Kama Taifa hatujui tulipo wala tunapoelekea

Kama Taifa hatujui tulipo wala tunapoelekea

Habari wanajamvi!

Naam hakika unaweza kusema pasipo mashaka yoyote kwamba sasa kama Taifa ujinga wetu umefikia full tank.Tumekuwa hatujui wapitulipo na wapi tunaelekea. Walau wachache wanajua tulipo toka. Tunabishana hata mambo ya msingi kabisa kwasababu za kisiasa tuna acha Taifa likiangamia na kufedheheka. Kisa wanasiasa na siasa. Ujinga ulioje?

Tazama,thamani ya Shilling imeshuka kwa kiwango kikibwa sana kuliko wakati wowote tangu tupate Uhuru. Kwasasa Dollar moja ya Marekani ni sawa na shilling 2548 za Tanzania. Au Shilling moja ya Kenya ni Shilling 28 za Tanzania. Badala ya kukaa chini tutafakari nini kimesababisha jambo hili kutokea? Tunakuja na sababu za kisiasa eti tunahujumiwa!! Kwanini wasomi waseme hivi? Wanajua ili wabaki salama ni bora waseme hivyo kuliko kuusema ukweli mchungu. Ukweli una tabia moja huwa haumpambi mtu. Hapo ndipo walipo ogopa kusema ukweli kwasababu watawakwaza wanasiasa. Bora Taifa liangamie kuliko kuonesha kuwa wana siasa wamekosea hapa au pale. Kizazi cha wanafikh!

Je, Shilling itaendelea kuporomoka? Hakika itaendelea kuporomoka zaidi na zaidi. Yafaa tuchukue hatua muafaka sasa tena bila kuchelewa. Hatua gani tuchukue? Ni lazima tuchukue hatua zifuatazo:-

. Kwanza, lazima tujenge mazingira ya kuaminika Kati yetu na wenye mitaji. Tabia ya kubadili gia angani
kuhusu mazingira ya uwekezaji imewafanya wawekezaji wengi kuwa na mashaka na mitaji yao.

. Pili, Biashara ya utalii imevurugwa sana siku za karibuni kwa kuweka kodi mbalimbali kuwa juu kuliko
Nchi jirani. Purukushani anazo fanya Kigwangala zitazidi kuporomosha mapato. Kwenye tatizo ni bora
kutumia diplomasia kuliko ubabe wa madaraka.

. Biashara ya dhahabu na makinikia ni lazima tukubali baadhi ya mambo yaende kama wawekezaji walivyo
Ingia mikataba hapo awali.

. Kunyantasa wawekezaji wenye mitaji mikubwa ni kujichimbia kaburi kiuchumi. Ni lazima tuheshimu
Mikataba iliyo ingiwa .

. Tuongeze uzalishaji wa bidhaa na huduma za kuuza Nchi za Nje.

Nini tutegemee? Bidhaa zote tutakazo agiza sasa zitapanda bei mara dufu. Maisha baada ya Desemba,2017 yatakuwa ni shida. Bidhaa zote zitapanda bei. Twafa twafa!
Wacha uwoga wewe!!!! Lazima tuwe smart sawa!!! Lakini sio waoga, kama kuna wizi au dhuluma hao wageni walitufanyia kwa mfano huko kwenye madini na mali asili na utalii wacha tuweke mambo sawa kwa faida ya kesho. Kama itabidi tulipe kwa uchumi kuyumba tuwe tayari kukabiliana na hilo mwisho wa yote tujue Tanzania ni lulu watakuja kukaa chini tukubaliane biashara kwa faida yetu. Wasiwasi wangu je hawa tulio wapi dhamana ya kushughulikia hili wakweli????!!! Wana nia njema kweli au ndio ni kupata mitaji ya kisiasa tu!!! Tuombe Mungu wawe kweli wana nia njema na nchi lakini kama nia ni kushinda mchezo wa kisiasa tu basi tumekwisha!!!! Twende mbele...
 
Watanzania daini katiba mpya ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana
 
Ndio hapo ninapo ona ujinga umejikita chini kuliko kawaida. Uchumi ukiporomoka zaidi itafika mahali hata kuagiza viberiti hatuta weza. Mtabaki kusifia wanasiasa eti ni jembe. Hapa tulipo fikia kuna jambo hata wajinga watajifunza. Let us wait and see.
Haitafikia huko kamwe
 
Back
Top Bottom