Kama nimejenga nyumba kwenye kiwanja si changu, kunivunjia nyumba au kuniambia ninunue hicho kiwanja kipi bora?

Wakati mwingine busara huwa inaitajika unapotoa maamzi. mediation inaweza kutumika .kwani kuna faida gani unapovunja nyumba ya mtu hata kama kiwanja si chake?

Wewe mwambie kiwanja si chake then akikubari mwambia nunua kiwanja hiki.ziko taasisi zenye kuthaminisha viwanja na majumba, Hivyo mhusika au mtuhumiwa ataweza kununua kiwanja hicho au nyumba hiyo kwa thamani halali iliyopangwa na wathaminishaji.unabomoa ghorofa ya mabilioni ili upate faida gani?

Kwanza Serikali inakosa mapato kupitia ubomoaji huo kwa sababu let us say ni nyumba ya kibiashara pale watu walikuwa wanaingiza hela na serikali inapata kodi sasa nyumba umevunja hapo serikali inapata nini?
Ukibomolew ni kwasababu ulimuon mwenye kiwanja unamuweza ,atakufanya nini,ashitaki popote ,kiufupi anaye bomolewa ni kiburi jeuri apambane na hali yake.
 
Kiwanja hakitegemei watu wa tahmini mtu akiamua kuuza ni yeye kuamua bei yake ambayo huangalia vitu vingi mfano wako watu wako tayari kununua kwa bei ambayo ni juu mara mia kuliko tathimini

Huwezi lazimisha mtu akuuzie kwa bei ya watathimini wako.

Akiona hailipi anakwambia toa jengo lako niachie kiwanja changu sitaki kukuuzia after all umenisumbua sana wewe.Ondoa takataka yako hapo Acha uwanja wangu wazi
na wakiruhusu tu busara ya kumuuzia mvamizi kwa bei ya soko ndio itafungulia mlango wa uvamizi wa viwanja vya watu kwa makusudi kabisa.dawa ni kukubaliana na bei ya mwenye kiwanja au ubebe mzigo wako uhamishie kwenye kiwanja chako halali.
 
Wakati mwingine busara huwa inaitajika unapotoa maamzi. mediation inaweza kutumika .kwani kuna faida gani unapovunja nyumba ya mtu hata kama kiwanja si chake?

Wewe mwambie kiwanja si chake then akikubari mwambia nunua kiwanja hiki.ziko taasisi zenye kuthaminisha viwanja na majumba, Hivyo mhusika au mtuhumiwa ataweza kununua kiwanja hicho au nyumba hiyo kwa thamani halali iliyopangwa na wathaminishaji.unabomoa ghorofa ya mabilioni ili upate faida gani?

Kwanza Serikali inakosa mapato kupitia ubomoaji huo kwa sababu let us say ni nyumba ya kibiashara pale watu walikuwa wanaingiza hela na serikali inapata kodi sasa nyumba umevunja hapo serikali inapata nini?
Hiyo itaendeleza uporaji
 
Nilivyosikia, mpaka greda linakuja kubomoa nyumba ya mvamizi ina maana mvamiwaji kashinda kesi. Greda haliji kwa kushtukiza.

Nakuuliza mleta mada, anayetakiwa kuanzisha usuluhishi wa kuuziana ni mvamizi au aliyevamiwa?

Ukisema mamlaka za serikali ndio ziwe zinaongoza usuluhishi wa kuuziana basi itazalisha wavamizi wa makusudi kwa kujua watasaidiwa na mamlaka ili wauziwe.

Kwa uzoefu tu, wavamizi wa bahati mbaya huwa ni wapole na ndio huanzisha majadiliano ya kuuziwa na mara nyingi hufanikiwa.

Wavamizi wa makusudi a.k.a matapeli wao ni watata na hufikishana mbali hadi katika mamlaka za sheria na wakati mwingine huchukua miaka kadhaaa kesi kuisha. Je, aliyevamiwa akishinda kesi atachelewa kupeleka greda?
 
Yaani hawana huruma hata na Jaji jamani mashetani hao.

Mahakama ziwakomalie hawa matapeli wa viwanja hata wao majaji waweza dhulumiwa pia hawaogopi hata majaji hao sio watu wema hao

Inabidi kila kona na kila mhimili uwavallie njuga hadi kieleweke watu waogope kupora viwanja vya watu
Kama mi tapeli langu la viwanja nimesha likabidhi kwa team Jinai ili liwajibishwe kwa mujibu wa sheria, na nina imani kubwa DPP nae atafanya kazi yake nzuri huko Mahakamani baada ya office ya DCI kukamilisha upelelezi wao!!
 
Swali zuri zaidi kwanini ujenge bila kufuata proper procedures ? Mara nyingine mpaka kuvunja ni kwamba ujenzi ule pale haufai, unaweza nyumba kwenye mkondo wa maji labda unasababisha mafuriko n.k. Hivyo kwa kufuata utaratibu unaepusha mambo kama haya Hata kama mambo yanaelezeka mtu mwenye kiwanja atatumia opportunity ya kwamba umeshajenga utamlipa fidia kubwa..., kama ulipenda kiwanja chake mfike kabla ya kuanza ujenzi (utakipata kwa bei nafuu zaidi)
 
Yaani unifuate nyumbani kwangu uniporomoshee mitusi mizito mbele ya familia yangu, watu wakusihi usifanye hivyo ndio unazidi kuyavurumisha huku nimekaa kimya. Siku ya siku yamekukwama unakuja kuomba suluhu unategemea nitataka suluhu na wewe?
 
Back
Top Bottom