Kama taifa tunaweza kufungua Account maalum

Kama taifa tunaweza kufungua Account maalum

Nchi zote zilizoendelea zilipata viongozi wenye maono wenye vipaumbele viwagusavyo wananchi ili wachochee uzalishaji.Kutegemea mikopo kisha kuwekeza pasipo Na tija au tija ndogo ni kuliuwa taifa
 
Wananchi wakishiba wataipenda serikali yao wakisomeshwa namba wataichukia hii ni principal
 
Siku za nyuma niliwai kupata wasaa wa kutafakari hili swala la kuwa na account maalumu kuhusu ujenzi wa nchi.

Kwamba kila Mtanzania awe anachangia kuanzia elfu moja na kuendelea kwa jinsi anavyojiskia.

Naamini kupitia hivi kwa mwaka tutakuwa tunaingiza mabilioni ya pesa na zote zitakuwa zinaingia kwenye miradi mikubwa ya kitaifa.

China, Marekani, Ulaya na kwingineko walipiga hatua kwenye medani za kiuchumi kwa kufanya maamuzi magumu kama Taifa.

Tuachane na dhana za misaada kila uchao ambazo nyingi zimekuwa na masharti magumu na masimango yasiyoisha.

Mzee Mkapa aliweza hili kwenye barabara za ndani kupitia Road Fund.

Ni rai yangu kwa Mh. Rais Magufuli atalifanyia kazi hili suala kwamba ifunguliwe account maalumu ya kitaifa ili Watanzania tuweze kuchangia na kuona fahari kujenga Taifa kwa pesa zetu wenyewe.

Alex Fredrick

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi mawazo yako yamekuwepo tangu mwaka 1984 lakini utashi wa Ccm katika hili haupo. Ela zinazotumika kununua wapinzani zingeweza kuondoa tatizo uhaba wa madawa katika hospital za umma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu hajaongezewa mshahara kwa miaka almost mi5 atapata wapi muda wa kufikiria kuchangia hela ya nini sijui.

Je kodi yetu inaenda wapi?

Ukinunua gari tu unapigwa kodi sawa and simtimes inazid bei ya gari lenyewe.
MATAGA msitukasirishe aisee tuacheni tuuguze mbunge wetu
Gharama ya kuingiza GARI nchini ni kubwa kuliko hata gharama za kuzalisha GARI kiwandani nje
 
Umelipa kodi toka siku unazaliwa, lakini unaamini mchango utakaojiamulia mwenyewe ndio suluhisho la kukuletea barabara?
 
Back
Top Bottom