Kama RC Mnyeti anatuhumiwa kwa rushwa basi Mhe. Mbowe na Kamati Kuu ya CHADEMA nao wana kesi ya kujibu

nakumbuka Lisu na Msigwe walikuwa tayari wameshaazira ikaundwa kamati ya kwenda kuwatukiza kwa 150ml kila mmoja na wao aibu ikawatoka nao wakaanza kuzungusha mikono ila mnyika alitosa na dk silaa akashikilia msimamo wake mpaka mwisho
IMG-20170617-WA0015.jpeg
Hivi kwa MSIMAMO na KAULI hizi hawa MAKAMANDA waliwezaje kumkumbatia huyu mh.? ..... Atakaepata jibu anishirikishe nami pia .... PESA BWANA
 
Umetumia nguvu nyingi kujibu mada "out of hatred" nadhani ungetuliza akili yako ukaweka ushabiki wako wa vyama pembeni walau ungeona mantiki ya nilichoandika.

Kama unalaumu Madiwani kuhongwa basi busara ikutume kwanza kulaumu Chama chako kuchagua wawakilishi wanaohongeka kirahisi namna ile na kusahau wajibu wao kwa wananchi waliowachagua. Kwahiyo kama ni kweli walihongwa, basi tatizo linaanzia ndani ya Chama siyo nje ya Chama. Ni vyema chama chako kikajitatmini inawezekana huu ni utamaduni uliofichika ndani ya chama. Ndo maana kila anaehama chama chenu, mnakimbilia kusema amehongwa lakini anaeingia anaonekana eti amejitambua. So kwa maneno mengine naweza kusema ndani ya CDM hakuna utaratibu wa watu kujiamulia mambo yao wenyewe (Demokrasia) ukienda tofauti na matakwa ya viongozi utaitwa msaliti au umehongwa.

Matatizo ya wananchi uliyoyaelezea yapo mpaka kwenye majimbo na halmashauri zinazoongozwa na Chama chako. Ssa sijui wajibu wa kuwaletea maendeleo wananchi ni la Serikali peke yake au ni la kila Chama/ Kiongozi kulingana na nafasi aliyonayo katika Jamii. Nijuavyo mmi matatizo hayawezi kuisha madhali watu wanazaliwa kila siku basi ni lazima changamoto nazo ziwepo. Cha msingi ni kulinganisha tulipotoka na wapi tulipo sasa ili kujua mafanikio gani tuliyofikia kama taifa na changamoto zipi bado zinatukabili.

Umezungumzia fedha zitakazotumika kati chaguzi za marudio, Kaka nadhani huelewi kwamba DEMOKRASIA NI GHARAMA. Ingewezekana kabisa kusifanyike chaguzi za marudio katika hizo kata na nchi ingeendelea kama kawaida. Lakini madhali umewekwa mfumo wa kidemokrasia wa kujitawala ni dhahiri Serikali inaoheshimu hilo itazingatia matakwa ya wananchi kujichagulia viongozi wao bila kujali sababu iliyopelekea hivyo.

Kuhusu kulinganisha suala la lowasa na Madiwani waliojiuzulu, nadhani hukuelewa nilichokihoji. Kwanza utaratibu uliotumika kumshawishi lowassa ni sawa kabisa na ushahidi unaotumiwa na kina Nassari kumtuhumu Mnyeti. Hebu tuone ulinganifu huu;

1. Kulikua na maongezi kabla ya lowasa kuhama CCM na vile vile ushahidi wa Nassari unaonyesha pia kulikua na maongezi kabla Madiwani kuhama.

2. Wote walipewa ahadi. Isipokua mmoja aliahidiwa Uongozi na wengie waliahidiwa fedha. Fedha ni za Umma lakini dhamana ya Uongozi pia ni ya Umma.

Sasa nachouliza kama utaratibu uliotumika kumshawaishi Lowassa ni halali kwanini utaratibu uliotumika kwa Madiwani unaonekana siyo halali wakati kila kitu ni kile kile?

Naomba nisipuuzwe jamani.



