Kama serikali imefilisika si bora kuwaweka wananchi wazi?

pesa inayotumika sana katika selkali ni ya nje :mfn dola nk ni pesa ya kigeni,nikupe mfano unalima mtama ila watoto wako hawali bali wanakula wali na wewe mchele unanunua na pesa ya kununua kila siku huna ,hapo hakika ipo siku watalala njaa
pesa za kodi nizakuzungusha humu ndani tu.ndio maana utasikia wanaenda kuomba kwa wenye nazo
 
Watu wengine huwa nashindwa kuwaelewa sijui hawafikirii au wanatoa uzi wakiwa wamelewa?
 
Mkuu sio kweli kwamba serikali imefilizika,waliofilizika ni wapiga deal.Ila natambua pesa za wapiga deal ziliongeza mzunguko wa pesa chafu.
Sasa usitafute mchawi jibu lipo wazi kwamba tulibweteka kwa kutegemea misaada na wapiga deal inatakia kusimama wenyewe kwa uhalisia na ukweli.
Ni aibu kupiga kelele ya mikopo ya sh milioni 2 kwa mwaka vyuo vikuu,wakati wananchi wazalendo wanalipia shule za msingi milioni 2 hadi 3 kwa mtoto mmoja.
Ifike mahali tutumie vichwa vyetu kufikiri na sio vinginevyo,kelele za chura hazimzui ngo'mbe kunywa maji
 
Watanzania tunalipa kodi kibao cha ajabu hatujui hizo pesa zinakokwenda, yaani ni Kama vile Kuna kikundi cha viongozi hukaa na kujigawia, Wakati wa utawala wa Nyerere Serikali ilikuwa na Mapato kidogo sana yaliyotokana na Faida ya viwanda vyetu

Wakati wa Nyerere hakukuwa na mitandao ya simu za mikononi wala vocha, hakukuwa na magari mengi na kwa hiyo ushuru uliotokana na mafuta na magari ulikuwa ni kidogo sana, bandari haikuwa na mizigo mingi Kama sasa kwa kifupi mambo mengi yalikuwa ndiyo yanaanza

Lakini Nyerere alisomesha bure, hospitali bure madawa bure, huduma nyingi za kijamii ilikuwa ni bure, Mungu amrehemu.

Tofauti na sasa, ukipiga hesabu ya ushuru tu ya magari yote hapa ambapo kila mwaka kila gari linalipa average ya laki nne litembee au lisitembee, ushuru wa mafuta yanayotumika kila Siku ni fedha nyingi mno, ushuru ktk muda wa maongezi kwa Siku ni fedha nyingi mno, VAT inayolipwa serikali ni fedha nyingi mno,

Pesa ya mauzo ya gesi yetu ni nyingi mno, Mirabaha ya madini ni fedha nyingi mno, pesa za watalii ni nyingi mno, fedha ya maliasili, mbao ngozi ushuru wa wanyama, ushuru wa mazao.ni nyingi mno,

Nataka kujua, hizi pesa zote huwa zinakwenda wapi ikiwa, maafa kidogo tu yakitokea serikali inaanza kutembeza bakuli Kama matonya, kila Siku tunaona ktk tv. Wagonjwa wakiomba msaada wa matibabu kutoka kwa hao hao walipa kodi. Kila Siku tu nasikia Mapesa kibao ya misaada toka Ulaya America China India, na mamikopo kila uchao, kutoka mabenki ya Africa na World bank.

Serikali ebu acheni Masihara tuambieni hizi pesa zote Zimekwenda wapi?. Hospitali siyo bure tena, kwa kifupi huduma zote za jamiii ni ghali Sana,

Kama mmefilisika tuambieni, lakini hatutaki tudharaulike na nchi Majirani kwa ajili yenu!.

Tumia tarakimu.
Unaposema nyingi mno unamaanisha nini?
 
Kupanga ni kuchagua mkuu..

kwa hiyo ni bora kuruhusu dili na rushwa, kukopa kwa sana hata mishahara ya wafanyakazi, kufanya semina makongamano, safari za nje, watumishi hewa, ili kusudi hela ipatikane mtaani?? au kupunguza hayo niliyoyasema hapo juu ili tuweze kujiendesha kwa mambo yetu na kukopa pesa kwa miradi mikubwa ya maendeleo??

Magu has choosen the second option.. Swali ni kwako, ungechagua lipi??
Simaanishi watu waishi kwa kupiga Dili, la! Ila kwa hali ilivyo kwa sasa ni dhahiri watu wamejenga chuki kubwa sana na Serikali Yao. Hii inatokana na ugumu wa maisha tofauti na mtawala aliyepita, sasa Kama mianya yote ya kifisadi imezibwa, kwanini wananchi hawaoni hizo pesa zikishuka kuja mikononi kwao Kama walivyoahidiwa.

Pesa ya maafa ya tetemeko ni uthibitisho tosha kuwa Serikali haipendi wanyonge Kama inavyojinasibu. Ni thahiri kuwa Serikali inafurahia maisha ya wananchi wake kuwa magumu, coz, hata ktk vitabu vya Mungu imeandikwa, "ukimpa Masikini nyama awagawie wenzake, itamuozea Mikononi." This is what happening now.
 
Mku
Mkuu sio kweli kwamba serikali imefilizika,waliofilizika ni wapiga deal.Ila natambua pesa za wapiga deal ziliongeza mzunguko wa pesa chafu.
Sasa usitafute mchawi jibu lipo wazi kwamba tulibweteka kwa kutegemea misaada na wapiga deal inatakia kusimama wenyewe kwa uhalisia na ukweli.
Ni aibu kupiga kelele ya mikopo ya sh milioni 2 kwa mwaka vyuo vikuu,wakati wananchi wazalendo wanalipia shule za msingi milioni 2 hadi 3 kwa mtoto mmoja.
Ifike mahali tutumie vichwa vyetu kufikiri na sio vinginevyo,kelele za chura hazimzui ngo'mbe kunywa maji
Mkuu ni jana tu tumekopeshwa bil 360. Sasa Kama serikali inakopa fedha kidogo hivi halafu inashangilia Kama siyo kufilisika ni nini, Ina maana ni wazi kuwa Bakhresa kwa sasa anazo pesa nyingi kuliko serikali, watuambie tu ukweli, waache kutuzungusha zungusha, hii Nchi ni Mali ya kila Mtanzania.
 
Back
Top Bottom