyekuja darasani kwetu huku akiwa na msululu wa A's! Huyu Six alitoka na IV ya kutisha!!
Sasa sijui wakienda zile shule zetu wanakuwa ni kama kuku wa kienyeji walioachiwa kutoka bandani na hivyo wana-misuse uhuru, au sijui huwa wanakumbwa na nini!
USHAURI: Kama una mwanao kutoka hizo shule halafu amepangiwa shule zetu hizi; kama mfuko bado unaruhusu, mrudishe tena kwa V & VI huko huko alikotoka au shule nyingine inayofanana na huko alikotoka! Ukipuuza ushauri huu, yatakapotoka matokeo yake ya Form VI hapo baadae usijisahaulishe huu ushauri!
Kufeli wakienda A-level, kuna sababu kubwa hizi
1. Wawapo ST. FRANCIS, hawajifunzi ile self control ya awe wapi wakati gani... wanakwenda kwa kitimiza matakwa ya walimu au wafanyakazi wa shule, vinginevyo anaweza hata kurudishwa nyumbani
2. Waingia A-level ambao kwa sehemu kubwa huwa wanaachwa ikiaminika ni wakubwa... kumbe walikotoka hayo hawakuyazowea, matokeo yake wengi hawazingatii shule na kwa vile hakuna wa kuwahimiza, wengine hupotea kabisa
3. Historia ya walikotoka huwafanya waone kumbe mambo ni rahisi tu... na kwa vile wanajulikana shule walizotoka, hutazamwa kama wanafunzi wenye akili sana... hili hupelekea baadhi kubweteka na hatimaye kufeli..
4. Wakiwa kwenye shule kama ya ST. Francis, bajeti ya fesha huwa inakuwa controlled na walimu au wafanyakazi wa shule. Na huruhusiwi kuwa na fedha mkononi inayozidi kiasi fulani.. au utapewa kiasi kidogo per week. Hii huwafanya wasizoweze ku-control hela. Waingiapo A-level, fedha huachwa mikononi mwao... wengine huishia pabaya.
ALL IN ALL ULE UHURU WANAOKUTANA NAO WAKIA A-LEVEL NDO HUWA SABABU KUBWA YA KUFELI KWAO.... TENA UHURU WA GHAFRA MARA BAADA YA KUTOKA WALIKOKUWA HAWANA UHURU..
Huo ushauri wa kumrudisha shule za A-level za aina ile ile ni mzuri, ingawa wengine huwakuta hayo ya kufeli wakiwa vyuo vikuu...tena huko uhuru ndo balaa kabisa..!!