Sent from my VFD 300 using JamiiForums mobile app
Kiongozi unaeleweka vizuri sana .... hongera kwa kuileta hii HOJA FIKILISHI
 
Jipange! Alichokifanya mnyeti ni rushwa isiokuwa na DOA! Kiongozi wa ccm kahamua kuibariki usituletee mada za "paukwa pakawa"!
 
Nikweli kabisa muosha huoshwa ndivyo ninavyoamini na ndivyo wahenga wanavyoamini

Awali ya yote naomba niwakumbushe jambo wanachadema kwa upendo na unyenyekevu mwingi kuwa hapo awali kuku hakuwa na tabia ya kunya ndani ila Siku moja Jogoo alibanwa kwakua yy ndo baba tena mkuu wa kaya akaona hamna tatizo akanya, Mtetea akaona na akatafakari akajua pengine utamaduni umebadilika hivyo na yy alipobanwa akanya, kifaranga naye akatafakari kama baba (Jogoo) kanya, mama(Mtetea) kanya basi kifaranga nacho kikanya, mpaka Leo kuku maisha yake ni kunya ndani

Hitimisho
Hanna haja ya kulaumiana kila mmoja aendelee kulenga target kwa wakati wake ilimladi kupata unachokitaka c unachokipata
 
kwa maana hiyo... kwa tafsiri yako rushwa ni ile inayotolewa kwa kutumia fedha ya umma. ila ukitumia fedha nyingine kutoa rushwa haiesabiki kma ni rushwa. sijui unauona huu ujinga ulioandika. inabidi uombeww
Kumbe unajua rushwa ni rushwa tu bila kujali ni taslimali au fedha za umma au binafsi? Kama tafsiri yako ni hiyo, ni kitu gani kilimsukuma mteuaji kumyeua mtu anayetuhumiwa kuhonga ilihali shauri hili lipo mbele ya mamlaka ya kisheria ikichunguza?
Niwaambie tu wanalumumba kuwa tuhuma pekee yatosha kupima uadilifu wa mtu na ukitaka kutengwa na jamii, walinde watuhumiwa!
Kwa akili yako unafikiri takukuru wataendelea na kumchunguza mteule? Yanajirudia yaleyale ya takukuru ya Kikwete iliyokuwa inafunika mambo siku iende!
 
Kuna mambo, ukimya unatosha kukuonyesha ulivyo mwerevu. Mwezetu kwakuwa ni kada wa CCM, unaweza kuandika chochote. Wengine hata tukijadili tu, tutaitwa wachochezi. Busara zinanituma kutoandika chochote katika kujadili jambo lako. Tuache tuendelee kufanya tafakuri kwa yote yaliyotokea na yanayoendelea kutokea.
Huwezi kumshtaki mkeo kwa kukuzalia mtoto. In kweli anashutuma ya rushwa, ila alipewa maagizo na mungu MTU wao anayewateua na kumfanya aende chooni.
 
"NAMI PIA NASIMAMA TENA KAMA MGOMBEA URAIS MWAKA 2020 KUPITIA CHADEMA" hiyo kauli ya Mh. saaaaana RAIS WA MIOYO YA WATU aloitoa kule kwa jirani zetu KENYA aliwezaje kuitoa kama HANA NGUVU YA USHAWISHI (pesa) NDANI YA CDM?
Jambo la ajabu MAKAMANDA WOOOOOOOTE KIMYA hata mmoja hajasikika akihoji juu ya hiyo kauli ya RAIS WA MIOYO YA WATU

Kwa hiyo kumbe una - "assume" tu, siyo? Kwa sbb ya maneno, then unageuza kuwa rushwa, au siyo?
 
Wasalaam Wana Jamii,

Nimefuatilia mijadala mingi kwenye hii forum na kuona watu wengi wakilaumu juu ya Uteuzi wa Mhe. Mnyeti kuwa RC - Manyara kwasababu eti anatuhumiwa (haijathibitika) kutoa rushwa kwa madiwani wa CDM ili wakihame chao na hivyo hakustahili kuteuliwa.Dhana hii imejengwa juu ya ushahidi uliowasilishwa TAKUKURU na Mhe. Nassari.

