Kama Rais ni mtetezi wa wanyonge na mtumbuaji majipu maarufu, kwanini hajamtumbua Said Lugumi?

Oct 7, 2015
86
108
Baada ya kuwasilishwa Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ndani ya Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, ilitakiwa kuwasilishwa Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ikitakiwa kuwasilishwa na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara hiyo, Mhe. Godbless Jonathan Lema (MB) Kuhusu makadirio ya Mapato na matumizi ya fedha ya Wizara hiyo.

Katika hali isiyo ya kawaida Hotuba hiyo ya Kambi Rasmi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyokuwa iwasilishwe leo Jumatatu 16/5/2016 Bungeni mjini Dodoma iliahirishwa kwa kile kilichosemekana Hotuba hiyo inatakiwa ikapitiwe upya na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Katika hali ya kawaida, inaonyesha kuna mam bo ambayo wasingependa viwemo kwenye Hotuba hiyo hili hali mambo hayo yana tija kwa mustakabali wa Taifa letu.

Hapo ndipo unapogundua ya kuwa Serikali hii ya awamu ya 5 imejawa hofu na inataka kuficha madhambi mengi huku ikiwaadaa wananchi na mambo mbalimbali kama wanavyoita utumbuaji majipu, huku majipu ambayo ni hatari zaidi yakiendelea kuachwa na kutakwa kufichwa na kuumiza Taifa.

Serikali ya awamu 5 imeshaonyesha viashiria vya wazi wazi ya kuwa ni Serikali yenye hofu na ya Kidikteta na isiyopenda kukoselewa katika hali yeyote mfano, kukataza kuonyeshwa moja kwa moja kwa vikao vya Bunge ili waweze kuficha mambo yao machafu, kuchukua mambo ya msingi ambayo wananchi wangependa kuyajua na kuwapa uelewa na kujua ni kipi wawakilishi wao wanakifanya ndani ya Bunge, hali yao ya Kikatiba imeminywa wazi wazi(In a daylight).

Sheria kandamizi kwa vyombo vya habari, kufungia vyombo mbalimbali vya habari, hivi ni viashiria tosha ya kuwa Serikali hii haitaki kukosolewa na kutaka kuendesha nchi inavyotaka huku Katiba, Sheria,Taratibu mbalimbali za nchi.

Katika hili la kutowasilishwa kwa Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inaonekana kuna mkono mrefu wa Rais mstaafu wa awamu ya 4 Mhe. Jakaya Kikwete akizuia na kutaka hotuba hiyo is iwasilishwe Bungeni kwani inamgusa kwa hali moja ama nyingine, Hotuba hiyo imetakiwa kupitia na na Kamati ya Maadili ya Bunge ili waweze kuondoa mambo mambo mbalimbali ambayo wasingependa yawasilishwe mbele ya Bunge letu tukufu la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, katika Hotuba hiyo anaingizwa IGP Mstaafu Saidi Mwema ambaye ni ndugu yake.

Said Mwema ndiye aliyekuwa IGP na kuingia mikataba na Lugumi Enterprises ambaye amemuoa mtoto wa Said Mwema IGP huyo mstaafu.

Kikubwa ambacho kinatakiwa kufichwa kuacha mengine mengi ni Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliyohoji utekelezaji wa mkataba wenye utata wa vifaa vya mfumo wa alama za vidole (AFIS) ulioingiwa Kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

Kuna malumbano yaliyojaa sintofahamu na inatakiwa sintofahamu hii imalizike bila shaka, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka Serikali kutoa majibu kwa maswali yafuatayo:

1. Kwa kuwa mikataba ya Serikali kwa mujibu wa Sheria lazima ufuate Sheria za manunuzi na kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),Je utaratibu huu ulifuatwa?

Kingine cha muhimu kujua ni kwamba, Je Mkataba wa Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi umetekelezwa ama haukutekelezwa na kama ulitekelezwa ni kwa kiwango gani, na ikiwa kulikuwa na tatizo la utekelezaji, Jeshi la Polisi lilichukua hatua zipi?

Yote kwa yote, swali la msingi, Kampuni ngapi ambazo zinahusika na hatua za utekelezaji wa Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, kwa kuwa Kampuni ya INFOSYS inatajwa kufunga vifaa hivyo (AFIS), kwanini C.A.G katika ukaguzi alioufanya hakuhoji suala la uhalali na kulinganisha thamani ya pesa ya manunuzi na faida ya vifaa vile?

