Kwanini Shule za Serikali za vipaji maalum hazifanyi vizuri mitihani ya kidato cha nne (CSEE) tofauti na ile ya kidato cha sita(ACSEE)

Chura

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,345
2,296
Hizi shule zinachukua wanafunzi wa wastani wa juu kabisa, yani wanafunzi waliofanya vizuri darasa la saba kwa kifupi wanachukua Cream tupu, Hapa naongelea shule kama Kibaha, Mzumbe, Kisimiri, Msalato, Tabora Boys n Girls , Kilakala na Ilboru .Shule hizi upande wa Olevel hazifanyi vizuri sana unakuta mpaka 0 za kutosha unabaki unajiuliza hii kweli ilikua Cream au samri? wakati mtoto alitoka shule ya msingi akiwa na Ufauru wa kutisha A zote anaenda kipaji maalumu kipaji kinayeyuka anazungusha yai.

Kwa Advance shule hizi kiukweli zinajitahidi na hapa tuangalie ulinganyifu wa ufaulu wa baadhi ya hizi shule kati ya Olevel(CSEE) na Advance (ACSEE) kwa miaka ya nyuma na sasa 2021

2️⃣0️⃣1️⃣6️⃣

1. MZUMBE (O LEVEL KITAIFA YA 27 ikiwa na div 4-1, na 3-12. ADVANCE KITAIFA YA 8)

2.ILBORU ( O LEVEL KITAIFA YA 42 ikiwa
na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 9)

3.KIBAHA( O LEVEL KITAIFA YA 1️6️ ikiwa na div 4-1. ADVANCE KITAIFA YA 7)

4.KISIMIRI (O LEVEL KITAIFA YA 592 ikiwa na div 0-22, 4-95, 3- 25. ADVANCE KITAIFA YA 1)

2️⃣0️⃣1️⃣8️⃣

1.KILAKALA (O LEVEL KITAIFA YA 76 ikiwa na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 14)

2.MSALATO ( O LEVEL KITAIFA YA 102 ikiwa na div 4-12. ADAVANCE KITAIFA YA 17)

3.TABORA GIRLS ( O LEVEL KITAIFA YA 90 ikiwa na div 4-4. ADVANCE KITAIFA YA 11)

4.TABORA BOYS ( O LEVEL KITAIFA YA 67 ikiwa na div 4-1.ADVANCE KITAIFA YA 15)

2️⃣0️⃣2️⃣1️⃣

kISIMIRI ( O LEVEL KITAIFA YA 404 ikiwa na div 4-60. ADVANCE KITAIFA YA 1)

KILAKALA ( O LEVEL KITAIFA YA 30. ADVANCE KITAIFA 56).

ILBORU (O LEVEL KITAIFA YA 23. ADVANCE KITAIFA .18)

MZUMBE ( O LEVEL KITAIFA YA 10. ADVANCE KITAIFA 10)

Baaada ya kuangalia viwango hivyo vya miaka ya nyuma mpaka karibuni utaona kabisa pamoja na kwamba shule za serikali zinachukua cream lakini wanashindwa kuzirutubisha ziendelee kubaki cream ambapo wengine hubadirika kutoka Cream kwenda maziwa mgando.kutoka kuingia na wastani wa A shule ya kipaji na kuchomoka na Div 4 au 0 ni hatari mno.

Ona shule kama Kisimiri unaweza kudhani wao labda wamejikita zaidi Advance na kuwaacha wale wa o level wapambane na hali zao shule Advance inakua ya 1 lakini O level 0 za kutosha na 4 wakati utaratibu kwa level zote ni ule ule kuchukua Cream.

Shida ipo wapi wazee wangu? Huku government hususani o level ni kwamba serikali inashindwa kuvilea vipaji vyenye umri wa balehe na kuweka mkazo zaidi kwa wanaojitambua maana Advance kidogo mtu akili inaelewa na kupambanua majambo.

Hii tofuati kabisa na shule za binafsi ambazo pia moja ya sababu za ufaulu wao mkubwa kuchukua cream inatajwa lakini mbona wenzetu wanawasha kote kote mfano Marian boys and girls, Feza Boys n Girls wakiwasha top 10 olevel unakuta na Advance wamo....Pia wenzetu wa Binafsi O level ambapo government inachechemea wao ndo wanawasha haswa si unaona Cream za KEMOBOS zote one , Cream za St Francis Zote one, Cream za Bright na waja zote one sasa kwa nini Cream zetu za O level ni ngumu kutoa one zote basi angalau muishie 3 kweli Cream mnailambisha 4 na 0 sijapenda aisee.

