BABYLON,
Hata huko Zimbabwe kuna watu wanasema kama sio Mugabe, Zimbabwe wasingekuwa Huru leo.....sidhani kama maneno haya yana ukweli, na hata kama upo haufuti machafu ya mtu huyu...Waswahili wanasema Mzazi (baba) sio kutunga mimba kwani kila mwanamme rijali anaweza, baba ni yule anayeweza kulea vizuri hadi mtoto akakua!
Hivi ni kweli Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi alitaka kuvunja muungano?
Nini kilikuwa kiini cha "machafuko ya hali ya hewa" Zanzibar yaliyopelekea kujiuzulu kwake?
Seif Sharif Hamad alimchongea nini kwa Nyerere wakati akiwa waziri kiongozi?
Hamad aliteta nini na Nyerere Butiama baada ya kutoka CCM?
Junius,Kama kuna binaadamu m-binafsi hapa Tanzania aliyewahi kuishi basi Nyerere anaongoza, si kuwa aliifuta historia ya mashujaa wengine waliotoa mali zao na roho zao kwa nchi hii bali aliwafanya wakaonekana maadui wa nchi hii, na kujigeuza yeye kwa kila sifa inayomstahiki na isiyomstahiki,mbali na Jumbe watu kama Bibi Titi Moh'd, Oscar Kambona,Kasela Bantu n.k waliomtengeneza na Kumpromote Nyerere enzi hizo, walifikia hata kutoa fedha na mali zao kumpeleka Nyerere U.N akawasemee kwa kuwa tu alijua kingereza, wengine walimbeba hata pale alipotaka kupinduliwa (Oscar kambona), shukurani za mtu huyu kwa watu wote hao ni kama za punda, aliwapiga mateke na kuwanyanyasa kama vile hakuwahi kuwajua seuza kupata hisani zao,Manyanyaso aliyomfanyia BB TT, kwa kisingizio cha kutaka kumpindua, yanasikitisha hata leo ukiyasoma tu, lau kama kungekuwa na vyombo vya habari siku hizo kama ilivyo sasa vikapaza sauti zao kwa madhila waliyofanyiwa "mashujaa waliosahaulika" nchi hii na "kufutwa" historia na michango yao ya ujenzi wa taifa hili na Mwalimu Nyerere kwa makusudi, hakuna mtu angelitoa chozi lake kwa kifo chake.
JASUSI.
Hivi si kweli kuwa Mwalimu alipanga Propaganda hizi, kwasababu "mbovumbovu" na akazigandamiza katika vichwa vya "wanafunzi" wake kama nyinyi ambao,alikuimbisheni unafiki,mkaitikia ndo ukweli,alikusomesheni batili mkasema haki,alipanga hila na madhila kwa wote waliotaofautiana nae,kama Kambona alitaka kumpindua kwanini asitumie fursa ile ya maasi ya kijeshi1960s ambao walikuwa wakimsikiliza yeye tu wakati ule, aje asubiri badae? BB TT kukataa "ujamaa,azimio la Arusha na kudhulumiwa watu mali zao" ndo alistahili kitanzi? basi ni afadhali angempiga kitanzi kuliko kumpeleka kule kiinua miguu zanzibar,na kuvuliwa nguo na watoto wadogo wa kuwazaa kama si kuwajukuu,ama kweli ww "umekhitimu" mafunzo ya "Mwalimu" wako? na kweli unadumisha "fikra" zake. Usitake kukataa kama fedha za safari ya U.N zilichangwa sikusema Mzee Rupia hakutoa, pengine yeye alitoa nyingi hasa, lakini juhudi hizo zilifanyika kwa pamoja, na walimuwezesha kufanikisha kawarudi kinyume.
eti kuwa BIBI TITI na WENZAKE WALIPANGA KUMPINDUA,MAANA WAKATI ANASHIKILIWA KULE KIINUA MIGUUU, ALILAZIMISHWA AWATAJE WATU JUST FOR "IMPLICATION" KWA MAAGIZO YA MWALIMU, WATU "WALIOMSHUGHULIKIA" BADO WANGALI HAI HAPA NA TUNAO, HAWAFICHI KITU WANASEMA WAZI WAZI....Propaganda zipi unazozizungumzia rafiki yangu? Sijakuelewa.
Hivi ni vitu vinahitaji kuwekwa wazi wakati huu-kwa manufaa ya historia ya nchi yetu na vizazi vyetu vijavyo. Hivi nini kilijiri. Msituambiue tu -Kuchafuka kwa hali ya hewa ya Kisiasa. Hii ni khushi- haijitoshelezi.Hivi ni kweli Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi alitaka kuvunja muungano?