Akiwa ni Rais mtetezi wa wawanyonge kama anavyojinadi na mtumbuaji majibu maarufu, kwanini hajatumbua jipu la Said Lugumi na aliyekuwa IGP Said Mwema na Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kuwasimamisha kazi wote wanaondelea na kazi lakini kwa hali moja au nyingine wamehusika na mkataba tata wa Lugumi?
 
Na mimi nimeshangazwa sana na hiki kilichotokea bungeni leo, wamezuia bunge lisirushwe live haitoshi sasa wanataka waanze kuedit na hotuba za Kambi rasmi ya upinzani
 
Hapo kuna watu wazito wanalindana! JPM hapo ndio anaona kweli kazi itaelekea kumshinda!! Kama akiweza kutumia usemi w Baba Askofu aliompa basi nchi haitamshinda!! Bora mmoja afe kwa manufaa ya nchi....ili nchi isonge mbele!!
 
Suala LA mfumo wa vidole so kiki tena kwa upinzani hapo hollaa.....maana kila kituo kina hizo mashineeeee

Ccm oyeeeeeeeee
 
Muacheni JK basis,malizaneni na Pombe.
Kama Escrow ilijadiliwa kipindi cha JK,yeye ni nani hadi azuie Bunge?

Deal na Ndugai na Pombe.
Jk hana cha kupoteza wala kuchomoa kwani hajachomeka kitu!!
 
Masikini Tanzania,
serikali iliyoamininika hapo awali leo imegeuka na kuwa waficha maovu na watetezi wa Mafisadi.

Mkataba wa Lugumi ni mtarimbo ulioiganda serikali ya CCM.
 
Kambi Rasmi ya upinzani si itupatie hiyo soft copy tu
Kama ni msomaji magazeti yaliyomo kwenye hiyo hotuba ni mambo ya magazetini hamna jipya hata moja.NAKUAPIA.Alichofanya ni kukusanya habari za magazetini na kuziandikia hotuba!!! AIbu kuiita ile eti ni hotuba ya upinzani bungeni ni aibu.
 
Sasa hiv ukijal utaifa sijui uzalendo sijui yan unapoteza muda wako tuu kwasabab utakuwa unawatumikia na kuwaaneemesha mafisad wachache tu. Bora ujal maendeleo yako binafs na familia
 
walizoea kumkaba jk mpaka penalt,magufuli atawanyorosha
yan mnaujasir wa kusifia upuuz? Hamuon taifa linavyodidimia? Ama iyo juis nzito ya maembe na kuku wa kukaanga hapo lumumba zimewapofusha.

You guys come on
 
Kumbe hii nchi ina matabula laza wengi hivi?wengine uwaita ignoransia class kwa lugh ili ile,hata ukiwaita Lumpen proletariat kwa lugha ya marxism unakuwa hujakosea sana,nashangazwa na mtu anayeshangilia TOTARITARIANISM
 
Suala LA mfumo wa vidole so kiki tena kwa upinzani hapo hollaa.....maana kila kituo kina hizo mashineeeee

Ccm oyeeeeeeeee
You must see a psychiatrist kwani una shida kkubwa upstairs. Uliambiwa ni vitu 14 tu na 10 hazifanyi kazi. Wakati mwingine acheni kujipendekeza hadi kwa shetani kulikopitiliza. Tangulizeni utaifa kwanza na siyo matumbo yenu.
 
Masikini Tanzania,
serikali iliyoamininika hapo awali leo imegeuka na kuwa waficha maovu na watetezi wa Mafisadi.

Mkataba wa Lugumi ni mtarimbo ulioiganda serikali ya CCM.
CCM ndiyo chama dume,na Magufuri ndiye rais wa Tanzania.Ndugai ni mbunge wa Kongwa na ni mwana CCM na ndiye spika wa Bunge la Tanzania a.k.a bosi wa Mbowe,Lema,Lissu na Miungu wako wote waliopo Bungeni unaowafahamu ww.Km hutaki,fanya hayo yanaweza kukusaidia-ama jinyonge,hama nchi,jitupe bahari na mengine mengi fanani na hayo.Na yakupasa utambuye,CCM ndiyo chama TAWALA hadi mwisho wa kinyongo chako.
 
Back
Top Bottom