Kama Ningekuwa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Ningekuwa JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TANURU, Jan 25, 2010.

 1. T

  TANURU Senior Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,


  Kama ningekuwa JK pamoja na mambo mengine ningefanya yafuatayo:


  1. Ningejenga Multi-purpose Science Laboratories kila wilaya.


  2. Ningeongea na vituo vyote vya televisheni hapa nchini ili kila siku kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 6 usiku, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na ofisi ya waziri Mkuu, wawe na vipindi vya elimu tu vikilenga zaidi wanafunzi wetu katika ngazi mbalimbali za elimu na Watanzania kwa ujumla wetu kwa ajili ya kutupatia ujuzi katika stadi mbalimbali za maisha.


  3. Ningehakikisha kila mwajeshi hapa nchini anakuwa mtaalam mzuri sana wa ICT na Computer kabla ya mwisho wa mwaka 2015.


  4. Ningelikabidhi rasmi jeshi letu kazi ya kuhakikisha kuwa barabara zetu zote zinapitika mwaka mzima.


  5. Ningefunga VIDEO CONFERENCING FACILITIES katika kila wilaya na tarafa hapa nchini kabla ya mwisho wa mwaka 2013.


  6. Ningejenga National Science Retreat and Research Centre pale Butiama kwa angalau gharama ya shilingi bilioni 20.


  7. Ningeibadilisha Pemba na kuifanya kuwa kitovu za maendeleo ya ICT hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla ndani ya miaka mitano. Hapa ningeanza na Pemba ICT University.


  8. Ningewashawishi viongozi wa Afrika Mashariki kuanzisha kwa pamoja shule za Sayansi za Afrika Mashariki lengo likiwa ni kujenga angalau shule 50 za namna hiyo kila mwaka kwa mgawanyo wa shule 10 kila mwaka kwa kila nchi.


  9. Ningependekeza ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma kujengwe EAST AFRICA PhD CENTRE na pia kuanzisha EAST AFRICA PHD SCHOLARSHIP FUND ikiwa na uwezo wa kufadhili angalau Wana Afrika Mashariki wasiopungua 5000 kwa wakati mmoja. Asilimia angalau 70 iwe kwa ajili ya PhD za Sayansi na Teknolojia.


  10. Ningefuta ada na michango mingine yote kwa shule za sekondari za Serikali hapa nchini.


  11. Ningekopa toka mifuko yetu ya hifadhi ya jamii angalau shilingi bilioni 200 kila mwaka na kujenga High Schools za kisasa angalau 200 kila mwaka na nyingi zikiwa kwa ajili ya combinations za PCM na PCB.

  Nawasilisha.
   
 2. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  East African PhD Research centre ijengwe Dodoma? haahahha
   
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Mawazo yako ni mazuri ila naona kama si practical.
  Ni ndoto nzuri lakini.
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mawazoo mazuri ila nashangaa hata washauri wa JK hawawazii kama wewe...kwa nini????????
   
 5. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  mawazo mazuri lakini si paractical.
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  You must be kidding!
   
 7. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Life is not that easy.....hata wana-mtandao walikuwa na ndoto nyingi kupita hizo
   
 8. GY

  GY JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  You would best fit as a minister for eductaion, science and technology sio president
   
 9. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu,

  Tulijaribu mambo yanayofanana na haya wakati wa Mwalimu, matokeo yanaeleweka.
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mawazo yako mazuri lakini problem wahusika sasa wako bize na uchaguzi hawatakusikiliza mheshimiwa Mkulu mtarajiwa uchaguzi ukiisha watakuwa bize kulipa fadhila na kumalizia vijumba vyao.
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ndiyo maana you are not JK, you think too much!!!!!!
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,912
  Trophy Points: 280
  Ndani ya system hii kama ungekuwa JK na mawazo hayo hapo juu unadhani ungefikia hapo JK "really" alipo?Some stuff dont go hand to hand,too cold to hold and too hot to handle....
  Kasome signature ya Josh Michael you'll then c where im coming from.
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani kama unampigia mbuzi gitaa vile kwa serikali yetu na aka kauchaguzi sana sana watatumia hayo kama gea ya kuchota kura kwa wananchi wakishapata nduki
   
 14. T

  TANURU Senior Member

  #14
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Ni ngumu. Lakini bila mawazo mazito ya namna hiyo na mengineyo na utekelezaji wa dhati hakuna njia ya kutoka hapa tulipo. Sana sana tutakuwa tukisubiri miujiza ambayo bahati mbaya sana haitakaa itokee.

  Nyongeza nyingine ni kuhakikisha SHAMBA DARASA linakuwepo katika kila kijiji.
   
 15. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mawazo mazuri hila kama kawaida yetu Serikali kuu haina bajeti ya kutosha katika Elimu. Kwa kifupi pesa ya kufanya mambo kama hayo hakuna, na itachukua miaka mingi kuwepo, kuna pesa za siasa tu inayosaidia kuwapata viongozi wetu.
   
 16. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ndio maana huwezi kuwa JK, wala kuwa na cheo cha JK.
   
 17. C

  Chief JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Ninngebwaga manyanga na kutugombea awamu ya pili.
   
 18. T

  TANURU Senior Member

  #18
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nono,

  Asante kwa changamoto zako. Naomba niseme kuwa hayo yote niliyoyapendekeza yanawezekana bila tatizo. Tatizo letu kubwa ni rushwa, ufisadi na vipaumbele visivyo sahihi katika matumizi yetu kama taifa.

  Chambua vizuri bajeti za wizara zetu na ofisi ya PM na ile ya Rais utanielewa ninachosema.

  Bajeti ya ofisi ya PM kwa mwaka huu wa fedha ni shilingi trillion 2.63. Naomba nikwambie kuwa unaweza kupunguza shilingi bilioni 394.5 (15%) toka katika bajeti ya PMO na kuwekeza kwenye maeneo niliyoyapendeza bila kuathiri ufanisi katika ofisi ya Waziri Mkuu.

  Hivi ni lini Serikali yetu imekuja na mikakati thabiti ya kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali? ILI FEDHA ZITAKAZO OKOLEWA TUZIWEKEZE KWA UFANISI KATIKA KILIMO, MAJI, NISHATI, ELIMU, NA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

  Nasikitika kuwa safari yetu bado ni ndefu sana.
   
 19. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni vyema Tanuru,
  Lakini pale unapoanza kuweka mikakati na malengo siku zote unaanza kwa kufanya tathmini ya kina kuwa nini kilichotufanya tukawa hapa tulipo, na nini kifanyike ili tuweze kutoka. Vinginezo hizo ulizoeleza awali zitaishia kuwa ngonjera kama zile JK alizoimba za "maisha bora kwa kila mtanzania" bila kusema kuwa atafanya nini ili yawe bora. Mwisho wake baada ya kupata nafasi huo msamiati wa maisha bora hautaki tena.
   
 20. T

  TANURU Senior Member

  #20
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nono,

  Ni kweli. Kwa mwendo tulionao labda miujiza ndiyo itatutoa hapa tulipo.
   
Loading...