Kama si Mbowe, basi mtoto wa Mbowe, kama si Kafulila, basi mjukuu wa Kafulila n.k

Nimewataja hao kuwakilisha wapinzani wa nchi hii ambao wamefanya kazi kubwa tena kwa miaka mingi na katika mazingira magumu sana ya kisiasa kumtetea mtanzania masikini wa nchi hii.

Katika kuwaombea kwa mungu nasema, kama si Mbowe, basi mtoto wa Mbowe aje kuwa raisi wa nchi hii; kama si Kafulila, basi mjukuu wa Kafulila aje kuwa waziri katika serikali ya nchi hii; kama si Tundu Lisuu, basi mjukuu wa Lissu aje kuwa Raisi wa nchi hii; Kama si Halima Mdee, basi mtoto wa Halima Mdee aje kuwa makamu wa raisi wa nchi hii.

Nawaombea kwa mungu awajalie uzima ili siku moja basi, kwa mapenzi yake, waje washuhudie watoto wao wakikamilsha kazi walioianza.

Ni sera na kelele za wapinzani hawa ndio leo hii zinamuwezesha mtoto wa masikini kule kijijini kupata elimu bure n.k.

Fadhila pekee iliyobaki kwa wanasiasa hawa ni Mungu kuwalipa kupitia vizazi vyao.
Umelaaniwa wewe. Fisadi mbowe hawezi kuwa rais na ukoo wake wa wezi. Mbowe na chadema wote ni wezi.
 
Eti Ridhiwan hafanani na baba yake!! Umechunguza?

Vitu vinavyo mjenga mtu ni pamoja na shida alizopitia kufikia hapo
Kikwete hakuwa na Baba CCM au watu wa kumbemba kupata ubunge
alifika hapo kwa jitihada zake.....Ridhiwani kawa mbunge huku baba yake ni Rais..
hawawezi kufanana
 
mimi niliwahi kusema siku ikitokea mbowe, lissu, na wengine wakaacha siasa basi tutegemee nchi kukosa watetezi , kwa sababu hata siku moja mtetezi wa wanyonge hawezi toka ccm. tuombe mungu awape roho ya uvumilivu ili waendelee kuwapigania watanzania

Hiv kabla ya mbowe na lissu hakukua na watu...hawa wakiacha kuna wengine wapo na watakuja...msitulishe matango pori hapaaa
 
Hili wazo siliungi mkono.
Yatakuwa yaleyale ya CCM ,kurithiana na kufanya uongozi uwe wa kwa ajili ya faida na sio utumishi
 
Nosense !!


nimewataja hao kuwakilisha wapinzani wa nchi hii ambao wamefanya kazi kubwa tena kwa miaka mingi na katika mazingira magumu sana ya kisiasa kumtetea mtanzania masikini wa nchi hii.

Katika kuwaombea kwa mungu nasema, kama si mbowe, basi mtoto wa mbowe aje kuwa raisi wa nchi hii; kama si kafulila, basi mjukuu wa kafulila aje kuwa waziri katika serikali ya nchi hii; kama si tundu lisuu, basi mjukuu wa lissu aje kuwa raisi wa nchi hii; kama si halima mdee, basi mtoto wa halima mdee aje kuwa makamu wa raisi wa nchi hii.

Nawaombea kwa mungu awajalie uzima ili siku moja basi, kwa mapenzi yake, waje washuhudie watoto wao wakikamilsha kazi walioianza.

Ni sera na kelele za wapinzani hawa ndio leo hii zinamuwezesha mtoto wa masikini kule kijijini kupata elimu bure n.k.

Fadhila pekee iliyobaki kwa wanasiasa hawa ni mungu kuwalipa kupitia vizazi vyao.
 
Binadaaaaaamu!!!Mbowe,Tundu Lissu,Kafulila ni watetezi wa wanyongeeeeeee!Akili ni nywele
 
Back
Top Bottom