Kalbandika
Member
- Oct 10, 2010
- 40
- 25
Nakumbuka kamsemo kazamani kidogo pale mtu unapopata kitu kizuri halafu bado unalalamika. Utasikia mtu anakuambia 'Mungu akupe nini, au gunia la chawa?
Hii ni kauli ambayo inatolewa kwa watu ambao hawana shukrani, hawana jema. Kila kitu kwao kibaya. Ukiwa mkali utasikia dah, fulani mkali sana. Ukiwa mpole utasikia dah, fulani mpole sana. Ukiwa kati kati, utasikia dah, fulani haelewiki.
Hakika, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutujalia kumpata Rais Magufuli. Wengi wasiofikiri vizuri wanaponda kila kitu bila kuangalia uhalisia wa jambo husika.
Mfano mzuri, Mheshimiwa Rais Magufuli amesema wazi juu tetemeko la ardhi lililoharibu vitu na watu Mkoani Kagera. Amesema wazi Serikali haina uwezo wa kusaidia kila kitu. Inabidi jamii na watu wenyewe tufanye kazi na kusaidiana. Haiwezekani mtu nyumba yake imepata ufa anasubiri Serikali ije irekebishe ufa.
Rais wetu ni mkweli, hana ubabaishaji. Nyeupe anasema ni Nyeupe, na nyeusi ni nyeusi.
Watanzania mnataka nini badala ya JPM? Mheshimiwa Waziri Mkuu amepewa kazi ya kusimamia urejeshwaji wa hali ya Mkoa wa Kagera. Ameambiwa wazi kabisa na Mhe Rais juu ya matumizi yenye tija ya michango.
Tumuunge mkono JPM, tuache kufuata maneno ya wanasiasa wa matukio.