Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,638
- 697,929
Ni mbinu fulani ya kimafia kuwapata unaowataka huku ukiupambaza umma kwa kuanzisha kampeni fulani, ambayo huanza kwa mbwembwe nyingi na mwishoni wakishapatikana watarajiwa mambo huisha kimyakimya.
Tumeyaona haya kwenye vita ya madawa ya kulevya(madaraka ya kulevya) nchi ikazizima ikawa ni kampeni ya safisha nchi/dar, wakakamatwa wa kukamatwa, tukaletewa na wahanga (watoto wadogo) wakatoa ushahidi kisha mambo yakaisha kimyakimya.
Limekuja hili la kodi, ambalo ni faraja ya wengi, tumechoka kuwa ombaomba wakati tuna kila kitu na wachache wanafaidi kwa kutolipa kodi, tunahitaji kodi ili kupeleka maendeleo ya nchi mbele, hospital ziwe na madawa na vifaa tiba, shuleni kukamilike, miundombinu iwe bora nk... Tunahitaji pesa.
Kufungiwa kwa Star TV ni kielelezo tosha kwamba hii vita haina macho ya makengeza. Walikuwa wanadaiwa BILLION NNE na ushee, kisha wakaja mabepari wa madini wakapigiwa mahesabu yaliyozua mijadala dunia nzima.
TRILLION 425 hivi, Hawa ni wezi bila kujali wana bei gani kibindoni! Walipe walichotuibia ili iwe fundisho kwa wengine.
Masikitiko yangu!
Je kodi iliyokwepwa kuiba ina mazungumzo? Kwamba kama ukikubali kosa basi upunguziwe ama usamehewe? Je star TV wamelipa ama wamepunguziwa au wamesamehewa? Kama wamelipa wamelipa bei gani? Kupitia akaunti gani? Kama kwa Star TV imekuwa hivi kwa ACACIA haiwezi kutokea?
KILINGE leo kikavu hakuna wateja hakuna kabisa nakuja mjini kubangaiza chenchi za kodi
Sent using Jamii Forums mobile app