Nini kilikuwa kiini cha "machafuko ya hali ya hewa" Zanzibar yaliyopelekea kujiuzulu kwake?
Seif Sharif Hamad alimchongea nini kwa Nyerere wakati akiwa waziri kiongozi?
Hamad aliteta nini na Nyerere Butiama baada ya kutoka CCM?
Usicheze na Mwalimu wewe. Ni mweledi. Na mjanja. na Mlaghai. Anachokitakam kiwe huanza kukipinga na kuwazubaisheni kumbe huku anakifiringa. Acha tu wewe na hadithi yake- Zanzibar haiwezi kumezwa. Amefanya nini?Kwa wote wana-JF waliochangia mada hii hadi sasa, mnasahau kwamba wakati Jumbe (pamoja na wengine) alipokuwa anajibidiisha kuiasisi CCM, hakujua kwamba yangemkuta yaliyomkuta. Ne mengineyo mengi yanayowakuta Wazanzibari hadfi kufikia majuto kwa wengi wao.
Kwa Wazanzibari, kuanzishwa kwa CCM kulikuwa 'ironical' -- kwani ilikuwa ni mwanzo wa mwisho wa 'sauti' huru ya Wazanzibari, kwani baada ya hapo masuala yote kuhusu mustakabali wa visiwa hivyo yalikuwa yanaamuliwa Dodoma. Hata masuala ya kuchagua viongozi wao.
Matokeo yake ni kwamba CCM imeziduwaza na kuzidumaza fikra za Viongozi wa Zanzibari kiasi kwamba misimamo yao mingine inasikitisha kweli kweli.
Nitatoa mfano. Ktk uchaguzi wa 2005, pamoja na kwamba ilionekana kuwa ni zamu ya Visiwani (ingawa haiko ki-Katiba) kutoa rais, na kwamba walikuwa na candidate ambaye alikuwa very strong, viongozi wa huko, kwa sababu zisizokuwa na msingi kabisa, waliamua kuwa potelea mbali, na kuonekana kuwaambia watu wa bara: "endeleeni tu nyinyi kutoa Rais tena! Sisi hapana."
Halafu hapo hapo wanapiga kelele ya kutaka usawa baina ya pande mbili za muungano!
Nawaheshimu sana wazee wetu waliopo na waliondoka. Mzee Thabit Kombo ana kosa la kuichukua Shirazi Association kuiunganisha na African Association kuunda ASP. Mzee Aboud Jumbe ana makosa zaidi ya kuichukua ASP kuiunganisha na Tanu kuunda CCM. (Naomba radhi kama nimewakwaza wanasiasa)- Naongelea kwa mintarafu ya historia tu.Mzee Aboud jumbe kama binadamu mwingine ana upungufu wake lakini chakushangaza leo serekali mbili hizi hawataki hata kuyazungumzia yae mazuri aliyowafanyia pande mbili hizi za Mungano .kama asingelikubali kunganisha chama cha ASP ule mwaka 1977 kusengekuwapo na CCM, leo ukiwauliza wanafunzi hawamjuwi Mzee aboud jumbe ni nani wao wanambiwa tu muanzishi wa CCM ni mwalimu nyerere, lakini ikumbukwe historia ipo siku itabainisha hili na mengine.nakumbuka kama leo siku ile ya kunganishwa ASP na TANU mzee wetu shekh Thabit Bin kombo mtumzima alitokwa na machozi machozi yale yalikuwa na maana yake .leo imefika pahala hawa watu hawataki hata kuyaeleza au kulitaja jina la mzee Aboud lakini tusijisahau kuwa hakuna aliyejiumba, hapa wanamsubiria ili waje watueleze ambayo wanataka wao tuyasikie. Mungu ampe afya nzuri mzee wetu baadhi yetu hatuto msahau kwa mazuri aliyotuletea na tupo tayari kumsamehe kwa makosa aliyofanya ambayo leo hii yanatukosesha usingizi.
Junius,
Hivi si kweli kuwa Bibi Titi alishiriki katika mipango ya kumpindua Nyerere? Pamoja na Kambona? Ubinafsi unaousema ni upi? Wa kumsamehe Bibi Titi asiwekwe kitanzi? Aliyetoa fedha zake kumpeleka Nyerere UN alikuwa Mzee Rupia. Kambona naye alibebwa tu na TANU. Aliifutaje historia ya mashujaa? Ni wapi Nyerere ameandika historia ya juhudi za ukombozi? Acheni kupindisha ukweli wakati tunaoujua ukweli bado tupo hai.