field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,730
Wakati viongozi waliopo madarakani walivyokuja kuomba kura wanakuja kwa unyenyekevu, heshima na ahadi nyingi zote zikiwa za kutetea wananchi wanyonge. Wakipata ukubwa wanaanza kuja na "decrees" nyingi za kuwapendelea wao wenyewe na kutoa maneno ya kujionyesha wao ndiyo wao hakuna wengine......Wamesahau walichosema wakati wa kuomba kura.
Kumekuwa na wimbi la kufungia wanamuziki na vyombo vya habari kwa "TRIVIAL reasons", mfano hivi karibuni kufungiwa kwa miziki kwa sababu ambazo zinaelezwa kuwa ni kukiuka utamaduni wa Mtanzania. Sijui utamaduni wa mtanzania upoje maana nimeulizia sikupata jibu hadi leo.
Nimesikiliza mahojiano ya Diamond Platnumz, mwanamuziki huo amejieleza vizuri sana nampa pongezi kwa kueleza mawazo yake, Viongozi wetu wapo hapo kwa ajili ya kuadhibu na si kurekebisha au kuelekeza, wanashindwa kuelewa kuwa muziki ni kazi kama kazi nyingine za ofisini hivyo unavyomfungia msanii kama ROMA unamuondolea ajira (employment) yake....je serikali itamlipia "Welfare"? Au kwa vile inafikiria hiyo ajira inahusu "entertainment" hivyo haifai kuwa ajira rasmi....sasa kama serikali inasema SANAA NI SAWA NA KAZI NYINGINE unavyomsimamisha au unamfungia kazi huyo mfanyakazi (msanii) ataishi vipi yeye na familia yake? Ndiyo maana nasema huo ni uonevu.....Kwenye kazi nyingine tunakosea hata kufanya kazi lakini hatusimamishwi, kufungiwa au kunyimwa mshahara...Kazi zote zina utaratibu mmoja!
Waziri kasema kile kituo cha radio kilichomhoji Diamond kitashughulikiwa..KWANI KOSA LA KITUO CHA RADIO HIYO NI NINI? Nikisema serikali hii inakandamiza uhuru wa habari kuna mtu atabisha?
Kuna utaratibu wa vituo vya TV au Radio kucheza muziki au kuonesha filamu zenye "rating R" kuanzia saa tatu na nusu usiku na kuendelea, hii ni systems ya nchi zote duniani. Watoto wanafanya nini kwenye TV saa nne za usiku? Kuna filamu zenye categories: Universal au PG-13 ambazo hazina tatizo kuangaliwa na watoto chini ya uangalizi wa wazazi......sasa haya mambo ya kusema sijui watoto wanafundishwa utamaduni mbovu unatoka wapi?
Kwanini tuwe kisiwa peke yetu wakati majirani zetu wanafanya yale tunayoyaona kwetu hayafai? UTAMADUNI GANI HUO WA MTANZANIA SERIKALI INAYOONGELEA? au ni jinsi ya kurasimisha ukandamizaji wa watu fulani fulani?
Kwa jinsi hii ningemshauri Diamond ahamie nchi kama Kenya au South Africa....nchi hizo au nchi zingine nyingi zinajali kazi za wasanii wake siyo kwetu ambako serikali inapigana na kila mtu...si wafanyabiashara, wafanyakazi, wasanii, viongozi wa dini, na wanasiasa wa upinzani.
Les Wanyika ilihamia, Simba Wanyika ilihamia Kenya, Super Volcano ilihamia Kenya, Patrick Balisidya alihamia Kenya na wengineo wengi, na kazi zao zilithaminiwa na kuinyanyua Kenya kimuziki, Hivyo Diamond akihamia nchi hizo ataendelea kufanya vizuri kwa sababu ana msingi mzuri na wenzetu wanajali, Tanzania ni nchi isiyo na msimamo!