Kama serikali imefilisika si bora kuwaweka wananchi wazi?

Kikwete alikusanya wastani wa bilion 650 kwa mwezi, aliweza kulipa wafanyakazi hewa wote wanafunzi vilaza wote walipewa mikopo, watu walipiga Dili kama kawaida, lakini pesa ilionekana kwa kila mfuko wa mtu, ilitawanyika kila mahali. Biashara zilishamiri kila kona ya Nchi hii, Barabara zilijengwa kila mahali,

Sasa hivi hakuna wafanyakazi hewa, wanafunzi vilaza wote wamerudi nyumbani, makusanyo wamesema ni mara mbili, sasa tunajiuliza, ziko wapi? Mbona hatuoni lolote?. Kuna tatizo gani huko juu?. Ni uchoyo au ni Roho mbaya, au hakuna kabisa?
 
Unataka watu waache kazi ? Hivi kwa mfano uwaambie polisi kwamba serikali imefilisika si watajazana KK SECURITY , maana 98% hawana ujuzi mwingine .

99% ya polisi wanaujuzi mbalimbali. kazi ya polisi ni fani na baadhi ya kazi zao lazima uwe na ujuzi kama Uasibu, fundi, wanasheria. Wanachojifunza katika upolisi ni namna ya kukukamata na sheria mbali mbali za nchi. Ila bado wapo wazembe wazembe baadaye wanaangukia kwa kilna Malisoka security Guard.
 
Mkuu Asante kwa uzi wako.

Kwa ufupi serikali hii ya awamu ya 5 IMEFILISIKA.
Hili wala sio la kupepesa macho tena..

Serikali imefilisika completely na it's high time ilo lazima walikubali hivi sasa.

Yale ma trilioni ya kila mwezi tunayotangaziwa kila mwezi ni UONGO MTUPU.

Mnaweza vipi kila mwezi kukusanya trilions halafu juzi mnakopa 360Bil from ADB???

Serikali mufilisi hii kwa sasa.
kipofu anaendesha gari la abiria
 
Mkuu kwa hiyo kuna haja ya kujumlisha mapato yote ya TRA yanayotangazwa kila mwezi toka waanze kutangaza ili tupate hesabu kamili, alafu tuje tuangalie matumizi ili tupate balansi.
Ni kweli mkuu, kwa sababu ni pesa zetu za kodi, tunalipa ili zituhudumie, au kwa maana nyingine zirudi kwetu. Sasa Kama hazirudi sisi wananchi tuna haki ya kujua pesa zetu ziko wapi? Kama wamemkopesha mtu mtu watuambie, loh!
 
Warsha Semina, Makongamano, Safari za nje Marufuku. Sasa shusheni basi hizo pesa kwa Raia! Au mnasubiri mpaka wafe?
 
Ukiskia watu wana lala njaa wakat chakul kipo ndio hap sas, Maan kila sku tunaskia tumeokoa sijui billion 3.4 lakin hatujui znaenda wapi.
 
Warsha Semina, Makongamano, Safari za nje Marufuku. Sasa shusheni basi hizo pesa kwa Raia! Au mnasubiri mpaka wafe?
Tunahitaji pesa au maendeleo? Kwani maendeleo ni pesa? Kwani sadaka ni pesa?????
 
Mkuu Asante kwa uzi wako.

Kwa ufupi serikali hii ya awamu ya 5 IMEFILISIKA.
Hili wala sio la kupepesa macho tena..

Serikali imefilisika completely na it's high time ilo lazima walikubali hivi sasa.

Yale ma trilioni ya kila mwezi tunayotangaziwa kila mwezi ni UONGO MTUPU.

Mnaweza vipi kila mwezi kukusanya trilions halafu juzi mnakopa 360Bil from ADB???

Serikali mufilisi hii kwa sasa.

Hivi kuna mradi mkubwa wowote ulioanza mpaka sasa?
 
