Kama ni Urafiki basi Bora Uishe

Kama ni Urafiki basi Bora Uishe

Real Deal

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Posts
280
Reaction score
114
Habari wanaJF

Hii habari ni ya kweli na imenitokea si mara moja bali ni mara kadhaa na hadi sasa inaniogopesha kuwasiliana na marafiki zangu wa zamani.

Wakati nasoma sekondari na chuo nilikuwa na marafiki wengi (hawa ni wale niliokuwa nao kwa karibu kwa kiasi fulani, ila sio ile kwa saaaaana). Baada ya masomo ya sekondari wengi nilipoteza mawasiliano na baada ya chuo pia wengi nilipoteza mwasailiano nao. Miaka ya hivi karibuni hasa baada ya FB, LinkedIn na mitandao mingine ya kijamii nimekuwa na mawasiliano na hwa rafiki zangu wa zamani.

Kitu kinachonichanganya ni kuwa karibu asilimia 50% ya hawa marafiki wa zamani baada ya kubadilishana namba na mara nyingi mimi ndo huwa nawapigia kwanza na kuongea na "ku-catch up on what happened during that respective period" huwa nabaini kuwa wote wanakazi tena nzuri tuu na title kubwa kubwa. Cha ajabu ni kwamba eidha siku hiyo hiyo au baada ya siku moja napata simu kutoka kwa jamaa anataka nimkopeshe/nimsaidie kiasi fulani cha hela kati ya sh 10,000 hadi laki kadhaa.

Huwa najiuliza hivi katika jumuia zao na kuwa wamefanya kazi na kuishi miaka yote hiyo hawana watu wa karibu wanaoweza kuwakopa? hadi mimi nimpigie simu ndo aweze kunikopa na kutimiza mahitaji yake? Hii sii elewi kabisa na naomba wana jukwaa maoni yenu kama ni hali ya kawaida au kunatatizo eidha kwangu mimi au hao marafiki zangu wa zamani?

Ushauri na uzoefu tafadhari
 
aisee kama huna wambie huna kama unayo wape si case hata matajiri huwa wanakopa.
 
labda huwa unajisifia mafanikio makubwa mbele zao ndo sababu wanaona wakikupigia watahisi wanajipendekeza kwako
 
Labda wanafikiri maisha yako afadhali kuliko yao. Wanataka wakutumie. Marafiki wanaoweka pesa mbele si marafiki wema. Mwisho utakua ugomvi wa madeni. Hachana nao. Binadam wanachange ndugu, yule ulie muona mwema mwanzo leo ni hatari. Wengi wanakazi nzuri lakini mambazi pia. Na wanawake maofficer lakini wanajiuza, tamaa tu. Hawatosheki.
 
Sio walipaji hao, so hawana wa kuwakopesha!
 
We unadhani ukinipgia mie cmu then ukaanza kujitapa kwamba unafanya kazi BOT au tanapa,unadhani ntaacha kukukopa?
 
Hela zao zina kazi za maendeleo, za kwako ndo za kukopwa waendeshee vitu visivyo vya msingi.

Dawa yao wakishamaliza kujisifia na kazi zao nzuri waambie im hussling nisaidieni mchongo. Wakikopa waambie nimetoka kununua tiles za kiitaliano hapa sina hali. Nimeishiwa kama mzungu. Afu muunganishie kumuuliza ule mchongo wa kazi.
 
Labda wanafikiri maisha yako afadhali kuliko yao. Wanataka wakutumie. Marafiki wanaoweka pesa mbele si marafiki wema. Mwisho utakua ugomvi wa madeni. Hachana nao. Binadam wanachange ndugu, yule ulie muona mwema mwanzo leo ni hatari. Wengi wanakazi nzuri lakini mambazi pia. Na wanawake maofficer lakini wanajiuza, tamaa tu. Hawatosheki.

Anyway nadhani unapoint hapo, acha maisha yasonge mbele, ila inasikitisha kuona jinsi binadamu tunavyobadilika =, ndo ukubwa na mjukumu lakini.
 
Ata kwangu jambo hilo hutokea best

Pole, ila yalisha semwa "kua uyaone" ule urafiki wa wakati ule nadhani ulikuwa ni wa kitoto, sasa tumeshakua na ndo tunaonekana uhalisia wetu.
 
Just like me mpaka nafikiri kuchange sim card.. Kwanini kila mtu asife na shida zake mwenyewe??
 
Back
Top Bottom