Eti wakuu mnaona sifa kuitwa wakuu wa shule special na kupewa kipaumbele cha kufanya selection? Wakati mikakati ya kumaintain vipaji vyetu ni 0 😱

Kwa nini yani Whyyyy jaman whhhhy ??
 
Ni kweli hayo uliyoyasema.

Binafsi, naweza kukupa sababu nne:

1: Mazingira kwenye shule hizi si wezeshi kama tunavyofikiri. Walimu, miundo mbinu na vitendea kazi. Walimu hawako hand in hand na wanafunzi wao kama zinavyofanya shule binafsi zinazofanya vizuri.

2: Kulingana na mazingira hayo hapo juu, A level husaidiwa sana na maturity yao. Huwa na mwamko wa kupambana na kujisomea. Kupambana kati yao wenyewe kwa performance na kutafuta zaidi hata nje.

3: Mentality ya uandaaji. Ushauri wa kulea vijana bado pia ni tatizo. Nani yuko karibu kuwapa ushauri wajihimize na njia kuu?

4: Motivation, ni ngumu kuizungumzia sana kwa sababu hawa watu wako kwenye mazingira yaleyale na shule moja. Ingawa inaweza kuwa sifa kulingana na kiasi cha mishahara na kujichanganya ili kujiongezea kipato. Ingawa kwa ujumla, mazingira ya shule zetu za serikali ni magumu jwa wafanyakazi wake.

Pamoja na mafunzo yanayopatikana pale, ni kila mmoja kula kwa urefu wa kamba yake.

Niliyaona kama challenge wakati wangu binafsi. Kuna mwalimu alikuwa anasema waziwazi:

1: " Kwanza mmekuja wengi sana, sitaweza kufanya practical na kusahihisha madaftari yote haya"

2: "Nenda kamwambie baba yako PCB imenishinda, naenda PGM au EGM, PCB siyo mchezo"

Hapo inabidi upige moyo konde na upambane maana huyo ndio mwezeshaji.
 
Ni kweli hayo uliyoyasema.

Binafsi, naweza kukupa sababu mbili.

1: Mazingira kwenye shule hizi si wezeshi kama tunavyofikiri. Walimu, miundo mbinu na vitendea kazi.

2: Kulingana na mazingira hayo hapo juu, A level husaidiwa sana na maturity yao. Huwa na mwamko wa kupambana na kujisomea. Kupambana kati yao wenyewe kwa performance na kutafuta zaidi hata nje.

3: Mentality ya uandaaji. Ushauri wa kulea vijana bado pia ni tatizo. Nani yuko karibu kuwapa ushauri wajihimize na njia kuu?

Pamoja na mafunzo yanayopatikana pale, ni kila mmoja kula kwa urefu wa kamba yake.

Niliyaona kama challenge wakati wangu binafsi.
Nimecheka ulivyomalizia kama Mtukufu Hangaya 😂😂😂😂😂😂😂
 
Itakuwa government skuls hazina walimu bora ama walimu wanaojituma. Nadhani ufaulu huo wa government skuls ni juhudi za wanafunzi wenyewe.

But, kwa kawaida praiveti kuna walimu wabobezi, wenye uzoefu, wanalipwa vizuri mishahara na marupurupu yote, uchumi mzuri, so mwanafunzi anafundishwa to the maximum.

Wanasema ufaulu wa mwanafunzi, 25% juhudi za mwalimu, 75% yeye mwenyewe. Sasa praiveti asimilia zote 100 walimu wanasaplai. Govamenti, asimilia almost zote ni juhudi za mwanafunzi.

See the difference?
 
Itakuwa government skuls hazina walimu bora ama walimu wanaojituma. Nadhani ufaulu huo wa government skuls ni juhudi za wanafunzi wenyewe.

But, kwa kawaida praiveti kuna walimu wabobezi, wenye uzoefu, wanalipwa vizuri mishahara na marupurupu yote, uchumi mzuri, so mwanafunzi anafundishwa to the maximum.
Kama hawajitumi mbona Advance wanafanya poa sana...miaka karibu mitatu mfululizo anaongozaga kisimiri?
 
Ni kweli hayo uliyoyasema.

Binafsi, naweza kukupa sababu mbili.

1: Mazingira kwenye shule hizi si wezeshi kama tunavyofikiri. Walimu, miundo mbinu na vitendea kazi. Walimu hawako hand in hand na wanafunzi wao kama zinavyofanya shule binafsi zinazofanya vizuri.

