Kama Rais hajui uwepo wa baadhi ya sheria, AG na Waziri Mwakyembe wajiuzulu. Haki zetu zi mashakani

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,903
4,051
Mh Rais amesema hakujua kama alitakiwa kuchagua kamishna wa mamlaka ya dawa za kulevya,na hata hakuletewa mapendekezo ya majina ya watu wa kuteuliwa!.

Mh amesema hata waziri mkuu hakujua kama yeye ni mwenyekiti wa baraza la kudhihiti dawa za kulevya na hata mawaziri waliotajwa na sheria walikuwa hawajui kama nao ni wajumbe,na kama wamejua basi wamejua jana!.

Siku zote naamini sana katika kutoa maoni yanayoonesha udhaifu wa kampeni hii,tulipiga kelele sana kutaka baraza na mamlaka zifanye kazi kwa mujibu wa sheria,baadhi hawakutuelewa wakadhani tunaipinga kampeni hii!.

Tulihoji inakuaje tunaanza vita hivi bila mamlaka,tunapambanaje huku baraza lipo kimya?tukashauri uwajibikaji wa pamoja ni muhimu katika vita hii,kinyume na hapo hatutafanikiwa!.

Leo nimemsikia Rais akivitaka vyombo vyote vya kimamlaka sasa kuwa active!,

My take!.
Mh Rais kaa na wasaidizi wako,wape semina wajue mamlaka yao kisheria ili wakusaidie kufikia malengo uliyojiwekea!.
By Doto Bulendu
 
Inashangaza nchi hii ina mwanasheria mkuu wa serikali halafu mkuu anakiri hajui uwepo wa baadhi ya sheria.

Katika hali hii haki za mwananchi ziko salama? Au ndio kutangazana majukwaani na kutumbuana? Je kuna briefing ya kisheria kabla ya kufanya jambo?

Mwanasheria ofisi ya mkuu wa mkoa ana kazi gani? Ndio alishauri watu wadhalilishwe?

Naona hatari mbele!!!
Ndio maana kila kukicha huyu kakamatwa,yule kafunguliwa kesi,huyu kanyimwa dhamana,kumbe kuna watu hawajui uwapo wa baadhi ya sheria!!

Hivi hatuna wazee wa kutoa tahadhari?
 
Hapa tatzo kubwa ni kuwepo kwa MBOWE kwenye hii LIST....

ASINGETAJWA mbowe KWENYE HII list STORY ZINGEKUWA NI NYINGNE KABSA.....nADHANI TUNGESIKIA yafuatayo....
...mbna wamepewa dhamana...
...mbna hawapelekwi mahakamani...
...Mbna hawajatatwa wote......wametajwa vidagaa
Yaani stor ingekuwa tofauti kabsa.......

Mchawi mkubwa wa kupambana na MADAWA YA KULEVYA NCHII HII NI CDM......hata baadhi ya wabunge wa CCM wamesafiria nyota ya CDM kwenye haya mapambano kutokana na mslahi yao binafsi na chuki walio nayo juu ya MAKONDA......
 
Du kuna watu hawajawajibika hapa na lazima wawajibishwe.hata dokezo la kumshauri kwenye uteuzi hajapelekewa na PM kama kujua kajua jana au juzi inamaana wanasheria wao wamelala.
 
Ni kweli maana kwa akili zako nusu anaejua SHERIA kwenye hii nchi ni LISSU tu.......
Umepewa wasaidizi lukuki halafu unaibuka unasema "nilikuwa sijui"

There is no excuse inapokuja kwenye mambo ya public office
 
Miaka nane Lissu na bendi yake wamezunguka nchi nzima wakiita watu ni mafisadi na watu hapa Jf wakawa wanashangilia. Lakini leo katajwa Mwenyekiti yule Lissu anakuja na single ya sheria! Kuna nini? Na watu wanaopiga kelele kuhusu wanaotajwa kinawahusu nini au wanaogopa watakifiwa?
 
Utawala umekuwa kama wa mateja yaani unaloamka nalo asubuhi ndio hilo hilo.
 
Kujiuzulu si jambo jepesi mkuu..Ila bwana yule nadhani hayuko sawa kichwani..Nahisi atakuwa amempigia simu Maconder akamwambia aendelee...
 
Miaka nane Lissu na bendi yake wamezunguka nchi nzima wakiita watu ni mafisadi na watu hapa Jf wakawa wanashangilia. Lakini leo katajwa Mwenyekiti yule Lissu anakuja na single ya sheria! Kuna nini? Na watu wanaopiga kelele kuhusu wanaotajwa kinawahusu nini au wanaogopa watakifiwa?
Jitekenye tu!!
 
Kujiuzulu si jambo jepesi mkuu..Ila bwana yule nadhani hayuko sawa kichwani..Nahisi atakuwa amempigia simu Maconder akamwambia aendelee...
Hatari sana......maagizo mengi yanatolewa na watu wasiijua kwamba kuna sheria fulani! Maagizo hayo yanaenda kudhuru raia wa nchi hii wanateseka .

Ona Gwajima,kalazwa sero siku tatu,Manji mpaka leo, wasanii,wabunge wanahangaishwa na watu ambao kumbe hata hawajui uwapo wa sheria Fulani,aibu kubwa hii
 
Hapa tatzo kubwa ni kuwepo kwa MBOWE kwenye hii LIST....

ASINGETAJWA mbowe KWENYE HII list STORY ZINGEKUWA NI NYINGNE KABSA.....nADHANI TUNGESIKIA yafuatayo....
...mbna wamepewa dhamana...
...mbna hawapelekwi mahakamani...
...Mbna hawajatatwa wote......wametajwa vidagaa
Yaani stor ingekuwa tofauti kabsa.......

Mchawi mkubwa wa kupambana na MADAWA YA KULEVYA NCHII HII NI CDM......hata baadhi ya wabunge wa CCM wamesafiria nyota ya CDM kwenye haya mapambano kutokana na mslahi yao binafsi na chuki walio nayo juu ya MAKONDA......
Asanteeeeeeee umenena
 
Miaka nane Lissu na bendi yake wamezunguka nchi nzima wakiita watu ni mafisadi na watu hapa Jf wakawa wanashangilia. Lakini leo katajwa Mwenyekiti yule Lissu anakuja na single ya sheria! Kuna nini? Na watu wanaopiga kelele kuhusu wanaotajwa kinawahusu nini au wanaogopa watakifiwa?
Ndicho mlichobakiza siku hizi. Hamna hoja..
 
Back
Top Bottom