Hakuna kitu kibaya kua na kiongonzi muhongo muhongo
Mkuu ati Jana wamekopa bilion 360, toka ADB nayo wameona iwe ni taarifa ya habari, wakati ilitakiwa tena iwe ni habari ya Siri na ya aibu. Sasa Kama makusanyo ni 1.25 trillion hiyo 360 bilion inaingia wapi, na huo si ni sawa na mishahara ya wafanyakazi kwa mwezi moja tu?. Inasikitisha sana.
 
Uliishaambiwa hii nchi ni ya watu wawili sasa ww unauliza km nani?
 
Gharama za kukusanya pesa zaweza kuwa kubwa na hivyo kuishia kuwa na maandishi yenye tarakimu kubwa lakini mwisho wa siku kilichopatikana kidogo.
Mikataba mibovu siyo ya madini na gas tu, hata hii midogo midogo ya kukusanya mapato yaweza kukosa ufanisi. (Matatizo makubwa ni matokeo ya yale madogo madogo).
Hivyo TRA hawawezi kukusanya wenyewe bila kutumia madalali? Madalali wanafanya nini cha zaidi ambacho hakiwezi kufanywa na Taasisi za serikali pengine? Tenda sio lazima ziwe za uniform au madawati.
 
Ukiskia watu wana lala njaa wakat chakul kipo ndio hap sas, Maan kila sku tunaskia tumeokoa sijui billion 3.4 lakin hatujui znaenda wapi.
Mshahara unatokaga mapema tarehe 25, njaa inayokaga wapi wijimeni????

Mmeambiwa usafi kama Rwanda, hamufanyagi eti wa TZ wote ni Wasabato. Dodoma hamutakagi kwendaga.
 
Kikwete alikusanya wastani wa bilion 650 kwa mwezi, aliweza kulipa wafanyakazi hewa wote wanafunzi vilaza wote walipewa mikopo, watu walipiga Dili kama kawaida, lakini pesa ilionekana kwa kila mfuko wa mtu, ilitawanyika kila mahali. Biashara zilishamiri kila kona ya Nchi hii, Barabara zilijengwa kila mahali,

Sasa hivi hakuna wafanyakazi hewa, wanafunzi vilaza wote wamerudi nyumbani, makusanyo wamesema ni mara mbili, sasa tunajiuliza, ziko wapi? Mbona hatuoni lolote?. Kuna tatizo gani huko juu?. Ni uchoyo au ni Roho mbaya, au hakuna kabisa?
ukimaliza kujiuliza maswali hayo, jiulize tena jk alikuta deni la taifa ni sh ngapi na ametuacha na deni la sh ngapi, ndo utajua hela yote hiyo aliipata wapi!..
 
ukimaliza kujiuliza maswali hayo, jiulize tena jk alikuta deni la taifa ni sh ngapi na ametuacha na deni la sh ngapi, ndo utajua hela yote hiyo aliipata wapi!..
Lakini si pesa ilionekana kila mahali, mabenki walikuwa wanapita mitaani kutafuta wateja wa kukopesha na wanakubembeleza. Sasa hivi ukiomba mkopo wanakuangalia Kama nyanya mbichi! Duh
 
Lakini si pesa ilionekana kila mahali, mabenki walikuwa wanapita mitaani kutafuta wateja wa kukopesha na wanakubembeleza. Sasa hivi ukiomba mkopo wanakuangalia Kama nyanya mbichi! Duh
Kupanga ni kuchagua mkuu..

kwa hiyo ni bora kuruhusu dili na rushwa, kukopa kwa sana hata mishahara ya wafanyakazi, kufanya semina makongamano, safari za nje, watumishi hewa, ili kusudi hela ipatikane mtaani?? au kupunguza hayo niliyoyasema hapo juu ili tuweze kujiendesha kwa mambo yetu na kukopa pesa kwa miradi mikubwa ya maendeleo??

Magu has choosen the second option.. Swali ni kwako, ungechagua lipi??
 
Back
Top Bottom