2: Kulingana na mazingira hayo hapo juu, A level husaidiwa sana na maturity yao. Huwa na mwamko wa kupambana na kujisomea. Kupambana kati yao wenyewe kwa performance na kutafuta zaidi hata nje.

3: Mentality ya uandaaji. Ushauri wa kulea vijana bado pia ni tatizo. Nani yuko karibu kuwapa ushauri wajihimize na njia kuu?

Pamoja na mafunzo yanayopatikana pale, ni kila mmoja kula kwa urefu wa kamba yake.

Niliyaona kama challenge wakati wangu binafsi.

Kama mtu kukamilisha Pihechidii yake lazima awe na profesa wa kumwongoza, seuze sekondari? Hata kama mwanafunzi ana akili inayokaribia kushabihiana na ile ya Thomas Edson ama Isaac Newton ama Kihombo au Profesa Majimarefu, if hana guidance ya karibu kutoka kwa mwalimu, ni vigumu sana kuweza kukompiti successfully na wanafunzi wengine kitaifa.
 
Kama hawajitumi mbona Advance wanafanya poa sana...miaka karibu mitatu mfululizo anaongozaga kisimiri?
Wewe Chura , haya mambo utayajulia wapi? Juhudi n'azozizungumzia ni kwa upande wa walimu. Ukweli ni kwamba sidhani kama wanalipwa mishahara ya kutosha, mazingira yao yakoje, maisha kiujumla na kadhalika. So, pengine kabisa hawana munkari wa kufundisha kwa hamasa na kujitolea, tofauti na skuli za praiveti.

Halafu kuna suala la kusimamiwa. Gavamenti skuls inawezekana kabisa walimu hawasimamiwi vilivyo ili kutimiza majukumu yao ipasavyo. Wanaweza kuchagua kufundisha au kutofundisha muhula mzima, na hakuna wa kuwauliza. Hiyo haiwezi kutokea kwenye praiveti skuls.
 
Wewe Chura , haya mambo utayajulia wapi? Juhudi n'azozizungumzia ni kwa upande wa walimu. Ukweli ni kwamba sidhani kama wanalipwa mishahara ya kutosha, mazingira yao yakoje, maisha kiujumla na kadhalika. So, pengine kabisa hawana munkari wa kufundisha kwa hamasa na kujitolea, tofauti na skuli za praiveti.

Halafu kuna suala la kusimamiwa. Govementi skuls inawezekana kabisa walimu hawasimamiwi vilivyo ili kutimiza majukumu yao ipasavyo. Wanaweza kuchagua kufundisha au kutofundisha muhula mzima, na hakuna wa kuwauliza. Hiyo haiwezi kutokea kwenye praiveti skuls.
If so mbona humo humo wengine wanapiga 1 kali wengine wanalamba 0?
 
Hapo kisimiri itoe kwa upande wa olevel wanasoma wamasai na wameru tena wanatokea kule milimani hao hawanaga mpango wa kusoma kabisa, na boarding ni kwa advance tu so ni kama shule ya kata na sio kipaji maalum kwa olevel
 
Kidato cha nne mitihani mingi ukilinganisha na kidato cha sita.
O-level walioko special schools sio wote ni special, wengine walipiga multiple choice na majini wakatusua, wengine walipewa majibu.
Sasa A-level mtu akifaulia special school huyo ni special haswa.
Mwaka niliomaliza la saba tulipofika form one lilipopigwa pepper la form 2 kibaha ilitema watoto wengi tu.
Jambo jingine ni kwamba hizi shule Bado zinafanya vizuri sana tatizo ni pale wewe unapoleta comparison na hawa wafanyabiashara Waturuki n.k
 
