Kama ni kweli, basi NECTA ni janga

Kama ni kweli, basi NECTA ni janga

Shida inatokea wapi ? We hujui kuwa NECTA hawatoi cheti kwa division zero?
 
Na huyu aliyepata cheti cha mwenzie na kuwa nacho ofisini, kakipataje na kwa mamlaka ya nani, na yeye hata akae na nyaraka ya serikali isiyomuhusu?
Kakipataje tutajua badae, ILA aweke mambo hadharani kwanza.
 
Nauliza tu, hivi tokea lini NECTA wanatoa vyeti kwa waliopata division zero? Maana nimesikia na ninaamini asilimia kubwa baadhi yetu tumesikia hii kauli ya kuwa kuna mtu ana cheti cha mwenzie kipo ofisini kwake kinachoonyesha kapata division zero.

Basi kama ni kweli kuna mtu ana cheti halafu alipata zero huu ni uhaini.

Sitetei mtu kwenye huu uzi wangu ila kauli ya Mzee mwenzangu ndio imenichanganya kidogo.
Ndio utajua kama ni kweli au sio kweli mtu awe na vyeti ambacho kimoja kinaonesha alipata sufuri!, na kingine cha kupewa!, nimeshindwa kuiamini hiyo stori kwa kuwa mtu akipata sufuri hapewagi cheti. Shida nyingine ni kwa mtuhumiwa, swala la kusoma halinaga siri. kama kweli alisoma na kuhitimu si atoe mavyeti tu bila kusema chochote atakuwa amemaliza biashara na hizi habari za mtu kupata sifuri halafu akawa na cheti zitajiishia zenyewe na watu wakafanya mengine. Lakini ukiona kimya hiki katika hili inawezekana kuna ukweli ingawa haujakaa kama tunavyosikia.
 
Back
Top Bottom