Baada ya kutafakari kwa kina, nimeona kimsingi walichofanya kina nassari dhidi ya mnyeti ni siasa na lengo lilikua ni kurudisha imani ya wananchi kwa chama chao ionekane madiwani hawakuhama kwa hiari yao au kwasababu walizotoa bali ni kwa kununuliwa/tamaa ya fedha. Well, hata kama ilifanyika hivyo nijuavyo mimi siasa ni maslahi (cheo, fedha n.k) hakuna mwanasiasa (hasa walio kwenye uongozi au wenye ushawishi mkubwa katika jamii) ambae ameshawahi kuhama chama chake kwenda kingine bila kufuata maslahi niliyoyataja na kabla ya kuhama ni lazima mazungumzo yafanyike kwenye chama anachohamia ili kujihakikishia kwamba maslahi yake yanazingatiwa.

Kuthibitisha haya, nitolee mfano kwa kujikumbusha wakati Bw.Lowassa anahamia CDM kutoka CCM. Kabla ya kuhama, yalifanyika mazungumzo ambayo mengine yalikua ya siri na mengine yalifanyika wazi ingawa hayakua public (yale yaliyofanyika bahari beach) lengo la mazungumzo yale pamoja na mambo mengine ilikua ni kumhakikishia Bw. Lowassa kwamba atakapohamia CDM basi atapewa nafasi ya kuwa mgombea urais na ikawa hivyo, japokua CDM ilikua tayari imeshakamilisha mchakato wa kumchagua mgombea urais wake na ilikua imebakia kuafikiana na UKAWA na kisha kumtangaza (rejea maelezo ya Dk.Slaa wakati anang'atuka CDM na ujio wa Lowassa).

Sasa tunapozungumzia rushwa kwa tafsiri isiyo rasmi ni kitu chochote mtu anachotoa kwa lengo la kupata kitu fulani kwa njia isiyo halali. Sasa swali la kujiuliza hapa ni ipi 'njia isiyo halali' hususan kwenye siasa. Je, kumpa ahadi mwanasiasa kwa kuzingatia maslahi yake ya kisiasa (fedha, cheo n.k) ili ahamie kwenye chama chako ni njia isiyo halali? kama tunakubaliana kwamba njia hii siyo halali basi tukubaliane pia kwamba hata Lowassa alihamia CDM kwa njia isiyo halali kwasababu alihama kwa lengo la kupata cheo/ nafasi ya kugombea u Rais aliyoahidiwa (vinginevyo asingehama). halikadhalika, kama tunaamini kwamba DC Mnyeti (sasa RC) kitendo chake cha kufanya mazungumzo na madiwani waliohama CDM na kutoa ahadi ili wahame chama chao ni kosa ambalo linahusiana na rushwa basi hata Kamati Kuu ya CDM, Mhe.Mbowe na washirika wao waliofanikisha lowassa kuhama CCM basi inabidi na wao washitakiwe kwa kosa hilo hilo la rushwa ya kumshawishi Lowassa ahamie kwenye chama chao ili apewe nafasi ya kugombea rais. Otherwise, kama tunasema njia iliyotumika kumshawishi Lowassa kuhamia CDM ilikua halali basi tuseme pia njia iliyotumika kuwashawishi madiwani ni halali.

Hivyo, Mhe. Mnyeti hakufanya kosa lolote na wala hatupaswi kuwashurutisha TAKUKURU kuchukua hatua dhidi yake kwa sababu ile haikua RUSHWA bali ni USHAWISHI uliozingatia maslahi ya kisiasa. Na kwa maana hiyo Mhe.Rais hakukosea kumteua kada mtiifu aliefanya kazi yake kwa uadilifu na werevu Mhe. Alexander Mnyeti kuwa RC mpya - Mkoa Manyara.

Naomba kuwasilisha.
Hakuna kosa linalo halalisha kosa jingine. Unataka kusema tume ya uchaguzi ni mbumbu?
 
Back
Top Bottom