Hapo kisimiri itoe kwa upande wa olevel wanasoma wamasai na wameru tena wanatokea kule milimani hao hawanaga mpango wa kusoma kabisa, na boarding ni kwa advance tu so ni kama shule ya kata na sio kipaji maalum kwa olevel
Mnajiandikia tu ngoja nikupe stori ya Kisimiri nje ndani mtu wangu tena kiufupi kabisa 9aliyeanzisha ni Prof mmoja Mswizi anaitwa Karafiat ambaye pia alijenga shule ya msingi Kisimiri kama asante kwa wanakijiji wa pale kwani wazazi wake mwamba waliishi maeneo hayo ambayo ni chini tu ya mlima Meru. ...yule mzungu akasepa kumbuka wakati huu ilikua private wakilipa kidogo baadae sasa akarudi unacheki? Jamaa alirudi kutembelea shule akiwa na rafiki yake Prof. Nava Setter ambaye alikuja na wazo la kuanzisha Advance na alijenga madarasa manne, Labaratory tatu pamoja na mabweni mawili ya wanafunzi wa kike . Hapo ndipo A level ikaanza. Hapo Kisi ikiwa na o level mixer na Advance yenye mabweni ila kwa wanawake tu...Baadae shule yote ikataifishwa na serikali ikawa mojawapo ya special schools Tanzania ila ndio special school pekee ambayo ni mchanganyiko maana tunajua nyingi ni single schools( katibu wa wizara wakati ule ndo ali icertify kuwa special ila kwa olevel ikabaki day ambayo inachukua Cream za wanafunzi wa eneo hilo. Kwa Advance ikawa boarding ambapo cream zinachukuliwa all over the country kama unabisha jaribu kwenda kumuombea nafasi mwanao olevel pale Kisi kama utapata akiwa na ufauru mdogo.
 
Ni kweli hayo uliyoyasema.

Binafsi, naweza kukupa sababu nne:

1: Mazingira kwenye shule hizi si wezeshi kama tunavyofikiri. Walimu, miundo mbinu na vitendea kazi. Walimu hawako hand in hand na wanafunzi wao kama zinavyofanya shule binafsi zinazofanya vizuri.

2: Kulingana na mazingira hayo hapo juu, A level husaidiwa sana na maturity yao. Huwa na mwamko wa kupambana na kujisomea. Kupambana kati yao wenyewe kwa performance na kutafuta zaidi hata nje.

3: Mentality ya uandaaji. Ushauri wa kulea vijana bado pia ni tatizo. Nani yuko karibu kuwapa ushauri wajihimize na njia kuu?

4: Motivation, ni ngumu kuizungumzia sana kwa sababu hawa watu wako kwenye mazingira yaleyale na shule moja. Ingawa inaweza kuwa sifa kulingana na kiasi cha mishahara na kujichanganya ili kujiongezea kipato. Ingawa kwa ujumla, mazingira ya shuule zetu za serikali ni magumu jwa wafanyakazi wake.

Pamoja na mafunzo yanayopatikana pale, ni kila mmoja kula kwa urefu wa kamba yake.

Niliyaona kama challenge wakati wangu binafsi. Kuna mwalimu alikuwa anasema waziwazi:

1: " Kwanza mmekuja wengi sana, sitaweza kufanya practical na kusahihisha madaftari yote haya"

2: "Nenda kamwambie baba yako PCB imenishinda, naenda PGM au EGM, PCB siyo mchezo"

Hapo inabidi upige moyo konde na upambane maana huyo ndio mwezeshaji.
Umenena kweli tupu.
 
If so mbona humo humo wengine wanapiga 1 kali wengine wanalamba 0?
Just imagine now, kwamba hata kwenye mazingira hashirifu kama hayo, halafu wakafundishwa kwa ukaribu na walimu wenye hamasa na uwajibikaji, matokeo yangekuwa bora kiasi gani, if hata sasa bado wapo wanaotusua?

1. Environment
2. Teachers--their munkari, availability, uwajibikaji
3. Materials. As we speak, there are many government schools whose teachers (and therefore their students) don't even know if and when a new syllabus has come, until some years forward. Huu ni mfano mdogo tu. Text books? Basic materials? Items na tools za praktiko? Maabara? Laibrari?

On the other hand, private schools are mostly VERY responsible and always handy. The supervisors and managers and the boards have a single-handed purpose of seeing their students succeed.
 
Pengine nitakuwa nje ya mada lakini naomba kujuzwa wakuu.

Hivi kuna uhuisho(justification) gani wa kupima wanafunzi wenye vipaji maalum walioko kwenye shule bora kabisa,(ziwe za serikali au private) kwa mtihani huo huo unaoutumika kupima wanafunzi wasio na vipaji(au wenye vipaji kiduchu), wanaosoma kwenye mazingira magumu yasiyo rafiki kwa wanafunzi wenyewe na hata waalimu wao?

Lengo la serikali katika kuzitenga hizi shule za vipaji maalum ni lipi hasa ikiwa kwenye ngazi za juu za elimu mwenye PCM ya Ilboru na yule wa Dr Olsen( ni mfano tu) wote wanajumuika hapo COET kusomea Civil Engineering?
 
Umeongea bonge moja la Point sikuwahi kuzani
 
Back
Top Bottom